Aibu ya mwaka kwa Mwigulu

Aibu ya mwaka kwa Mwigulu

Status
Not open for further replies.
Mwigulu jamaa la magumashi anataka sasa kufukuza watu baada ya kukosa waangaliaji mechi ya simba jisommeeni wenyewe alivyooandika kada wa CCM Ndugu wana Jamavi,
Sina shaka habari za Iramba zimetawala sana jamvi jioni hii.
Hata hivyo, sakata hili limechukua sura mpya baada ya vijana 11 wa Chama Cha Mapinduzi wilayani hapa kuja na malalamiko mazito ya kudaiwa kurudisha fedha walizopewa kwa nyakati tofauti ili kuhamasisha ushiriki kwenye mechi ya Simba leo jioni.
Vijana hao wamewasilisha maelezo yao kwa mwenyekiti wa CCM wilaya, maelezo ambayo amepatiwa pia kiongozi mmoja wa CHADEMA hapa Kiomboi, na wanajiandaa pia kuyatoa kwenye media.
Akizungumza mmojawapo kati ya vijana hao anayejulikana kwa jina la Laurent Kiula amesema;
"Tuliitwa siku ya jumanne na aliekuwa mgombea wa Mkutano mkuu wa taifa bwana Daudi Amosi Madelu aliekuwa pamoja na aliewahi kuwa mwenyekiti wa Urughu, Simon Tyosela. Katika kikao hicho, Madelu alitupa kazi ya kuhamasisha mtaa hadi mtaa watu wahudhurie mechi ya Simba jumamosi (leo) badala ya mkutano wa wapinzani wetu CHADEMA na akatuahidi angetupa fedha ya kulifanikisha hilo. Alituomba tuwe 10, lakini baadae alituongezea dada mmoja kutoka Arusha tukawa 11. Siku ya Alhamisi, Madelu alituomba tukutane J.L.C Club iliyo nyuma ya ofic za CCM wilaya na akatuomba feedback. Tulimpa strategies zetu na akatutambulisha kwa dada huyo kutoka Arusha aitwae Scholastika, ambae ndie angekuwa master planner wetu. Alitupa Laki 3 kwa ajili ya mafuta, mabango na T'shirt, ingawa tulimwambia zisingetosha, na Tyosela alituongezea elfu 80. Madelu aliahidi kutupa zingine Ijumaa saa 4 asubuhi pamoja na posho zetu. Jioni ya Ijumaa, Tyosela alituomba tumpelekee T'shirt kadhaa kama ziko tayari, lakini tulimwambia kuwa tumecancel wazo la T'shirt kwa kuwa muda ulikuwa umeisha. Jumamosi asubuhi Madelu alituita Kisiriri Guest haraka. Tukiwa tunaendelea kujadiliana, alipigiwa simu na Mbunge ambae alimpa taarifa kuwa CHADEMA wanaanza mkutano sa kumi, hivyo tujipange vizuri na hapo ndipo tukajua kua mbunge ana taarifa. Cha ajabu, majira ya saa sita mchana, tulisikia matangazo kuwa mkutano wa CHADEMA unaanza saa 7 mchana!! Tulipompigia Mbunge, hakuwa anapatikana na ya Madelu hakuwa anapokea. Ilipofika saa 7, watu wengi walianza kufurika uwanjani kwenye mkutano wa CDM. Kilichonishangaza, mida ya saa 12 jioni tumeitwa na Tyosela na Madelu wakitutuhumu kuwa tulikuwa tunawasiliana na Kitila Mkumbo na viongozi wa BAVICHA Mkoa na wa wilaya ya Singida mjini na kuwavujishia mpango huu huku wakiwa hawana kithibitisho chochote. Cha ajabu zaidi, tumepewa muda hadi kesho turudishe fedha zote kwao la sivyo tutavuliwa uanachama. Yule dada aliekuwa anatusimamia (Skola) ameshaondoka tangu sa'9 alasiri kuelekea Arusha. Huku ni kuoneana, kosa letu ni Lipi"? Anamaliza Laurent ambae anasema alipewa jukumu la kuhamasisha watu wa kata yake ya Bomani.

