Ajali ya Meli: SMZ yakataa misaada ya VODACOM

Ajali ya Meli: SMZ yakataa misaada ya VODACOM

Kwa kuanzia mi napiga chini line ya voda na modem yao.<br />
Mtu akiwa na line ya voda pia inabidi nifikirie kwanza kabla ya kumpigia!
<br />
<br />



Ingekuwa Busara hiyo Hasira yako ungeielekezea Serikali ya Zanzibar kuliko Vodacom,usishughulike na Matawi,shughulika na Mzizi wa Tatizo!! Vodacom ni Wawekezaji,matatizo ya nchi yetu hayawahusu moja kwa moja,wakitoa rambirambi ni Hisani tu!!
 
na CCM walikuwa wanakata mauno ya kufungua kampeni mbona wamechuniwa? nidham ya uoga au unafiki? ukweli unaosikitisha ni kwamba voda wataendelea kumake super profit hata watu wakichukia hadi wakajinyonga. uzembe wa serikali ya zanzibar kama wapo serious boat wakati inajaza mara mbili ya uwezo wake wenyewe walikuwa wapi? hii ni sawa na kuzaa watoto 10 wakati unajua huna uwezo wa kuwatunza kisha unaanza kuwachukia ndugu kwamba hawakusaidii kuwalea.
 
Jamani, tatizo ni vodacom kudhamini miss Tz au kuna jingine? Naona kama kuna element ya udini kwani wenzetu wamekuwa wakipinga mashandano ya mamiss kwa muda mrefu. Nachelea kuhisi kuwa hisia yao zimepitishiwa tu kwenye ajali.
 
Ni kweli walichokifanya voda si kizuri na wanapaswa kujifunza kutokana na hilo!kv vp wote wenye laini za voda tususie kwa siku tatu ili wajue kuwa tuko msibani.
 
Mkandara JF imedhihirisha in chachu ya mabadiliko.
Hapana mkuu wangu ujinga mtupu kwani huyo Miss wenu huko aendako atabeba bendera ya Voda au ya Taifa?
Mnaposhindwa kutazama vitu kwa upeo mpana zaidi ni dalili ya ufinyu..hizi ni chachu sawa na zile za Loliondo...
 
ninachokiona mimi humu ndani jamvi ni washindani wa vodacom ambao ni tigo, airtel na zantel wanajaribu kuichafua vodacom kwa kuwa wanashindwa kupambana nayo katika njia za kawaida. otherwise waende wakailaumu basata ambao ndio wadaaji wa shindano la miss tz, vodacom ni sponsors tu, hivyo hawapaswi kulaumiwa! kitu kingine cha muhimu ni kwamba nani alaumiwe yule aliyesababisha msiba utokee au yule ambae aliendelea kiufanya kazi wakati msiba unatokea?

Mkuu hapa haijalaumiwa voda bali imekataliwa msaada wake,kwa kukosa ubinaadamu na kudharau mila za nchi,na kwavile voda iliona biashara ni bora ili iingize faida zaidi basi ibakie na fedha zake izidi kunufaika.
 
Hili suala limenipa huzuni sana kwa kweli na sitoweza kuwalaumu wazanzibar kwa lolote lile.
Msiba ni wao wana haki yakuamua kama wao
 
Msiba ni wetu tumuombe mwenyezi mungu atujalie uvumilivu, upendo na moyo wa imani, na wala tusitumie msiba uliotukuta kupima upendo uliopo baina yetu na wengine, na wala sio kipindi cha kutaka hisani ya mtu kutusaidia kwa hili wala lile.
 
biye2009
.............Naunga mkono hoja,nadhani ni kati ya mambo machache ambayo nimekubaliana na wanzanzibar.....VODACOM wanapaswa wajifunze utu,kuendesha shindano la umalaya wakati tuna msiba mkubwa namna hii,sidhani kama ni haki...watu wenye hekima wanajua kuwa Miss Tanzania ni shindano la kutafuta wasichana wazuri watakao uzika kwa mapedeshee.....

Siyo Sahihi kuilaumu VODA kwani yenyewe haiendeshi hayo mashindano bali ni kampuni ya RHINO inayomilikiwa na Lundenga. kwa hiyo voda hawahusiki kwa namna yeyote ile!!!
Isitoshe, kama ni kuisusia VODA basi CCM nayo isusiwe kwani wakti wazanzibar wanaomboleza, CCM walikuwa wakinengua jukwaani huku wakifungua kampeni zao za kumuingiza fisadi mwingine bungeni!!!
 
