Ndugu zangu wana JF,
Kama ilivoelekezwa hapo awali, Katibu mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Dr. Wilbroad Slaa anaendelea na ziara yake nchini. Leo hii, Dr. Wilbroad Slaa akiambatana na ujumbe wake wameanza ziara ya kichama Mkoani Singida. Awali, Dr. Slaa alipanga kufanya mkutano Kiomboi leo jioni. Hata hivyo, katika hali isiyo ya kawaida, Mbunge wa Iramba magharibi, Mwigulu Nchema aliialika timu ya Simba kucheza na timu ya Kiomboi bila kiingilio. Hii ilikuwa ni strategy ya makusudi ya kupunguza mahudhurio katika mkutano wa CHADEMA. Lakini pamoja na mbinu hiyo mufilisi, mkutano wa CHADEMA ulioanza majira ya saa nane Mchana ulifurika kupita kawaida, na wananchi walibaki katika hali ya utulivu mpaka pale Dr. Slaa alipomaliza kuhutubia na kupanda Helikopta kuelekea Singida Mjini kwenye mkutano mwingine. Katika mechi hiyo ambayo ilichelewa sana kuanza kutokana na gari waliyokuwa wamepanda timu ya Simba kupata matatizo ya kiufundi njiani ambayo imemalizika hivi punde, Simba S.C ilifanikiwa kuwakung'uta mahasimu wao kwa mabao matatu pasipo majibu.
Ndugu yangu Mwigulu, siku baada ya siku mambo yanazidi kukuendea vibaya. Huoni umuhimu wa kujirekebisha na kutimiza majukumu yako ya kibunge? Hizi gharama za kuwaleta Simba S.C hapa Kiomboi zingeweza kuwaleta Kindai Shooters au Magic F.C kutoka pale Singida Mjini na bado zikatosha kuwasaidia wananchi wa Urughu pale wanaojifungulia majumbani mpaka leo kwa kukosa kituo cha afya.. Badala yake, ulijitafutia utukufu kwa kuileta Simba yenye jina na uwezo mkubwa, sio ili kuwaburudisha wananchi au ili kujipima kimchezo, bali ili uizuie CHADEMA.
Sina shaka mfululizo wa kushindwa kwako kutakufundisha jambo.
"Akili ndogo vs. Akili kubwa"..
Naomba kuwasilisha.