Al-Jazeera walipoenda undercover na kufanya kazi za Polisi wa Tanzania (Video ya Mauaji ya Albino)

Mkuu, hatukuhitaji kwasababu Polisi wanajua fika nani anahusika na njia zipi wanatumia..kwa kifupi hatuna Jeshi la Polisi kwa ajili ya kulinda usalama wa raia bali kulinda wenye fedha na walio madarakani..natamania AJE waaabishe hawa mafisadi wasaini mikataba ya kinyonyaji..
 
Mwanakijiji,
Ushirikina kama unafanyika mpaka ofisi nyeti kabisa, then ni kitu kigumu sana kukikabili kama Taifa maana hatuna hiyo will ya kukabiliana na tatizo. Pengine wanao neemeka pia wapo ndani ya ofisi hizo hizo.
Unless we change our belief systems, we are wasting our time. Tusubiri kuendelea kuabishwa na Aljazeera na wengine wengi.
 
Al-Jazeera big Up!
Richard Mgamba big up!
Yote hii ni kuonyesha kuwa nchi yetu HAINAGA JESHI LA POLISI ila ina POLISI WA CHAMA CHA MAJAMBAZI ambao kazi yao ni kutwa kucha WAKIPAMBANA NA VYAMA VYA UPINZANI kwa visingizio vya Intelijensia. HII NI AIBU KUBWA KWA JESHI LA POLISI TANZANIA!

Iwapo chombo cha habari kama Al-Jazeera wameweza kuingia Tanzania na kufanya kazi ya UPEPELEZI WA HALI YA JUU kama huu kwa kutumia mikono BANDIA YA ALBINO(Plastic) na wakaweza kuwanasa wahusika wa janga hili,Polisi wetu wanashindwa nini???.

Tunataka IGP Mwema ajifunze kwa AL-JAZEERA na ikiwezekana apeleke baadhi ya MAJANGU wake wakapate SEMINA ELEKEZI toka Al-Jazeera! Si ndiyo wanayoita POLISI JAMII???

Chonde chonde IGP Mwema,AL-Jazeera wamekurahisishia kazi. Mwambie na PM wako Pinda aache kulialia mbele za Watanzania kuhusu mauaji ya Albino anatakiwa achukue maamuzi magumu kama walivo onyesha Al-Jazeera.

Once again big up Al-Jazeera.
 
Mkuu, hatukuhitaji kwasababu Polisi wanajua fika nani anahusika na njia zipi wanatumia..kwa kifupi hatuna Jeshi la Polisi kwa ajili ya kulinda usalama wa raia bali kulinda wenye fedha na walio madarakani..natamania AJE waaabishe hawa mafisadi wasaini mikataba ya kinyonyaji..
Ili tuwe na jeshi la polisi lazima kwanza tumtafute Rais!Al-Jaeera wamefanya kazi ya Polisi sasa tutafute chombo kingine kufanya kazi ya Rais.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Chanzo cha watu kuamini ushirikina ni nini?

Huyu Bwana Mtangazaji anasema kisa watu are "uneducated". Hivi Tanzania wale waliosoma hawaamini ushirikina?

Manake nimekumbuka kisa cha Chenge na ungaunga Bungeni
 
Mhh, ama kweli. Poleni ndugu zangu Albino! Sio Mungu aliyewapenda zaidi kwa wale mliotangulia kupitia vifo vya aibu kiasi hiki.

Wengi wanaweza kushauri kuliombea taifa hili. Nakumbuka miaka kadhaa rafiki zangu huko ughaibuni waliniambia Waafrika tunapenda sana kuomba, na jinsi tunavyozidi kuomba shida ndipo zinavyozidi kuongezeka. Ukiangali haya maneno yana mantiki; sio kuondoa uwepo wa Mungu, ila ni Waafrika kutotekeleza wajibu wao na kupenda tu kupokea vilivyotayari. Tunaacha kuweka mikakati na mipango yakukabiliana na maisha/majanga/n.k tunabakia kusema kuwa tunamwachia Mungu. Ndio maana utawasikia viongozi wa dini na serikali wakihitaji taifa kuombewa. Kwanini wasiinuke na kumshukuru Mungu kwa akili alizowapa, nchi aliyowapa na vitendea kazi alivyowapa; na kunuia kwa nia moja kuingia kazini?