Source: Laurent Kiula
Katibu-UVCCM
BOMANI-KIOMBOI
 
He! Kwa haya Mwigulu anahitaji wokovu! Ana njama nyingi sana na amekuwa mshabiki mkubwa wa mambo ya giza kuliko nuru, na kwa mambo yanavyomwendea vibaya utadhani muda wa revenge umefika kwenye zile muvi za kihindi au za kichawi za nigeria
 
Kwa akili zenu za kibavicha mnataka shughuri zote za kiuchumi zisimame kwa sababu kiongozi wetu wa chama anahutubia watu wa eneo fulani nchini.

By the way, who is slaa katika nchi hii mpaka shughuri za kiuchumi zisimame.

Mnafahamu ni lini mipango ya timu ya simba kucheza ilifanyika na makubaliano yakawepo na pia ni lini mipango ya kiongozi wa CHADEMA ilifanyika ili kuhutubia eneo hilo.

Halafu ni kuwadharau wananchi kama vile hawafahamu priority zao kimaisha mnapotaka waende kwenye outdated CHADEMA public rally.

Siasa za kilaghai hazina nafasi katika ukweli.

Keep on crying baby

Devil's message!
 
Nao simba nawalaumu kwa kukubali mwaliko wa kijinga kama huo.

Wako kimaslahi mkuu. Wanalipwa kwa hiyo ni kama wafanyabiashara tu. Au ulidhani wangeenda Singida kucheza bure bila posho? Mwigulu lazima kaomba fungu toka kwenye kodi za wavuja jasho na kuwalipa Simba.
CCM wana hela gani kama sio kodi za walala hoi?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Wakuu, huyu ndiyo chama cha mapinduzi kinamwamini kwamba anamikakati kamambe ya kukimaliza CHADEMA, ndio kama hizo...
 
This is too cheap,jamaa anafanya siasa za kishamba kweli..simba nao wamechemka vibaya.

Mkuu jamaa ni kama ule usemi "an old dog old tricks" you will never teach old dog new tricks. Haiwezekani

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Wakuu, huyu ndiyo chama cha mapinduzi kinamwamini kwamba anamikakati kamambe ya kukimaliza CHADEMA, ndio kama hizo...

Kwa hiyo Nchemba ndio Strategic Planner wa CCM? Na hiyo nayo tuiite mikakati kamambe?
Kweli?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Nao simba nawalaumu kwa kukubali mwaliko wa kijinga kama huo.
Hawana kosa Simba wao wameenda kibiashara wamelipwa kwa kwenda huko usije ukakosea kuwa walikwenda kiCCM. Aliyepata hasara ni Akili ndogo!
 
Huo mkutano uliojaa kupita kawaida uko wapi,
Achani utani hawa watu ndiyo utasema kujaa kupita kawaida uongo mwingine majanga.
 
Huo mkutano uliojaa kupita kawaida uko wapi,
Achani utani hawa watu ndiyo utasema kujaa kupita kawaida uongo mwingine majanga.


Issue hapa sio kujaza, ila ni kuangalia proportion ya watu kwenye mechi ya Simba na Iramba Combine v/s proportion ya audience ya Mkutano wa CDM with regard na hatred campaigns za Mwigulu Nchemba dhidi ya ujio wa Dr.W.Slaa.
 
Last edited by a moderator:
Mtakodisha sana Simba na itabidi muwalete hata Manchester kwa sababu mikutano itakuwa zaidi ya 170 (angalau 10 kila kata) kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwakani. Itabidi mkubali siasa za kistaraabu na za akili. Siasa za kijinga na fitina hazina nafasi katika karne ya leo. Poleni sana.
 
