Hakika huku ndiko kutumia masaburi haswahaswa.
Biashara ya Vodacom ni kuuza airtime kwa maana kwamba voucher zitauzwa tu hata kama serikali nzima ya Tanzania ingekuwa imeangamia kwenye meli hiyo.
Mnaotumia masaburi hamjui kwamba ni abiria wangapi walioripoti ktuoka melini kwa kutumia simu za Vodacom. Hivyo kwenye maafa kama haya ndipo mawasiliano yanapotakiwa zaidi na ndipo Vodacom inatakiwa kufanya kazi overtime kuliko wakati wowote.
Kumbuka ajali kadhaa ambazo Vodacom imeokoa kwa wavuvi kupiga simu na kisha kuokolewa.
BIahsara ya urembo si fani ya Vodacom. Kudhamini urembo ni msaada tu toka Vodacom kama msaada huo kwa waliofiwa.
TUje kwenye suala la uzembe. Nyinyi wenyewe humu JF mmepiga kelele mapema kwamba vyombo vyote vya habari vilikuwa vinatangaza porojo zingine asubuhi siku ya tukio. Kama ni hivyo basi JF itangazwe kuwa ni chombo rasmi cha habari maana ndicho pekee kilichoripoti mapema wakati vingine viliripoti mnamo saa mbili asubuhi.
Ukitumia masaburi kufikiri utashindwa kubaini kuwa maandalizi ya Miss Tanzania si rahisi kuyazima ndani ya masaa machache yale. Kumbuka watu wameshakata tiketi toka kokote nchini na wako D'Salaam. Nasikia siku ya tukio umeme haukuwepo na hivyo generator zilikuwa zinawaka pale mliani City.
Hivyo, ni nani angegharamikia cost za kuahirisha shindano. Na waliotaka liahirishwe hadi lini maana maombolezo ni siku tatu. Na kumbuka kuwa uamuzi si wa Vodacom kwani japo Voda ni mdhamini mmoja lakini shindano lile linahusisha taasisi mbalimbali.
Kitu kingine tunatakiwa tukumbuke kuwa tumeanza kujenga utamaduni wa kufanya mambo ya hiari kama lazima. Hivi nani aliyetufundisha kwamba kumsaidia mtu imekuwa lazima. Hivi mimi hata jirani angu kama amekufa nikakataa kwenda msibani, ni kweli mnaweza kunishangaa, lakini nani alisema kwamba ni lazima nihudhunike.
Huyo, Zitto mnayemsema kuwa amezima simu yake inawezekana alikuwa bado mtoto mwaka 1994 ambapo Rwanda na Burudni zilipata maafa wakati marais wa nchi hizo waliotunguliwa na ndege. Kumbuka ndege ile ilikuwa imetokea Dar kama ile helikopta ya John Garang ilivyotokea Kampala. Kukawa na amombolezo.
Lakini wakati East Africa inaomboleza, wanyarwanda hapa Mwanza wakafanya sherehe kufurahis Habyarimana amekufa. Malecela akiwa waziri mkuu akawakamata. Nyerere akakemea kwamba kama wameshaangilia kufa kwa Abyarimana tatizo ni nini.
Binafsi ninapofiwa ninaona kuwa ni jukumu langu. Jirani aje asije ni uamuzi wake na sina sababu ya kunung'unika wakati tatiz limenifika. Hivyo mtu au kampuni kutoa misaada hata kama imekuwa ni mazoea bado ni hiari hata kama hatupendi.