Barabara ya Dar- Mwanza kuwa njia sita na muarobaini wa ajali za barabarani

Undava King

JF-Expert Member
Aug 11, 2017
3,107
5,158
Kwa kipindi kirefu tumekuwa na tatizo sugu la ajali za barabarani chanzo kikuu kikiwa ni uendeshaji usiofuata taratibu na kanuni za usalama barabarani pamoja na ubovu au uchakavu wa vyombo vya moto huku tukifumbia jicho suala la utoshelevu na ubora wa miundombinu yetu.

Ajali za barabarani haziwezi epukika kamwe kwa njia moja tu ya kudili na madereva hili wasifanye makosa ya barabarani na kuhakiki uhalali wa leseni zao.

Ajali za barabarani zitaepukika pale tutakapo kiri kwa dhamiri zetu kama taifa kuwa tuna miundombinu duni na hafifu isiyoendana au kukidhi uhitaji wa wakati tulionao hivi sasa.

Ni ukweli usiopingika kwa takwimu kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye barabara zenye ubora duni lakini pia mtandao mdogo wa barabara za lami ukilinganisha na nchi zinazotuzunguka hapa Afrika ya mashariki na Afrika pia, kama taifa lenye amani na wingi wa maliasili hili si jambo la kujivunia.

Kiuhalisia ni wazi kuwa imefikia wakati barabara kuu ya Dar es salaam mpaka Mwanza itanuliwe na kuwa njia sita (6) kwani imeshazidiwa na idadi ya magari pamoja na watumiaji wengine wa barabara hii.

Ambapo ndani ya njia sita (6) hizo; njia mbili (2) zitumike kama njia za malori, njia mbili zingine (2) Mabasi na njia mbili zilizobakia (2) Magari madogo.

Hii itasaidia kuepusha overtaking zinazosababisha ajali za mara kwa mara katika barabara hii ambayo ina-accommodate kwa wakati mmoja mamia ya malori ya mizigo(yanayoendeshwa taratibu),mabasi ya masafa marefu (yanayohitaji kufika kwa wakati),magari madogo(yanayohitaji kuokoa muda na kufika haraka), bajaji, pikipiki, n.k ndani ya lanes 2 pekee ni vurugu mechi na kuweka maisha ya mtumiaji rehani licha ya umuhimu mkubwa wa barabara hii katika uchumi wa nchi.

Naamini kama serikali iliamua kufunga mkanda na ikaweza kujenga reli ya kisasa ya matrilioni ya shilingi kwa manufaa mapana ya uchumi wa nchi haiwezi kushindwa pia kulisimamia hili na likatekelezeka.

Ukweli ni kuwa suala hili la upanuzi wa barabara hii ambayo ni kitovu cha uchumi wetu alijapewa kipaumbele kinachostahili na serikali yetu pengine kwa kuchelea kuwa kwa kuwa tutakuwa na reli mpya basi pengine hatutokuwa na uhitaji wa barabara ya namna hii kwa wakati huu.

Hili linaonekana wazi katika utekelezaji wa kusuasua wa barabara ya njia nane ya Dar to Kibaha lakini pia utafutaji wa mwekezaji binafsi wa njia nne za pembeni ya zile mbili zilizopo sasa kwa njia ya Kibaha to Morogoro,

Kwa maoni yangu nilitamani serikali ilisimamie hili kwa rasilimali na nguvu zake yenyewe japo sikatai uwekezaji binafsi ila katika barabara hii umuhimu wake katika uchumi wetu ni mkubwa na unapaswa kuzingatiwa.

Idadi ya watu,idadi ya magari ya abiria na mizigo inazidi kuongezeka siku hadi siku huku miundombinu ikibakia ile ile na inaendelea kuzidiwa,

Huku ikionekana dhahiri kuwa serikali ina kasi ndogo na pengine inasuasua katika ujenzi wa barabara za lami kwa wakati na kuendana na uhitaji.

