Al-Jazeera walipoenda undercover na kufanya kazi za Polisi wa Tanzania (Video ya Mauaji ya Albino)

I can't believe my eyes. It is one thing to hear of it, and another thing to see it...
Kama walivo sema wengine hapo juu ni lack of political will tu. Ingekua kuna advocacy kubwa kwenye maswala kama haya, na watenge budget for their protection, reporting system na vinginevyo mbona tuneona decrease in demand? Hawajataka tu
 
...Hakuna ushahidi unaoonyesha bungeni kuna watu "educated", hata wa kimazingira. Badala yake, kuna watu waliohudhuria shule.

...Wengi tumehudhuria shule tu. Hatukujifunza, ndio maana haya na mengine mengi yanafanyika, na baadhi wanashangaa inakuwaje.

Great point kuwa educated na kumiliki vyeti ni vitu viwili tofauti. But again kuwa educated maana yake nini? Wangapi wako educated lakini wanadeal bado na imani (ukristu, uislamu, ubudha nk)? Na sasa si kuna sijui freemasons na wengine ambao ni rasmu; but also imani ambazo hazijawa documented na zinazotokana na evil (Satan if u like), si lazima ziwepo? Bahati mbaya education tunayopata si ya kiimani bali ni ya kifact zaidi; au mawazo ya kimagharibi zaidi.

Hivyo as long as kuna good, evils pia zinakuwepo. Na waamuni wa both good n evil ni binadamu bila kujali how educated they r in elimu dunia.
 
Chanzo cha watu kuamini ushirikina ni nini?
Huyu Bwana Mtangazaji anasema kisa watu are "uneducated". Hivi Tanzania wale waliosoma hawaamini ushirikina?
Manake nimekumbuka kisa cha Chenge na ungaunga Bungeni

In my view; chanzo cha kuamini ushirikina ni sawa na chanzo cha kuamini uwepo wa Mungu; "searching in vain for explaination".
 
What I also found interesting ni kuwa mwandishi wa Nigeria ndiye aliyeenda anda cover; ukiona Vick Mtetema sidhani kama kuna waandishi wetu wakubwa ambao waliwahi kwenda kuzama kama alivyofanya huyu jamaa. Au hatuna vifaa na uwezo - hadi tuwezeshwe?

Yeah, tukiwezeshwa tunaweza! Bottomline, is we don't have the will to do it. How could we go about doing it?


huyu mwandishi ni mnigeria aisee..sisi waandishi etu wanafanya nini? lol!! hawana ujasiri au hawana elimu

Ndugu zangu, tusisahau wadanganyika…ooops sorry, I mean Watanganyika..hah..sorry again.. I meant.. Watanzania.. wote Tumelogwa.. yaani Ingawa uwezo wetu wa kufikiri ni mkubwa..lakini jamaa aliyetuloga ameufanya uwe unafikiri katika “Reverse order”.. yaani “kinyumenyume”..

Kwa mfano
  • mwandishi wa habari ambaye ni mzuri katika investigative journalism badala ya kutumia ujuzi wake kufanya kazi kama hiyo ya Aljazeera basi in Tanzania atatumia ujuzi huo kwa “reverse order” na kufuatilia kina Kanumba na Uwoya na kuandika habari kwenye gazeti la uwazi au atajifanya mpelelezi na kutuletea habari za majungu hapa JF…
  • Polisi mahiri badala ya kufuatilia majambazi atapoteza muda wake kwa “reverse order” na kukimbizana na Chadema…
  • Mwanasiasa mahiri badala ya kutetea wananchi na taifa lake ata “reverse order” na kutetea posho ya tumbo lake na changudoa kule dodoma..
  • Askari Traffic badala ya kufuatilia uvunjaji wa sheria atapoteza muda kufuatilia kama gari lina Jack, sticker za usalama barabara na Vibabaji…
  • Na mwisho baadhi ya viongozi wetu.. badala ya kuongoza .. kwenda mbele.. wataongoza in Reverse order… Yaani wao ndio watasubiri kuongozwa na mafisadi…
 
In my view; chanzo cha kuamini ushirikina ni sawa na chanzo cha kuamini uwepo wa Mungu; "searching in vain for explaination".

Nchi zilizoendelea kuna wimbi la watu kutoamini uwepo wa Mungu (na ushirikina) ndicho kinachopelekea hayo maendeleo?
 
Nchi zilizoendelea kuna wimbi la watu kutoamini uwepo wa Mungu (na ushirikina) ndicho kinachopelekea hayo maendeleo?

