Kabembe
JF-Expert Member
- Feb 11, 2009
- 2,548
- 1,741
Wakuu naandika uzi huu nikiwa shuhuda wa ninalotaka kuongelea, inawezekana labda mimi ndio sijui mabadiliko ya mifumo ya kibenk haswa kwenye kufungua account mpya.
Nimewahi fungua account kadhaa kwenye bank tofauti hapo nyuma lakini hili nililolishuhudia NMB limenistua.
Mara zote unapofungua account mpya ya bank unatakiwa kuwa na kitambulisho cha taifa, kura , barua ya serikali ya mtaa au mwajiri na kiasi cha pesa au ada ya kufungulia account.
Kama wiki imepita nilienda kufungua account NMB bank, bahati nzuri desk la kufungulia account halikuwa na foleni kubwa, kulikuwa na wateja wanne tu mbele yangu.
Sasa kilichonishangaza ni kwamba ile ada ya kufungulia account (kulikuwa na ada ya 10,000/ kwa account ya Chap chap na 15,000/ kwa account ya saving) ,kwa kawaida bank nyingine ukishafungua wa wanakwambia uende counter uka-deposit hicho kiasi but surprisingly yule bank officer alikuwa akichukua pesa na kuweka mfukoni bila kukupa risiti au bank slip.
Yaani kachukua ya mteja wa kwanza kaweka mfukoni, wa pili , wa tatu , wa nne hadi yangu pia. Sasa mimi nikawa najiuliza kama nikinunua kilo ya sukari shs 2,500/ napewa risiti, iweje bank haitoi risiti au kwa nini ile ada isiwe deposited moja kwa moja kwa account then wao wakaikata?
Je, serikali inapataje kodi yake toka kwa ada ya kufungua account? Na je NMB wanalijua hili au ndio utaratibu wao? To me this is theft, yaani kama siibiwi mimi basi serikali inaibiwa.