Hapana mkuu wangu ujinga mtupu kwani huyo Miss wenu huko aendako atabeba bendera ya Voda au ya Taifa?
Mnaposhindwa kutazama vitu kwa upeo mpana zaidi ni dalili ya ufinyu..hizi ni chachu sawa na zile za Loliondo...

kwa nini unataka iweje? voda wasamehewe ili iweje?
kama kuna serikali imehusika hiyo nayo ni hoja lakini kusema VODA wako sahihi ni kutupoteza

WRONG +WRONG= WRONG

kwa hiyo hoja yako bado haina kichwa, sisi tutapiga hapo kwenye VODA waliotoa mavumba kwa maana nyingine waliwezesha
na hatakaye mpa huyo miss bendera siku anaenda nje ya nchi tunaye
sio kwamba anapochaguliwa tu ana beba bendera ya TAIFA bado tuna haki ya kumkatalia pia kwa sababu kapatikana siku ya msiba
 
biye2009

Siyo Sahihi kuilaumu VODA kwani yenyewe haiendeshi hayo mashindano bali ni kampuni ya RHINO inayomilikiwa na VODA. kwa hiyo voda hawahusiki kwa namna yeyote ile!!!
Isitoshe, kama ni kuisusia VODA basi CCM nayoisusiwe kwani wakti wazanzibar wanaombeleza wao CCM walikuwa wakinengua jukwaani huku wakifungua kampeni zao za kumuingiza fisadi mwingine bungeni!!!

you are so stupid my friend,
aisee
umeshindwa kuelewa kwamba hapo umeongelea kitu kimoja yaani VODA
 
As a matter of principle SMZ wako sahihi kabisa... Kama VODACOM waliona ni sawa kufanya sherehe za ulimbwende ilihali taifa lipo kwenye
msiba mzito hivi. Hii inaonesha serious lapse of judgement kwa upande wa Vodacom, hasa ukizingatia Director of Corporate affairs wake
binti Makamba, alichoose Miss Tanzania over msiba wa kitaifa. Maana alikuwa ni mmoja wa washereheshaji.

SMZ hailazimiki kupokea misaada isiyokua na utu ndani yake. Kama kampuni inadhania kwa vile ina financial muscle, basi inaweza kujifanya
kakakuona. Kwamba wakati wa msiba wa kitaifa inadhamini sherehe ya kitaifa, halafu hangover zikiwa&#305;sha ndio wanakuja navimisaada vyao.
Hii hata Mwalimu Nyerere angekuwepo angewaunga mkono SMZ kwa msimamo thabiti.

Mayor Giulliani baada ya shambulio la September 11, 2011, New York. Alikataa na kuurud&#305;sha msaada wa USD 10Million toka kwa Prince Walid al Saud wa Saudi Arabia, kwa kile ''alichokitafsiri'' kama ni kujaribu kujustify attacks kulikofanywa na Pr&#305;nce Walid, pale aliposema kuna haja ya U.S kutazama upya siasa zake za Mashariki ya Kati. Hakuwa amekosea, ila kwa kukosa utu na kuguswa na vifo vya maelfu ya watu wakati muafaka, alirudi na cheque yake arabuni.
 
ninakubaliana na msimamo huu. sometimes tunatakiwa kuwaonyesha wanaodhani kuwa wanaweza kununua utu wetu kwa pesa zao wanajidanganya! na kwa taarifa yao huyo malaya wao atatembea na laana ya waliochukizwa na umalaya wao hadi kifo!shame on them!
 
IMG_6959.JPG
 
Hivi unafahamu kinachofanyika katika mashindano ya umiss au unajaza post tu. Na kuhusu hiyo vita unayoisema, yes huwa wafanyabiashara wana vita za namna hiyo lakini ujuwe kuwa Zantel pia wanatumia facilities za vodacom katika kutoa huduma zao bara? Usiishi kwa hisia ishi kwa uhalisia, at least kampuni za simu ni miongoni mwa kampuni ambazo zina-public image isiyojinasibisha na tofauti za dini, kabila, umri wala utaifa. Kama ishu ni imani ya dini kwanini hawakususia before, pia je bara hakuna waislamu, mbona hawakutoa tangazo la kususia huduma? Nadhani hampati picture namna tatizo lilivyo-impact jamii ya kizanzibari. Ivi kweli kifo cha mtu mmoja katika familia kinafanana na vifo vya watu 18 kwa familia moja, tena karibu kila kaya. Je can you imagine kwamba familia hizi zitakuwa na nafasi ya kuangalia mashindano ambayo watu wanacheza, wanakunywa, wanaimba, yaani ni furaha tu?