Maendeleo huchangiwa na factors nyingi sana, sipendi kuisolate moja; kwani hata neno lenyewe ni contextual. Lkn my point ni kwamba imani za kishirikina ziko deep sana; the only educated people ambao hawako prone nazo ni wasioamini kabisa juu ya supernatural (Mungu na Shetani). Wengi wetu, huamini juu ya Mungu, issue inakuja pale ambapo Mungu au anachelewa kujibu maombi yetu au hajibu kama tunavyopenda; so with desperation tunatafuta alternative kwa kuwafuata waganga ambao huongea na hutupa reassurance kwa kutuambia if u do this n that within a short period utaona matokeo.

Well huo ni mtazamo mmoja; mtu asiyeamini juu ya supernatural power, yeye atajitegemea yeye zaidi na natural being wengine (fellows, animals n plants) na environment kutackle the problems; SCIENCE.

Swali; nini maana ya kuwa educated?
 
S Katabalo(RIP) na J Muro walikusudia kuwa na uandishi wa habari wa namna hii, lakini kimbunga kimedeflect target kabisa. S Kubenea anajaribu lakini ndo vile tena! Vick alianza katika hili hopefully kwamba polisi wangemfuata, wakashirikiana nae, wakamlinda na hatimae kubaini ukweli kwa dhati kabisa. Wapi bana. Haya sasa, ndugu zetu walemavu wa ngozi, chukueni mkanda huo andamaneni mkimwambia PM kuwa Mwema ameshindwa kuwatendea yaliyo mema.
 
Nakumbuka wakati wa kesi za wale Watanzania maskini walioshatkiwa kwa tuhuma za mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi, huko Shinyanga katika utetezi wao walisema walikuwa wakitumwa na 'Mwarabu' kwa ahadi ya mamilioni ya fedha. Nway lakini pia, kama baadhi yao walikiri, kwa nini upelelezi haukwenda extra miles kujua soko lao na kitu gani hasa kilisababisha wao kujua kuwa kuna demand, hivyo inahitajika supply. Yu wapi yule mwarabu na mamilioni yake! Yako wapi matokeo ya kura za maoni juu ya mauaji ya albino iliyowahi kufanyika, I guess 2009? Yule Mbunge wa CCM kutokea Kigoma ambaye hata mamla za chama wilaya na mkoa zilisema kuwa watu wa kijijini kwake wana suspect anahusika na mauaji haya, yuko wapi leo kama si bungeni na wale wote walioleta madai hayo kushambuliwa badala ya tuhuma kuchunguzwa? Wanajuana.

Mwarabu!!!!!!Astakhafirullah!!!
 
Chanzo cha watu kuamini ushirikina ni nini?

Huyu Bwana Mtangazaji anasema kisa watu are "uneducated". Hivi Tanzania wale waliosoma hawaamini ushirikina?

Manake nimekumbuka kisa cha Chenge na ungaunga Bungeni
Serikali yote ilikwenda kwa Babu
 
Lowasa,Sumaye, Sofia Simba, Nimrod Mkono, Lukuvi, Tayson, Mrema, Wote ni Washirikina!!. wote walikwenda kwa Babu kutibiwa kishirikina wakati mganga mwenyewe hajathibitishwa na gvt
 
Mwanakiji,

Sisi tunasubiri kupewa misaada tu!!! Tatizo ni mfumo, mfumo wa serikali umeshafaynya idara zote za serikali na watumishi wote kusubiri kuambiwa nini kifanyike!!!

Police is full of failures toka top to the bottom!! Hakuna creativity! Ukienda pale central police ukawaona wapelelezi, utachoka!! Wote wanasubiri kuambiwa nn wafanye!!

Juzi tume-graduate kuwa omba omba wa kwanza africa kwa furaha tena tukiongezea na kibwagizo cha 50 years of independecy!!
 
Great point kuwa educated na kumiliki vyeti ni vitu viwili tofauti. But again kuwa educated maana yake nini? Wangapi wako educated lakini wanadeal bado na imani (ukristu, uislamu, ubudha nk)? Na sasa si kuna sijui freemasons na wengine ambao ni rasmu; but also imani ambazo hazijawa documented na zinazotokana na evil (Satan if u like), si lazima ziwepo? Bahati mbaya education tunayopata si ya kiimani bali ni ya kifact zaidi; au mawazo ya kimagharibi zaidi.
...Unajua, kuelimika ni kama kuokolewa toka kwenye ujinga, ambao ungeshikilia maisha yako yawe kwenye hali duni isiyo na maendeleo. Bahati nzuri, kuelimika hakuhitaji uende darasani kwa kiasi kikubwa. Wapo wasio na elimu rasmi kubwa -kwa maana wamefika hadi darasa la saba hivi- lakini wameelimika kuliko waliopata digrii ya udaktari wa falsafa.