Huenda Mungu hasikilizi blabla! Inatupasa kufanya home-work
 
Our police force is a total failure! Sometimes I do not blame them at all. Its the system which they are operating under. When you work under the guidance of someone else who only issue Al -Shabab threats when he hears people want to air their views to the government, you know we have a long way to go. The solution is to separate the police force from the executive interference. These people operate according to what they are being told to do. Again when you look at what they earn, its makes you shudder if at all they are have any motivation to work hard. That is the situation we find ourselves in 50 years after independence!
 
Maujai ya Albino mapambano yake ni ya uongo mtupu viongozi anajidai wanalia uongo, kiundani wanayakubali,tunakumbuka mwandishi a BBC alifichua mengi serikali ilichukua hatua gani? wao ni washirikina wakubwa, wanatoa vibali leo utashangaa kuona jijini au manispaa katikati kuna duara la ushirikina serikaliminaangalia kazi yao kukamata wananchi wanojitafutia kwa kuuza yeboyebo
 
Me nachotaka kuuliza serikali inafanya nini?mbona kwenye sherehe na posho tunawasikia saaana ila kwenye mambo mazito wote kimya kweli ndo miaka 50 ya uhuru kweli big up aljazeer
 
Ukifikiria kwa makini nchi yetu ilipofikia sasa hivi lazima machozi yakutoke.
 
Hongera al-Jazeera!

Ningetamani kuona pia TV zetu zikienda mbele na kufanya vitu kama hivi lakini yanaoendelea kwenye vyumba vya habari vya Tv ( na vyombo vingine) vya habari hapa kwetu sio vitu vya msingi sana.

Tv zetu zimejaa Thamthilia za kila mamna ambazo pamoja na yaliyomo kutokuw aya madili ya kitanzania, lakini hayamsaidii mtazamanji wa kawaida na jamii kwa jumla.

ukiangalia Tv zetu hasa siku za jumapili ni kikwazo kwetu wengine. kutwa nzima inakatika hakuna taarifa ya habari isipokuwa kinachjofanyika ni kubadili tamthlia moja kwenda nyingine zikiambatana na muziki!

wakati hayo yakiendelea nawapongeza al-jazeera lakini kwetu sisi hakuna jitihada za makusudi tunaozfanya kuwasiadia albino. mwezi uliopita mahakama kuu kanda ya Bukoba iliyokuw ikeindesha vikao vyake wilayani Biharamulo ilimwacha mtuhumiwa aliyekuwa akikabiliwa na shitaka la jaribi la kumwua albino bi mariam Stanford wa wilaya ngara

kilichotokea kama inavyofanyika kwenye kesi nyingine zinazosimamiwa na ofisi ya mwendesha mashitaka wa serikali DPP ni akuandaa ushahdi mbovu na hivyo kushindwa katia kesi nyingi inazofikisha mahakamani

pamoja na jitihada za al-jazeera, wauaji haw awa albino wataendelea kutamba kwa kuwa wadau wakuu, polisi na waendesha mahsitaka wanashindwa kutekeleza wajibu wao na kuwaacha wanaofanya vitendo hivyo kutamba mitaani
 
Ours is a Police Force and force is all what they know.

Going under cover to unearth Albino killers is of no interest, intelijensia yao ni kujua maandamano ya Chadema yataambatana na Al shabaab ama la.
 
What I also found interesting ni kuwa mwandishi wa Nigeria ndiye aliyeenda anda cover; ukiona Vick Mtetema sidhani kama kuna waandishi wetu wakubwa ambao waliwahi kwenda kuzama kama alivyofanya huyu jamaa. Au hatuna vifaa na uwezo - hadi tuwezeshwe?
Yeah, tukiwezeshwa tunaweza! Bottomline, is we don't have the will to do it. How could we go about doing it?
 
Huo ni mwanzo ni mwanzo tu kwa Aljazeera kufichua mambo mengi kwa bara hili, ni bora serikali ikabadilika na vyombo vyake vya ulinzi vikaanza kufanya kazi badala ya siasa. Suluhu kwa nchi yetu ni kubadili mfumo mzima wa utawala na hili lawezekana kwa kuiondoa ccm madarakani la sivyo kelele zetu ni bure.
 
Back
Top Bottom