Mjadala: Ubovu wa Barabara za Mtaani kwako: Je, viongozi wanawajibika?

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
1705937493346.jpeg

Hali ya Barabara za Mtaani kwako ikoje na je, Viongozi wa eneo lako na Mamlaka nyingine zinazohusika zimewajibikaje kuondoa changamoto zilizojitokeza?

Ungana nasi katika Mjadala wa XSpaces ya JamiiForums hapo Januari 25, 2024 kuanzia Saa 10:00 jioni hadi 12: 00 jioni Kifukia mjadala bofya https://jamii.app/XSpaces2024


MAONI YA WADAU

SEFEEMNH:
Chanika -Zingiziwa B huku hata huo muda hawana, sio Diwani wala Mwenyekiti wa Mtaa "as if" hawapo

NSHAMBAKWETU: Kibamba CCM kuelekea Mji Mpya barabara ni janga sijui hata kama tuna Viongozi huku kwetu, au kama wapo basi masaa yote wamelala nyumbani hawajui hata barabara za Mitaa yao zikoje. Ila tutakutana siku moja

AUTOMOTIVE_SEATCOVERS: Kuna Barabara moja hivi ni kubwa sana huko Kimara kuelekea Matosa. Barabara ni mbovu wameifanya ya kupigia Kampeni. Maana Uchaguzi ukikaribia wanakwangua halafu wanajaza Kifusi cha Vumbi, mvua ikinyesha mara moja tuu mabonde barabara nzima

GOODLUCK PAUL: Miundombinu ya Barabarani ni mibovu haswa barabara za Kisongo ni mbovu mno. Ipo barabara inayotoka Kona ya ATZ inaelekea Kijiji kimoja kinaitwa Lemnguru ikinyesha manyunyu tu hata Pikipiki haipiti

CANDY CUTHBET: Hakuna anayewajibika, ndio kwanza Mbunge wetu Bonnah Kamoli alihamisha Ofisi zake huku Mtaani kwetu Segerea sababu ya Ubovu wa Barabara. Yaani Tabata Segerea Mwisho Barabara hatuna ni hovyo.

Uchaguzi ukifika wanajaza Vifusi kisha vinaachwa hapo visambaratike na kuongeza maporomoko

PULLY PHILLIP: Hapana! Nipo Iringa Kata ya Mkwawa, Mtaa Bwawani B, barabara imeharibika toka mvua ya Mwaka juzi hadi mvua ya Mwaka huu imekuta barabara hivyo hivyo hakuna gari wala boda kupita

PRUDE TWESGETO JEMSON: Serikali ipi hiyo? Hizo barabara kubwa hovyo, hizi ndogo ndogo ndiyo kabisa. Cha zaidi wanaweka Vifusi na kupitisha greda Uchaguzi ukikaribia

Bady Savage: Mara nyingi ukienda kwenye Ofisi wanakwambia wanaohusika na hizi Barabara ni TARURA

Katika eneo ambalo ninaishi kuanzia Baracuda mpaka Bonyokwa hakuna Barabara ya Mtaa ambayo utapita na usipate shida. Barabara nyingi huku hazipiti kirahisi

Nancy: Mimi ningependa kujua ni nani huwa anahusika kwenye suala la kuzibua Mitaro. Tumeona kipindi hiki cha Mvua Barabara nyingi zimepata Changamoto na ukiuliza unaambiwa Mitaro haifanyi kazi

Je, hatuna utaratibu wa kurekebisha hii Mitaro mara kwa mara ukizingatia tahadhari ya Mvua ilitolewa muda mrefu lakini bado kila wakati wa Mvua bado tunarudi kwenye Changamoto ileile

Taji Liundi: Mimi nimekuwa nikifahamu kwenye Nchi za wenzetu kwasababu wao ni walipa kodi hawatarajii kwamba watakutana na Shimo Barabarani na Dereva anaweza kushtaki Mamlaka hata pale anapokuta Taa za Barabarani hazifanyi kazi vizuri

Hapo ndipo mahali Uwajibikaji kwa wenzetu ulipofikia. Tumeona Suala la Mitaro kuziba, tuangalie Kiwango cha Barabara zenyewe (Ni vumbi au Lami) na tunaona baadhi ya Barabara zenye Lami zimetengenezwa kwa Kiwango ambacho hakijaridhisha, Mvua kidogo inaharibika

Taji Liundi: Umesema suala la kuzingatia Mabadiliko ya TabiaNchi. Tunaona haya Mafuriko sio kwetu tu hata Newyork na Dubai nako yametokea

Wakazi wa maeneo haya wanachukua jitihada za kipekee kwasababu wanajua ni jambo linalojitokeza kila Mwaka hivyo maeneo yao hubaki salama bila kuathiriwa na Maji

Kalikenye: Huku kwetu Mwanagati ni kama jamaa wanasubiri Uchaguzi ufike waje kukwanguakwangua tu kuturubuni ili wapigiwe kura. Msidhani sisi ni vilaza hivyo.

Viongozi wetu eleweni kuwa nasi ni walipa kodi kama maeneo mengine wanakopewa huduma stahiki.

