Aina gani ya gari inafaa kuanzia maisha?

Gari yoyote ya Toyota inayotumia Engine 5A FE.
Sifa za gari la engine hiyo kwanza inadumu pili inafatumia mafuta vizuri tatu ukiwa jirani na mafundi wakati wanatengeneza mara kwa mara mwisho wa siku utaweza ata wewe mwenyewe kushusha injini na kuoverhaul yaani ni injini ambayo hautachukia kumiliki gari yaani utafurahi kumiliki gari maana kuanzia matumizi ya mafuta na kudumu utafurahi wastani wa matumizi ni 16km kwa lita na engine kama unazingatia service ni kilometres 500,000+ itadumu
1752347369952.png
 
Enheeeh wajomba naombeni msaada ni aina gani ya gari nafaa kuanzia maisha kama kijana mwenye mshahara wa 2M? Nilijichanga nikafikisha kiasi fulani nataman kupata gari ila nawaza aina ipi ya gari itafaa na yenye less service n maintenance.

Kuna fundi aliniambia Nissan Dualis nilipozifuatilia kidogo nizimie.

MSAADA
Tafuta 1nz fe.... yaani
TOYOTA
porte
Raum
Collora x
Spacio
Fielder
Rumion
Bb
Allex& runx
 
Enheeeh wajomba naombeni msaada ni aina gani ya gari nafaa kuanzia maisha kama kijana mwenye mshahara wa 2M? Nilijichanga nikafikisha kiasi fulani nataman kupata gari ila nawaza aina ipi ya gari itafaa na yenye less service n maintenance.

Kuna fundi aliniambia Nissan Dualis nilipozifuatilia kidogo nizimie.

MSAADA
Kuna haka kagari RR kanafaa sana, hska ka Rolls Royce bei yake ni chee.
 
Nunua gari lolote tu unalolipenda,ni raha sana kuendesha gari unalolipenda mwenyewe MUHIMU liwe zima na ikiwezekana usianzie la mkononi.

*Service gharama ni zilezile tu kwa wote wanaojali magari yao labda hayo ya kizungu.

*Usipokula mzinga,unaweza kaa hata 5yrs unafanya vitu vidogo vidogo tu kama utanunua gari zima na hauna safari nyingi.
 
Toyota Allex au RunX zenye Cc 1490 uhakika, faida yake hautakua kwenye midomo ya watu kama wanavyozisema IST ila gharama yake ya uendeshaji ni ileile ndogo kama IST
Anhaa! Services yake najua ni ndogo pia, nachukua kagari kadogo sababu sina route mingi mjini maana site kunazo gari za wafanyakazi
 
Nunua gari lolote tu unalolipenda,ni raha sana kuendesha gari unalolipenda mwenyewe MUHIMU liwe zima na ikiwezekana usianzie la mkononi.

*Service gharama ni zilezile tu kwa wote wanaojali magari yao labda hayo ya kizungu.

*Usipokula mzinga,unaweza kaa hata 5yrs unafanya vitu vidogo vidogo tu kama utanunua gari zima na hauna safari nyingi.
Asamte kwa ushauri wako nitafanya hivyo, natamani mpya pia
 
12M unataka gari showroom? Hapa labda ununue Used ambayo ipo kwenye hali nzuri ukichekecha vizuri unapata namba E za mwanzo
Ila ninauhakika 12M napata mkononi ambayo haina yowe, mfano nikienda showrooms za mliman city pale siwezi kosa, jana niliongea nao wakaniambia nifike ofisini
 
Anhaa! Services yake najua ni ndogo pia, nachukua kagari kadogo sababu sina route mingi mjini maana site kunazo gari za wafanyakazi
Toyota Alex au RunX zenye Cc 1490 ukipata hata ukitaka safari ya Dar Mwanza unaenda nayo fresh tu , na kwa misele ya town ni uhakika pia , binafsi naona ni gari nzuri mbadala wa IST , hizi IST zimeshakua kwenye midomo ya watu sana unakuta mtu hana hata baiskeli ila anaipondea, kwahiyo ili uwachanganye unatinga na Allex au RunX
 
Nimeona Body lake kanafanana na Allex.....kesho nitaenda kutafuta kwa vijana wenzangu ntaleta mrejesho.
 
Enheeeh wajomba naombeni msaada ni aina gani ya gari nafaa kuanzia maisha kama kijana mwenye mshahara wa 2M? Nilijichanga nikafikisha kiasi fulani nataman kupata gari ila nawaza aina ipi ya gari itafaa na yenye less service n maintenance.

Kuna fundi aliniambia Nissan Dualis nilipozifuatilia kidogo nizimie.

MSAADA
Lc 300 landcluiser VXR 2023
 
Back
Top Bottom