Weye akili yako haina akili:- Mashindano yamefanyika saa 21 usiku hadi saa 00 usiku wa kuamkia tarehe 11 septemba. Meli imezama usiku wa manane wa kuamkia septemba 11. kwa akili yako hao washindani wangetambua vipi baadaye usiku huo kuna meli itazama? hata kama walifahamu kuwa kuna meli imezama weye kwa akili yako unafikiri katika muda mfupi uli wangetambua vipi uzito wa tatizo? Zaidi ya yote VODA hawaandai hayo mashindano bali ni kampuni ya Rhina intertainment!!
Jamani acheni kulea majungu hayana tija!!!
 
I had so much respect for Zitto Kabwe, but in this one kaka--u have lost it. Folks used to say how opportunistic he can be--and obviously his track record proves that. However, his flashes of brilliance sometimes can mistake him with a modern day real leader. At the end of the day, his desire of scoring political points at the dawn of the massive disaster had changed the tone of the conversation about the disaster. Sasa instead of talking about relief efforts and preventing future disasters. Wabongo tuko page ya 10 discussing about VodaCom.

The implications of all this is 1) Zitto Kabwe is a powerful of a talking head to actually drive the conversation 2)Watanzania are so stupid to fall for an opportunistic politician in Zitto. Siku ingine ukijiuliza kwa nini TZ bado tuko maskini, at least we have some answers.
 
Nimewauliza vizuri bado hamjibu kitu.. Huyo Miss wenu atabeba bendera ya Voda au Tanzania?..Kwa nini Ziotto asizungumzie uwakilishi huu na nyie mnashindwa kutazama mapana haya?
 
Ndo maana nilihoji vodacom wana kosa gani? Ni kweli hilo shindano lilikuwepo lakini voda walidhamini tu (na walikuwepo wadhamini wengine pia) na kama kawaida makubaliano ya udhamini yalifanyika muda mrefu uliopita na kila mdhamini alitimiza lililompasa kwa mujibu wa mikataba/makubaliano yao na waandaaji wa Miss Tanzania (Kamati ya Miss Tanzania inayoongozwa na Lundenga).

Kama ni lazima kulaumu, basi ilaumiwe Kamati ya Miss Tanzania ambao ndo wako licenced kuendesha shindano hilo.

Vodacom have none but themselves to blame. Tabia za kukosa utu na utambuzi wa kujua mazingira haya yanafaa au hayafai kufanya jambo fulani ndio matokeo yake ni hayo. Wewe unasema Vodacom ni kama wadhamini hivyo hawana kosa inaonekana wewe umetumwa kuwatetea Vodacom na hivyo basi tukurudishe na maswali haya yafuatayo ukawaulize vodacom kama wadhamini:-
a. Je wao kama wadhamini wakuu wa Miss Tanzania walitumia njia zipi kujaribu kuzuia shindano hilo lisifanyike wakijua nchi ilikuwa imeingia katika msiba? Kwani wao kama wadhamini wana uwezo wa kutishia kujitoa, kushinikiza liahirishwe na hata kufutwa ikibidi kwani wao ni wadhamini wakuu na hivyo pesa nyingi zilizotumika kuandaa Miss Tanzania zitatoka au zimetoka kwao.

b. Watueleze inakuwaje wakati Rais Wetu Jakaya Kikwete na Rais Dr Shein wakiwa katika sura za huzuni mkurugenzi wenu Ms Mwamvita makamba alikuwa akicheka na kufurahi tu katika kipindi hichi cha msiba?

c. Je wamejuaje kama wafiwa walikuwa wanahitaji hayo mashuka na vitu vyengine walivyovipeleka waliwauliza?

Binafsi Vodacom, TBC na Media nyenginezo deserve the brunt huwezi kudai ati makubaliano na mikataba any contract is subject to eventualities there is no such a thing a fixed contract msitudanganye hapa!!!!

Hongera sana Dr Shein tunajua serikali yako iko makini na uamuzi mliofanya ni sahihi kabisa kwa watu wenye kuleta mzaha wakati taifa liko katika msiba.
 
Back
Top Bottom