Miundombinu bora (maji, barabara na umeme) huchochea maendeleo ya eneo husika. Inakwaza sana kuchukuliwa poa na waliopewa mamlaka

Brazameni: Tuna changamoto kubwa, huyo jamaa wa TARURA anasemaje kwenye uwekaji kiwango duni cha lami ambayo haidumu hata miaka 5 au mvua zikinyesha kidogo barabara zinatoboka kama vile iliwekwa karatasi tu?

Wakandarasi hawa wanafanya makusudi kuchezea pesa za Umma? Nani awajibike?

allynyuni1987: Hii ni barabara ya kutoka Chanika mjini kwenda Chanika Zingiziwa, hii njia ina changamoto kubwa sana. Hali ndio kama hivi inavyoonekana.


Kawiche Samwel: Kama Mwanza mjini tu hapa wilaya ya Nyamagana barabara za mitaa hazipitiki kabisa mpaka unawaza huu mkoa uliitwa Jiji kwa sababu ipi mazingira ya wananchi kutoka na kwenda kwenye shughuli zao ni tatizo. Basi wapulize pembe wenye kujua thamani ya barabara za mitaa tukazitengeneze.

Maige Nyala: Ni kweli Kuna kutokuwajika kukubwa saana Kwa viongozi tuliowachagua, morogoro mtaa wa kihonda azimio Kuna Kero ya kivuko Kwa watembea Kwa miguu kutoka ng'ambo ya relief ya mwendo Kasi kuja upande wa pili,nishida kuvuka daraja linalotumika ni lakupitishia maji Toka kilolo.

Multiverse King: Kuna mtindo wanaufanya sasa wa kuchonga barabara baada ya kuona kelele zimekuwa nyingi, hali hii inapelekea barabara kuteleza sana wakati wa mvua na Maji kukaa katika barabara na magari makubwa yakipita basi zikikauka zinabaki na mabonde ambayo siyo rafiki kwa magari ya chini

Lakini pia Kipindupindu kimekuwa tishio kuna Stendi nyingi sana hapa Mjini ambazo zipo katika Kiwango cha vumbi, ila hazitunzwi kabisa, zinamatope, mashimo, mabonde na biashara za chakula zinaendelea kufanyia, hii itatuletea mlipuko wa kipindupindu

Willy: TARURA kwenye kujenga barabara zao huwa wanatumia vigezo gani? Kwasababu unakuta kuna Barabara ambazo hazina watu wengi na kutumiwa na watu wengi zinawekewa lami, ila barabara zenye watu wengi na kuweza kuhudumia watu wengi zinaachwa.

Mfano ni barabara ya Goigi Mbezi Juu kwenda kutokea Barababara ya Goba imewekwa lami lakini haiwa tu wengi kama ile ya Makonde inayokwenda Baraza la Mitihani kuunga barabara ya Goba

John Haramba: Moja ya changamoto kubwa katika suala la ubovu wa barabara chanzo ni kukoseka kwa uwajibikaji kwa Viongozi kuanzia ngazi ya juu hadi chini

Nchi kama Indonesia ambapo nimebahatika kufika kuna Uwajibikaji wa kiwango cha juu na ndio maana hata suala la uchumi wao kukua limefanikiwa

Watanzania tunatakiwa kubadilika na kuruhusu kuwajibika, tofauti na hapo tutaendelea kuwasaidia wenzetu wanapiga hatua, barabara ni kero kubwa hasa Mitaani
 
Wameagiza vietee mpya LC300 ili wasisikie maumivu ya potholes. Hiyo ndo solution yao.
 
Viongozi wengi hawawajibiki ipasavyo suala la miundombinu ya barabara mtaani. Danadana zinakuwa nyingi sana wakazi wa maeneo husika tunapojaribu kuhoji.

Ila pia kuna viongozi wengi wanakuwa wabinafsi, utakuta kiongozi mkubwa mtaani mamlaka zinahakikisha kuwa barabara/njia ya kuelekea kwake inafanyiwa maboresho na kuishia kwake. Mfano hapo jogoo kuna kiongozi mmoja aliwekewa lami siku chache baada ya kuteuliwa kuwa waziri.

Pia nakumbuka mwaka 2020 wakati wa kampeni, barabara ya kuingia uwanja wa Tanganyika Packers kupitia stendi ya Kawe ilifanyiwa matengenezo kwasababu tu CCM walikuwa wanakuja kufanya mkutano ule wa nileteeni Gwajima, baada ya hapo wakaitelekeza. Nenda sasa hivi ukaangalie njia za kuingia na kutoka uone zilivyo mbovu na hakuna anayejali.
 
Huko Chole Road, Masaki, Haile Selasie yenyewe barabara zina mashimo na wanaishi wao huko viongozi

Ova
 
Njia kuelekea makabe ais3 hali ni mbaya na mvua hizi sijui
Huko kuna mkandarasi anajenga sahv anakaribia mwaka wa 2 hakuna anachofanya

Ova
 
Back
Top Bottom