Habar za muda huu!
Niende kwenye mada husika. Leo nilikuwa na jamaa yangu kuna sehemu tunaenda tupo na pikipiki, so jamaa akaona tupitie kwenye ATM atoe fedha kwa ajili ya mafuta.
Tunaingia kwenye ATM, hapo kwenye ATM kuna sheli ya mafuta lakini mabasi yanayoenda mikoani wanapita hapo kwa ajili ya kuchimba dawa na kupata huduma ya chakula.
Basi ile jamaa anataka kuingia ATM mlinzi akatumbia machine hazina fedha.
Basi kuangalia pembeni tukaona kuna NMB wakala jamaa akaona bora akatoe fedha kupitia NNB wakala.
Jamaa akaingia akatoa fedha na akapewa risiti kuwa ametoa fedha tayari na tukaingia sheli tukajaza mafuta hao tukasepa.
Tukiwa tumefika sehemu tunayoenda jamaa akawa ametoa simu yake kucheki anaoana kuna sms mbili za nmb kuwa ametoa fedha, sms zote zikawa zinaonyesha muda ni huo huo yaani hazikutofautina muda. Yaani kiujumla wake zote zinaonehsha saa 10: 10.
Jamaa akawa amenishirikisha kuwa mbona anaona sms mbili kwenye simu yake na zote za nmb?? Kiwango cha fedha cha kutoa kilikuwa sawa kwa sms zote mbili.
Nikamshauri jamaa aanglie salio kwenye simu yake na uzuri jamaa anatumia NMB app. Jamaa kuchek anakuta fedha imepungua, hapo tukaona basi huyu jamaa atakuwa amepigwa na hao wadada kwenye kutoa fedha kwa NMB wakala.
Tukashaurina tumalize kazi iliyotuleta then tupitie hiyo sehemu. Basi kazi ikaisha hao ikabidi tupitie hapo tulipotoa fedha. Tumefka dada kumuona jamaa kama akashtuka hivi, jamaa akatoa maelezo hapo, dada akamwambia ulitoa fedha saa ngapi? Jamaa akajibu, " nimetoa fedha saa 10.10" Dada akachukua machine yake akaanza kuangalia miamala ya muda huo.
Akaanza mara oooohhh we namba yako inaishia na ngap? Jamaa akamjibu inaishia 60. Dada akaanza mara hapa ngoja. Niangalie salio mara tena hapa miamala mbona ipo mitatu. Sisi tupo kimya. Mara dada akasema andika namba yako hapo kama nikikuta hasara nitakupigia ili urudishe hiyo fedha. Jamaa akaandika namba yake ya simu na hapo dada akatoa hiyo fedha. Jamaa akamuambia dada aitume hiyo fedha irudi kwenye account yake. Basi hao mimi na jamaa yangu tukasepa, tukiwa njiani tukawa tunajiuliza maswal kadhaa
1. Pale abiria wanashuka kupata chakula mfano ameenda kutoa fedha akapigwa inakuwaje?
2. Kama simu yako hujaunganisha na bank ili wawe wanakutumia sms ukitoa fedha au kuingiziwa fedha inakuwaje?
Tuweni makini sana na hawa wakala wa bank wakuu.