AJALI za Barabarani: Tatizo sio Polisi, Serikali oneni AIBU rekebisheni miundombinu! barabara ni mbovu sana

Mtemi mpambalioto

JF-Expert Member
Aug 23, 2015
3,277
7,424
Kuna Barabara ni tokea alivyojenga MWALIMU NYERERE, je mnategemea zitakuwa ni bora kwa maisha ya sasa?
Mfano barabara ya kutoka Morogoro mpaka dodoma yaan kila mita 100 kuna shimo! njia nzima ni mashimo tuuu je hizi ajali mnalaumu Askari wa usalama.barabarani?

nimeona barabara ya bagamoyo hasa kuanzia mapinga kwenda bagamoyo mjini watu wanakwepa mashimo bila tahadhari wanaleta ajali sana!
serikali oneni aibu kwenye hili jamani

HEBU TUWEKE PICHA YA BARABARA MBOVU HAPA tuwaonyeshe serikali kuwa chanzo ni hiki
 
Mwanza -Musoma kwa baba wa taifa mashimo lami imechoka tangu miaka ya 70.TANROADS kazi kwenu
 
Kuna Barabara ni tokea alivyojenga MWALIMU NYERERE, je mnategemea zitakuwa ni bora kwa maisha ya sasa?
Mfano barabara ya kutoka Morogoro mpaka dodoma yaan kila mita 100 kuna shimo! njia nzima ni mashimo tuuu je hizi ajali mnalaumu Askari wa usalama.barabarani?

nimeona barabara ya bagamoyo hasa kuanzia mapinga kwenda bagamoyo mjini watu wanakwepa mashimo bila tahadhari wanaleta ajali sana!
serikali oneni aibu kwenye hili jamani

HEBU TUWEKE PICHA YA BARABARA MBOVU HAPA tuwaonyeshe serikali kuwa chanzo ni hiki
Kwa Utafiti upi uliofanya wewe kwamba Barabara mbovu ndio chanzo Cha maajali ya Kila siku?

Dunia nzima inajua ni uzembe wa kibinadamu wewe unaleta stori za barabara
 
Barabara zetu zinachangia sana ajali Kiongozi! Unawezakuta sehemu nyingi daraja jembamba na Kila mmoja anamfanyia timing mwenzake kwenye kupita! Au Kuna seheme kwenye mikima panagitajika climbing lanes ila hakuna. Sasa unakutana na convoy ya malori yanapanga na 10 kph. Mtu anaona taabu kuongozana nao akitoka anakutana na kitu mbele! Serikali iboreshe barabara. Mfano pia tulipota barabara ya Moshi -Arusha,Ile barabara ni takriban umbali wa kilometre 80. Ingestahili kabisa 4 lanes hadi Moshi,kama ilivyoanzia Arusha hadi Tengeru,lengo kukwepa kukutana Kwa kupishana. Kila upande wapite kivyao Tena wakiwa ni line2. Hii itapunguza sana ajali!
 
Wakuu muwe na shukrani, mapungufu yapo lakini tunajitahidi sana, katika nchi afrika mashariki ina barabara nzuri ni tanzania, umewahi kudrive hata kwenda hapo uganda? unaijua barabara ya mutukula-masaka?.
 
Back
Top Bottom