He, he, heee! hana aibu. Ningekuwa yeye baada ya uwongo katika ule uzi uliofungwa ningeficha uso wangu hapa jamvini angalau kwa mwezi ili watu wasahau. Lakini waongo hawana aibu.
@Jasusi, we kweli jasusi kabisa. Sasa ushauri gani huo tena? Sema ajifiche siku mbili tuu,mwezi mzima atakula nini? Wenzio wako kazini hapo hakuna cha aibu mradi mkono uende kinywani, akijitokeza Kajikausha kama sio yeye vile! Chezea namba ya Ronaldo wewe? (7)
 
Mtakodisha sana Simba na itabidi muwalete hata Manchester kwa sababu mikutano itakuwa zaidi ya 170 (angalau 10 kila kata) kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwakani. Itabidi mkubali siasa za kistaraabu na za akili. Siasa za kijinga na fitina hazina nafasi katika karne ya leo. Poleni sana.

haha..eti nasikia anasema uliwanunu watu aliowanunu ulitoa kitu gani cha ghali ambacho pesa ya CCM imeshindwa....sasa mikutano 170,wakati lumumba hakuna tena mtu mwenye afya wala nguvu si mnataka muua kabisa mwigulu na Nape?


wapo busy wanafikiria hii plan, nadhani thisi time wanajua kiingereza ila kiingereza hakitokuwa issue ila uhalali:

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...siwe-km-walivyoomba-meno-ya-tembo-yauzwe.html
 
Ataumbuka sana hadi kufika 2015 atakuwa amesahaulika kwenye ulingo wa siasa - muflisi kabisa!!!!
 
Ndugu zangu wana JF,
Kama ilivoelekezwa hapo awali, Katibu mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Dr. Wilbroad Slaa anaendelea na ziara yake nchini. Leo hii, Dr. Wilbroad Slaa akiambatana na ujumbe wake wameanza ziara ya kichama Mkoani Singida. Awali, Dr. Slaa alipanga kufanya mkutano Kiomboi leo jioni. Hata hivyo, katika hali isiyo ya kawaida, Mbunge wa Iramba magharibi, Mwigulu Nchema aliialika timu ya Simba kucheza na timu ya Kiomboi bila kiingilio. Hii ilikuwa ni strategy ya makusudi ya kupunguza mahudhurio katika mkutano wa CHADEMA. Lakini pamoja na mbinu hiyo mufilisi, mkutano wa CHADEMA ulioanza majira ya saa nane Mchana ulifurika kupita kawaida, na wananchi walibaki katika hali ya utulivu mpaka pale Dr. Slaa alipomaliza kuhutubia na kupanda Helikopta kuelekea Singida Mjini kwenye mkutano mwingine. Katika mechi hiyo ambayo ilichelewa sana kuanza kutokana na gari waliyokuwa wamepanda timu ya Simba kupata matatizo ya kiufundi njiani ambayo imemalizika hivi punde, Simba S.C ilifanikiwa kuwakung'uta mahasimu wao kwa mabao matatu pasipo majibu.

Ndugu yangu Mwigulu, siku baada ya siku mambo yanazidi kukuendea vibaya. Huoni umuhimu wa kujirekebisha na kutimiza majukumu yako ya kibunge? Hizi gharama za kuwaleta Simba S.C hapa Kiomboi zingeweza kuwaleta Kindai Shooters au Magic F.C kutoka pale Singida Mjini na bado zikatosha kuwasaidia wananchi wa Urughu pale wanaojifungulia majumbani mpaka leo kwa kukosa kituo cha afya.. Badala yake, ulijitafutia utukufu kwa kuileta Simba yenye jina na uwezo mkubwa, sio ili kuwaburudisha wananchi au ili kujipima kimchezo, bali ili uizuie CHADEMA.
Sina shaka mfululizo wa kushindwa kwako kutakufundisha jambo.
"Akili ndogo vs. Akili kubwa"..
Naomba kuwasilisha.

Kurunzi Huru, tunakushukuru sana,sana kwa taarifa hii; naamini HAMY-D, RITZ na Ant-Dr Slaa na Mbowe wengine wamekusoma na kujionea wenyewe thru Pictures nini kilichotokea katika Mkutano huo. Nina ushauri ufuatao wa wana Singida na Watanzania ha hapa JF kwa ujumla. CCM inataka na hakika kwa namna yoyote and I mean kwa vyovyote kubaki madarakani milele na milele. Ili kufanikisha Agenda hii ya kubaki madarakani ni kuhakikisha kuwa wananchi wanaendelea kuwa masikini na kukosa Elimu ya kujitambua.

