Ajali ya Meli: SMZ yakataa misaada ya VODACOM

Ajali ya Meli: SMZ yakataa misaada ya VODACOM

ninakubaliana na msimamo huu. sometimes tunatakiwa kuwaonyesha wanaodhani kuwa wanaweza kununua utu wetu kwa pesa zao wanajidanganya! na kwa taarifa yao huyo malaya wao atatembea na laana ya waliochukizwa na umalaya wao hadi kifo!shame on them!

Indeed mkuu this is what is called in corporate governance, Corporate social responsibility. These large corporations needs to respect and understand their responsibility to the society. SMZ imeonyesha njia kuwa hizi kampuni kubwa zituheshimu sisi maskini walalahoi na sio kuleta dharau wakati taifa liko katika simanzi. Binafsi nawaomba SMZ waendelee na msimamo huo huo ili kampuni zengize zijifunze kuwa responsible to the community. Kuna siku utatokea msiba mwengine haya makampuni makubwa yanaweza yasiheshimu hata sekunde ya muda kwa kudai wao wako busy sana!!!!
 
Unatumia makalio kukumbuka! CCM ilizindua kampeni siku ya Jumamosi! Tukio lilitokea Usiku wa kuamkia Jumapili!
Hivi unapata faida gani kupotosha kwa makusudi habari iliyoshuhudiwa dunia nzima? Meli iliondoka bandarini Zanzibar Ijumaa jioni na ajali imetokea usiku wa kuamukia Jumamosi. Kwanini kwenye mkutano Mkapa alisimama kwa dk moja kama tukio lilitokea usiku wa jumapili shame on you.
 
FYI--

Sponsors wa Jamii Forum ni TIGO an AIRTEL. Thats why the non-siasa topic is not moved. Nyie wote ni wanafki tu. Mnatumia mgongo wa SMZ and Msiba to advance your own agenda.
 
quote_icon.png
By NGULI Mpige marufuku na misaada ya CCM pia walifanya uzinduzi wa kampeni siku ya janga.
Nikisikia SMZ wamepokea msaada wa CCM najua ni wanafiki naendelea na mtandao wa Voda kama kawaida.
 
kwan ajali imetokea muda gani na miss vodacom imeanza saa ngapi?
 
FYI--

Sponsors wa Jamii Forum ni TIGO an AIRTEL. Thats why the non-siasa topic is not moved. Nyie wote ni wanafki tu. Mnatumia mgongo wa SMZ and Msiba to advance your own agenda.
Agenda gani? pengine wewe ndiye mwenye agenda maadam hilo lipo kichwani mwako...Miss tanzania ni mwakilishi wa Taifa na msiba huu ni wa taifa iweje lisiwe kosa kwa Voda na waandaaji kuendelea kufanya tamasha hili? wangepoteza kitu gani kuahirisha wewe nambie maanake nijuavyo pombe haziozi tena inavyokaa sana ndio inapendeza zaidi. Au huo Ukumbi waliokwisha kodisha?.. ni kiasi gani kwa shirika kama Voda ambalo linaingiza mabillioni kila siku washindwe kuvumilia.
 
<br />
<br />
Acha kuuliza majibu,kwani siku zote anapeperusha bendera ya nchi gani?

Jibu swali la Mkandara na sio kuleta siasa. Jana niliuliza swali kama hilo kuwa navyofahamu Tanzania ni nchi inayojumuisha (Tanzania bara na Zanzibar) na anayeshinda hupewa bendera ya Tanzania kwenda kuiwakilisha. Sasa tuulizane kweli kulikuwa na uhalali gani wa kufanya sherehe za Miss Tanzania Jumamosi wakati taifa likiwa katika simanzi ya msiba??? Au aliyechaguliwa ni MISS VODACOM?
 
Jibu swali la Mkandara na sio kuleta siasa. Jana niliuliza swali kama hilo kuwa navyofahamu Tanzania ni nchi inayojumuisha (Tanzania bara na Zanzibar) na anayeshinda hupewa bendera ya Tanzania kwenda kuiwakilisha. Sasa tuulizane kweli kulikuwa na uhalali gani wa kufanya sherehe za Miss Tanzania Jumamosi wakati taifa likiwa katika simanzi ya msiba??? Au aliyechaguliwa ni MISS VODACOM TANZANIA?
Haswaaa tena angekuwa Miss Voda wala tusingepiga kelele lakini mijitu humu imeshuparia utadhani inalipwa na Voda. hili shirika nadhani linahitaji mtu makini sana ktk public relation inaonyesha sehemu hiyo linapwaya!
 