...Moja ya vitu vilivyo wasaidia watu kuondokana na ushirikina ni elimu rasmi pamoja na mafundisho ya dini, zote.

...Ni fikra zangu kwamba, imani ya ushirikina imeshamiri kwa mtu au eneo ambalo elimu rasmi, mafundisho ya dini na maendeleo ya kimaisha ni duni. Wapo wanaoamini kwamba hawawezi kuendelea bila kufanya ushirikina, kwakuwa hawafahamua au na hawaamini kuwa kuna kukosa na kupata katika dunia. Aidha, hawajui kuwa mafanikio ya maana hutokana na juhudi ya kazi na kutumia maarifa.
 
Lowasa,Sumaye, Sofia Simba, Nimrod Mkono, Lukuvi, Tayson, Mrema, Wote ni Washirikina!!. wote walikwenda kwa Babu kutibiwa kishirikina wakati mganga mwenyewe hajathibitishwa na gvt
...Matumizi ya mitishamba si ushirikina. Babu anatibu baadhi ya watu kwa mtishamba, kuthibitishwa na serikali ni mjadala mwingine. Mbona unakunywa juisi iliyotengenezwa na nanihii, imepimwa na kuthibitishwa na serikali? Nisieleweke vibaya. Siungi mkono matumizi ya vitu visivyothibishwa, ila, ukweli ni kuwa, tunatumia vingi tu.

...Nadhani unafahamu dawa kadhaa za malaria zinatoka na herbs.
 
Nawashangaa sana, toka lini Polisi wakawa waandishi wa habari?

Tuna waandishi wengi humu wengine wa vijarida vya kwenye mitandao, walikuwa wapi? wao kazi yao kuandika udaku tu?

Jifunzeni kutoka Al Jazeera, hata Riz Khan walimchukuwa kwa uwezo wake, namtaja huyu kwa sababu alisifiwa mpaka na Mkapa (Mwandishi wa zamani) na aliwaponda waandishi wa Tanzania, kumbe Mkapa alikuwa sahihi, leo ndio nimeyajua, nilikuwa namshangaa.
 
Tatizo hao police wanaogopa chama tawala bila kujijua kama hawapo kwa maslai ya chama wamesima kama serikal na wala sio chama na wanaongoza watanzania wala sio CCM,CUF,CHADEMA nk.Wanaogopa kufanya kazi zao kwa umakin kwakuwafichia makucha hao wa2 waliokosa utu Police wabadilike lasivyo kila hii hali ya kujichukulia upo juu ya sheria aitoisha tz wa2 watazid kufanya maovu wakiwa na uhakika hamna atakae wachukulia hatua .
 
I can't believe my eyes. It is one thing to hear of it, and another thing to see it...
Kama walivo sema wengine hapo juu ni lack of political will tu. Ingekua kuna advocacy kubwa kwenye maswala kama haya, na watenge budget for their protection, reporting system na vinginevyo mbona tuneona decrease in demand? Hawajataka tu

Fedha zote zinasubiri sherehe za Uhuru
 
Tatizo hao police wanaogopa chama tawala bila kujijua kama hawapo kwa maslai ya chama wamesima kama serikal na wala sio chama na wanaongoza watanzania wala sio CCM,CUF,CHADEMA .Wanaogopa kufanya kazi zao kwa umakin kwakuwafichia makucha hao wa2 waliokosa utu Police wabadilike lasivyo kila hii hali ya kujichukulia upo juu ya sheria aitoisha tz wa2 watazid kufanya maovu wakiwa na uhakika hamna atakae wachukulia hatua .
"Aisifuye Mvua Imemnyea"
Naamini sasa watu wanapoambiwa lazima CCM itoke madarakani ili nchi ianze kusonga mbele wataelewa.mfumo wetu wa viongozi ni washiriki wakubwa sana wa mambo ya kishirikina,na ukiangalia uhusiano uliopo kati ya umasikini na ushirikina ni mkubwa.palipo na ushirikina pana umaskini mkubwa.na ndio maana raisi wetu hajui kwa nini nchi yetu ni masikini wa kutupwa.Jibu leo limepatikana ni "ushirikina"asilimia kubwa sana ya Viongozi wa CCM ni washirikina ukitaka kulijua hilo subiri uchaguzi utakapowadia.FF yuko wapi/ huwa anatetea upuuzi sana humu jamvini.
 
Back
Top Bottom