Mfano jiji la Mwanza lina uhitaji ulio dhahiri katika upanuzi wa barabara zake kuu kutoka njia mbili za hivi sasa hadi nne ndiyo kipaumbele na tiba ya foleni kubwa ya magari katika barabara zake muhimu lakini cha kushangaza itachukua karne mpaka serikali ichukue hatua katika hili.
 
Mchawi pesa tu mkuu unajua kwanza Lami Dar to Mwanza Imekamilika juzi tu 2014-2015 hapo mwanzo kulikua na vipande vingi tu kwaiyo sasa Ni mwendo wa kuziba viraka na mashimo tu jla ndoto za 4 au 6 way bado mapema sana kuziota tunawalaumu tu bure viongozi ila bajet yake Miradi kama yote itabidi isimame kwa miaka 3-5 Bajeti yetu Apeche Alolo

Jana tu nimepita iyo njia kuna kiraka wanaziba pale Tinde kama nusu KM ivi unaingia kwenye vumbi
 
Wazo zuri mtoa mada ila kuwa na barabara sita sio muhimu sana,kinachotakiwa ni kuwa na barabara moja ila ijengwe kwa viwango mkuu, nitatoa mifano miwili hapa (ndani ya SADC),Zambia wana T2 inatoka nakonde hadi kapiri mposhi ilikua inaitwa barabara ya kwenda kuzimu, ila sasa inajengwa na imeingia chinsali ni super na ajali zitapungua sana,A3 ndani ya Botswana kutoka Kasane hadi Francis Town ni super na ni njia moja tu, na elewa barabara hii ina zaidi ya 300km za mbuga ya wanyama, ipo super na very rare wanyama kugongwa na magari (science imetumika kuzuia hili),our own T1 ina only 50km za mbuga ya wanyama na tunapoteza almost wanyama 700 wanaogongwa (tungeweza kuzuia hili ila politics ni nyingi mno),tunahitaji barabara bora na sio utitiri wa lines ambazo ni vurugu tu.
 
Kweli mkuu, kwa mwendo huu wa kunyata itachukua muda sana pengine ndoto itakamilishwa na vitukuu.
Uwezo upo ila ufisadi mwingi. Akiingia rais mwenye maono miaka 10 anaweza kufanya hili. Kimsingi barabara zote za kwenye mikoani eg Dar- Tanga- Arusha, Dar-Morogoro-Iringa-Mbeya nk zilitakiwa ziwe njia nne zote. Ukiambiwa fedha za serikali zinaishia kwenye matumizi yasiyo na lazima na zile zinazopigwa unaweza ukazimia.
 
Majizi mengi sana hayawezi kufanya hili yanaiba tu kwanza
Hii nchi kama zilivyo nchi masikini zingine za Afrika ni nchi zenye mifumo mibovu na duni katika ukusanyaji mapato,usimamizi na uthibiti ufujaji fedha za walipa kodi wake.
 
Sio kwa Tanzania hii, ambapo adhabu ya ufisadi ni kuambiwa stupid na kuhubiriwa kwamba pesa unazoiba hautazikwa nazo.
"Nani atakuwa wa kwanza kumfunga paka kengele?"

Hapo ndipo unapotambua kuwa taifa hili liwe na ustawi linahitaji kuwa na kiongozi mwenye maono na uthubutu.
 
Uwezo upo ila ufisadi mwingi. Akiingia rais mwenye maono miaka 10 anaweza kufanya hili. Kimsingi barabara zote za kwenye mikoani eg Dar- Tanga- Arusha, Dar-Morogoro-Iringa-Mbeya nk zilitakiwa ziwe njia nne zote. Ukiambiwa fedha za serikali zinaishia kwenye matumizi yasiyo na lazima na zile zinazopigwa unaweza ukazimia.
Mfumo wetu wa kudhibiti na kusimamia miradi bado unatoa fursa kubwa na mianya mingi ya upigaji lakini pia watanzania kiujumla hawana uzalendo na nchi yao vinginevyo haya yasingeendelea kutokea.

Pengine ni ufahamu wetu kuhusu mstakabali wa taifa na maisha yetu ndiyo mdogo kwa kuwa hata kielimu bado tumeachwa nyuma.
 
Back
Top Bottom