Sijui Yesu atashuka lini kutuokoa toka hii minyororo ya fikra. Yani tunailaumu voda! STUPID kabisa! Kuanzia Zitto hadi vidampa. Huwezi ukafikiri kwa ufinyu hivi. Wanaokufa migodini, barabarani, kwa ukimwi, malaria n.k nao ni voda chanzo?
 
Wasiisusie tu, waachane nayo kabisa. Hii nchi kila mwenyenacho anafanya anavyotaka akidhani kuwa hakuna atakayemgusa. Vodacom wakataliwe pia huku bara, tuhamasishane wote ili wajue thamani ya utu.

Kumbukeni Vodacom ni kampuni la kibiashara. Au mnalifananisha na shirika la umma ambalo mfanyakazi asipokuwepo kazini, au siku ikipita bila kufanya kazi watu wanalipwa tu. Nawapa tano vodacom kwa vile ajali nyingine ni uzembe tu wala si janga la kitaifa.
 
Sijui Yesu atashuka lini kutuokoa toka hii minyororo ya fikra. Yani tunailaumu voda! STUPID kabisa! Kuanzia Zitto hadi vidampa. Huwezi ukafikiri kwa ufinyu hivi. Wanaokufa migodini, barabarani, kwa ukimwi, malaria n.k nao ni voda chanzo?
Haya sasa ama kweli - Miafrika Ndivyo Tulivyo!
 
Sijui Yesu atashuka lini kutuokoa toka hii minyororo ya fikra. Yani tunailaumu voda! STUPID kabisa! Kuanzia Zitto hadi vidampa. Huwezi ukafikiri kwa ufinyu hivi. Wanaokufa migodini, barabarani, kwa ukimwi, malaria n.k nao ni voda chanzo?

You are the one who is stupid tena nafikiri unatumia masaburi kufikiri unashindwa kung'amua kuwa walichokifanya voda kinadhihirisha jinsi makampuni makubwa yanavyowadharau walalahoi wa nchi hii. Anapokufa mkubwa wa serikali utawaona voda na mashati meusi wamejipanga kwa mamilioni kwenda kuwaona wafiwa na viongozi wake. Wamekufa walalahoi wanapiga debe na kunywa mvinyo na kuulizana are you guys enjoying tell how is that sensible??????

Tukiwaachia voda basi hata Barrick Gold nao wasilalamikiwe kwani wanafanya biashara na kulipa kodi hawaitaji kuendeleza maeneo wanayoyachimba dhahabu wala kuchimba visima vijijini. Pia tusiwalaumu TBL na wala wasitoe misaada kwa jamii kama kuchimba visima na kupeleka watoto shule. It is part of their responsibility of investing in our country. Jiulize kati yako na Zitto pamoja na sie wengine nani walikuwa sahihi katika hili jambo!!!
 
Hiyo ndiyo dalili ya mtu anayetumia masaburi kufikiria. Hivi vodacom waliwatuma mjaze meli mpaka ikainamia upande mmoja kabla hata ya kuondoka!! Ebu tuache upumbavu na uvivu wa kufikiri. Kifo ni kifo tu wala tusijifanye eti tumepata uchungu sana kiasi cha kususia watu au makampuni.
 
Weye akili yako haina akili:- Mashindano yamefanyika saa 21 usiku hadi saa 00 usiku wa kuamkia tarehe 11 septemba. Meli imezama usiku wa manane wa kuamkia septemba 11. kwa akili yako hao washindani wangetambua vipi baadaye usiku huo kuna meli itazama? hata kama walifahamu kuwa kuna meli imezama weye kwa akili yako unafikiri katika muda mfupi uli wangetambua vipi uzito wa tatizo? Zaidi ya yote VODA hawaandai hayo mashindano bali ni kampuni ya Rhina intertainment!!
Jamani acheni kulea majungu hayana tija!!!
Sahihisho meli imezama usiku wa kuamukia J'mosi sept 10 mashindano yamefanyika J'mosi jioni usiku wa kuamukia J'pili.
 