Kitendo cha kuwapa wale vijana ile TZS 300,000.00 ili kufanikisha mkakati ovu wa kuhamasisha watu wasihudhurie Mkutano wa Dr Slaa ni moja tu lakini pia hao vijana wanaonekana wana njaa haswaa; sasa wanatakiwa wajiulize ok wao wangepata hata kama ni TZS 50,000 kwa kila kichwa, je hiyo itawasaidia kulipa kodi ya biashara katika vibanda vyao?, kulipia kodi ya mifugo yao?, kulipia huduma za hospitali?, kuwa support wazee wao? kulipia michango mbalimbali ya shuleni ?n.k. Kwa hakika jibu ni hapana. Kunahitajika fursa za muda mrefu ni si ZIMAMOTO ambayo Ndg Mwigulu anajaribu kuijenga miongoni mwa wana Singida. Fedha hizo angeweza kuzitumia kuchimba hata kisima ili wananchi wapate angalau maji ya kufulia, wote tunaijua Singida jamani.

Pili, Ndg Mwigulu inasemwa kuwa wewe ndio uliyeialika Timu ya Simba kuja Iramba na lengo likiwa ni kutaka kudhoofisha Mkutano wa Katiba wa Dr Slaa, hivi kweli Ndg Mwigulu, kwa sasa kipaumbele cha Wana - Iramba ni kukuza Soka?hapana you mighty be joking,.Kualika timu kubwa kama Simba ni gharama kubwa sana tena kama haikuwa katika Ratiba yao, You have to pay for Transport, pay for Foods, Snacks and Drinks, pay for Players and Leaders Allowances, pengine hata kuwahonga hao viongozi ili wakubali kuilete timu. Generally ni pesa nyingi, wewe unazo hatukatai lakini naamini zingeweza kutumika ku support shule zisizokuwa na vifaa vya kufundishia, kukarabati baadhi ya barabara za mitaa katika Jimbo lako,kusiadia familia masikini hapo Singida n.k, n.k; wewe umezipotezea kwa Simba Sports Club. Akili gani hiyo?

Polisi, Nimeshangazwa sana mmekaa kwenye Mkutano na kila aina ya Silaha as if mnaenda Vitani na hii bila shaka itakuwa ni maombi na maelekezo ya huyo Ndg Mwigulu ili kuwatisha Wananchi, jamani hivi hata nyie hamjui haki zenu. Hvi hamjisiii vibaya mnapowararua watu risasi then kesho mnakutana mtaani watu wankunyooshe vidole utadhani Mchawi au mtu aliyejinyea?Hivi nyie mlipata fursa ya kutoa maoni yenu au ndo ileile akisema IGP ndo mawazo yenu nyie, kwa taarifa yenu IGP hana shida yoyote wala hajui taabu mzipatazo hasa katika masilahi na mazingira ya kazi yenu. Zingatieni na mzinduke. Kama nyie mmeshindwa kuchangia, acha wazazi, ndugu na jamaa zenu wawasemee, sio mmejikusanya, mmejifunika nyuso, jua linawachoma hata posho hakuna, anakula Kamanda wenu. Za kuambiwa ongezeni naza kwenu.

Enyi wananchi, amka amka amka kumekucha, Saa ya ukombozi wa Pili wa Nchi yetu ni sasa, mimi, wewe, yule, sisi,,tuwakatae hawa Wakoloni weusi CCM, wanyonyaji na makupe weusi CCM. Kamwe tusikubali watutumie kwa sababu ya umasikini wetu, tujiandae kuwaondoa katika Sanduku la kura 2015. Taabu, hofu na machungu yote yatakwisha

CHADEMA Mpango wa Mungu, hii inathibitishwa na kuharibika kwa gari la Simba wakati wakienda Iramba na hivyo kuchelewa kufika uwanjani; hii kwa sisi tunaoamini katika Roho ilikuwa ni kuhakikisha wananchi walio wengi zaidi wanashiriki katika Mkutano wa Katiba chini ua Uongozi wa Dr Slaa.Hiyo ndio INVISIBLE ENERGY. Kwa mliosoma Physics ni LATENT HEAT.Hata hao wachezaji wanahitaji Katiba Mpya, si tunaishi nao jamani mitaani huku.

Ahsante sana CHADEMA; Ahsante sana Mwigulu, Mungu anakutumia kuing'arisha CHADEMA; Mungu Ibariki Tanzania
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom