Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,921
- 30,267
MAHOJIANO NA MOHAMED VALL WA AL JEZEERA 2007
Jana nilikuwa naangalia Al Jazeera yanayotokea Gaza mara nikamuona mtangazaji wa Al Jazeera, Mohamed Vall anatangaza habari za vita hivi.
Mohamed Vall akanikumbusha mahojiano tuliyofanya nyumbani kwangu Dar es Salaam na Tanga kati ya mwaka wa 2007 na 2008.
Hiki ni kisa cha kipekee katika maisha yangu ya kuhojiwa na vyombo vya habari.
Al Jazeera ilituma waandishi wake wakiongozwa na Mohamed Vall kuja Tanzania kufanya naamini ''documentary.''
Walinipigia simu Tanga na kuniuliza kama naweza kuja Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano au wao wanifate Tanga.
Nilikuja Dar es Salaam na wakafika nyumbani kwangu asubuhi kwa kuangalia mandhari ya nyumba yangu na kuipanga kwa namna waitakayo wao kwa ajili ya kufanya kipindi.
Kwa ufupi walibadilisha muonekano wa ukumbi wangu waliporidhika wakanifahamisha kuwa watarejea usiku kwa ajili ya mahojiano.
Mohamed Vall ndiye aliyenihoji na tulifanya kipindi cha takriban saa moja.
Tulizungumza kitu gani?
Al Jazeera walitaka kujua historia ya Waislam wa Tanzania.
Katika team yao kulikuwa na kijana mmoja yeye aliniambia kuwa ni Mtanzania na akinifahamu kwa miaka mingi sote tukiwa watoto Kinondoni.
Kwa hakika sura yake haikuwa si ngeni na alikuwa na muonekana wa Kisomali.
Nakumbuka kipindi kizima nilichokuwa nahojiwa mwanangu wa kwanza alikuwa kasimama mbele yangu sawasawa na mimi akiniangalia.
Sijui nani alimtuma kunikalia mbele yangu lakini kwa namna ya ajabu sana yeye akawa kama kioo cha mimi kujiangalia na kujitathmini.
Kila nilivyokuwa nikizungumza nilikuwa namuona kwa jicho langu la pemebeni akitabasamu na wakati mwingine akitingisha kichwa kama kusema, ''Ahsante,'' au ''Hakika,'' nk.
Sura ya mwanangu ilikuwa kama vile inaniambia kuwa maneno yangu niliyokuwa nasema yalikuwa mazuri yamamfurahisha.
Mwanangu alinikumbusha siku nafanya mtihani wa English Oral, Mtihani wa Cambridge 1970.
Siku zile tulikuwa tukitihaniwa Kiingereza kwa kuzungumza mbali na mtihani wa kawaida wa kujibu maswali kwa kuandika.
Mwalimu wangu wa English na Literature Miss Menez, msichana wa Kigoa siku ile alikuwa katika chumba cha mtihani na alikuwa kaweka kiti chake sawa na mimi uso kaukunja ananiangalia na kunisikiliza.
Nakumbuka jana yake wanafunzi wa Literature alituita na kutuambia kuwa ikiwa sisi wanafunzi wake hatukupata Merit Pass yaani First Class basi na yeye pia atakuwa kafeli mtihani.
Nilipokuwa najibu maswali nilimuona Miss Menez, wanafunzi sie kwa utundu wetu tulimpa jina, ''Lanky,'' kwa ajili ya urefu na wembamba wake.
Sijua nani alikwenda kumuambia.
Siku moja darasani akatuambia huku akicheka kuwa anajua jina tulilompa.
''So my golden class you have given me a nickname...''
Turejee kwa Al Jazeera.
Kila mazungumzo yalivyokuwa yanasonga mbele nilikuwa nawaona watu wa Al Jazeera ambao kwa hakika ndiyo walikuwa hadhira yangu walikuwa kama vile wanazamishwa na yale niliyokuwa nasema.
Sura zao ukiziangalia walikuwa wanafuatilia kila sentensi niliyokuwa naitoa.
Historia ya Waislam na uhuru wa Tanganyika na yaliyotokea baada ya uhuru siku zote imekuwa kisa cha kupendeza na kuvutia kusikiliza.
Mohamed Vall nakumbuka swali lake la mwisho aliniambia kuwa kesho alikuwa na mahojiano na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu.
Je, anaweza kuninukuu na kumuuliza maswali Rais kutafuta ukweli kwa yale niliyozungumza?
Jibu langu lilikuwa anaweza.
Baada ya kumaliza mahojiano haya wale vijana walinipongeza wakisemea kipindi kilikuwa kizuri sana.
Nilisubiri kwa muda mrefu kipindi kirushwe.
Hakikurushwa.
Baadae zikanifikia taarifa kuwa baada ya kumaliza kufanya vipindi Tanzania Bara walikwenda Zanzibar kwa mahijoano mengine.
Tape zao za vipindi vyote walivyofanya Tanzania Bara na Visiwani vilipotea hotelini Zanzibar.
Baada ya mwaka mmoja hivi Mohamed Vall na wenzake walirudi tena Tanzania na wakaja Tanga kwa mahojiano.
Sijui nini kilitokea safari hii.
Kipindi hakijaenda hewani hadi leo.
Picha ya mwisho ni mahoajiano na Mohamed Vall Tanga, Bombo Area 2008 nyingine ni mahojiano Dar es Salaam, Masaki 2007.