Twendeni taratibu jamani.. matusi ya nini tena? Hoja zijengwe, zitetewe na zikataliwe. Kwa kuitana majina hatufanyi hoja ziwe na nguvu zaidi inaonekana tunalazimisha. Binafsi nimeilewa vizuri kabisa hoja ya wale wanaotaka Vodacom iwajibishwe. Sikubaliani nayo lakini nimeielewa na ninaiheshimu. Lakini kutokubaliana nayo haina maana ninaamini Vodacom wamefanya kitu kizuri na siamini kabisa Miss Tanzania ingeendelea. Binafsi - na nilisema hili mwanzoni - ingeahirishwa japo kwa wiki moja kuonesha sensitivity kwa wahanga. Lakini suala la kuonesha sensitivity si tatizo la Vodacom tu. Ni tatizo la msingi ambalo tunalo kwani kwa kadiri kwamba ajali hizo zinawatokea watu wengine ni wachache wanajali sana.

Swali langu je viongozi wetu wako sensitive kwa hizi ajali? Well.. tunaridhika na wao kutoa rambirambi na pole na kutembea na suti nyeusi kuliko kuonesha kutoridhishwa na mipango yao ya usalama wa vyombo vya usafiri? Kwamba wakija na kutoa rambirambi na kuonesha nyuso za huzuni tunaguswa zaidi?
 
Hiyo ndiyo dalili ya mtu anayetumia masaburi kufikiria. Hivi vodacom waliwatuma mjaze meli mpaka ikainamia upande mmoja kabla hata ya kuondoka!! Ebu tuache upumbavu na uvivu wa kufikiri. Kifo ni kifo tu wala tusijifanye eti tumepata uchungu sana kiasi cha kususia watu au makampuni.
JF, kumbe kuna pumba wengi kama hii si pumba tu! Eti nae kaona kachangia point
 
Vodacom have none but themselves to blame. Tabia za kukosa utu na utambuzi wa kujua mazingira haya yanafaa au hayafai kufanya jambo fulani ndio matokeo yake ni hayo. Wewe unasema Vodacom ni kama wadhamini hivyo hawana kosa inaonekana wewe umetumwa kuwatetea Vodacom na hivyo basi tukurudishe na maswali haya yafuatayo ukawaulize vodacom kama wadhamini:-
a. Je wao kama wadhamini wakuu wa Miss Tanzania walitumia njia zipi kujaribu kuzuia shindano hilo lisifanyike wakijua nchi ilikuwa imeingia katika msiba? Kwani wao kama wadhamini wana uwezo wa kutishia kujitoa, kushinikiza liahirishwe na hata kufutwa ikibidi kwani wao ni wadhamini wakuu na hivyo pesa nyingi zilizotumika kuandaa Miss Tanzania zitatoka au zimetoka kwao.

b. Watueleze inakuwaje wakati Rais Wetu Jakaya Kikwete na Rais Dr Shein wakiwa katika sura za huzuni mkurugenzi wenu Ms Mwamvita makamba alikuwa akicheka na kufurahi tu katika kipindi hichi cha msiba?

c. Je wamejuaje kama wafiwa walikuwa wanahitaji hayo mashuka na vitu vyengine walivyovipeleka waliwauliza?

Binafsi Vodacom, TBC na Media nyenginezo deserve the brunt huwezi kudai ati makubaliano na mikataba any contract is subject to eventualities there is no such a thing a fixed contract msitudanganye hapa!!!!

Hongera sana Dr Shein tunajua serikali yako iko makini na uamuzi mliofanya ni sahihi kabisa kwa watu wenye kuleta mzaha wakati taifa liko katika msiba.


Hapo ndo uwezo wako wa kufikiri na kujenga hoja ulipoishia?
 
Kitu pekee Wazanzibari wanazuiwa kufanya ni kulaumu serikali yao. Wanaaminishwa kuwa tatizo n vodacom na hivyo hasira zao zinaelekezwa huko. Sijui bank atawasaidia.

Mkuu ahsante umeiweka vizuri sana, nashangaa watu hawataki kutambui mbinu hii
 
Back
Top Bottom