Hamy-D= mwigulu nchemba.
Last edited by a moderator:
Nao simba nawalaumu kwa kukubali mwaliko wa kijinga kama huo.
Nao simba nawalaumu kwa kukubali mwaliko wa kijinga kama huo.
Tunasubiri CCM wamakonde huku watuletee Real Madrid na Wacheze na kariakoo ya lindi iliyoshuka daraja ligi kuu,
Kweli mfa maji haachi kutapa tapa,
Na haya madawa wanayojishughulisha nayo KWELI YANAWALEVY SANA,2015 HII HAPA KWENYE KONA,VIJANA WA MJINI WANASEMA ''MWACHE MWACHE''
Wangekataa hela kamanda; wapo kikazi zaidi. Siasa za kishamba kabisa. Ni vigumu kuwaghilibi wananchi wa leo ambao njia za kupata taarifa zipo kibao.
Haya mawazo ni yale ya kwako au mengine umechukua ya watu ambao wanamatatizo sijaona unachoongea zaidi ya kujikanyaga na kujipinga mwenywe kweli bavicha kuna manyago ndiyo maana kila bavicha yeye ni matusi tu kumbe vichwa havina kitu.haha..eti nasikia anasema uliwanunu watu aliowanunu ulitoa kitu gani cha ghali ambacho pesa ya CCM imeshindwa....sasa mikutano 170,wakati lumumba hakuna tena mtu mwenye afya wala nguvu si mnataka muua kabisa mwigulu na Nape?
wapo busy wanafikiria hii plan, nadhani thisi time wanajua kiingereza ila kiingereza hakitokuwa issue ila uhalali:
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...siwe-km-walivyoomba-meno-ya-tembo-yauzwe.html
Tangu jana nilipopata taarifa hii nilijivua rasmi uanachama wa simba, na pia nimejivua rasmi ujumbe wa kamati ya ufundi , huyu Rage asidhani simba anaweza kuitumia kisiasa . SHAME ON HIM !
Mkuu jitahidi uanze kushabikia bavicha club ndiyo inakufaa,Kiukweli na naomba niliseme hili Wanairamba walielewe Mwigulu hafai hata kuachwa aiongoze familia yake! ni mtu wa ajabu sana! anafanya mambo ya kishenzi na ya aibu! mbona hajifunzi? Nimeichukia club ya simba kwa kutumika kijinga namna hiyo na "Natangaza rasmi kujivua ushabiki wa simba" Kama timu inaweza kutumiwa kipuuzi namna hiyo siwezi kuendelea nayo! Wanairamba ni lazima wachoshwe na mwenendo wa mbunge wao na wamuwajibishe kwa vitendo na ghadhabu kuu!
Sasa mtu mmoja atajigawa vipi mara mbili?? Yaani huyo huyo awepo kwenye mkutano halafu wakati huo huo awepo kwenye kazi zake nyingine...???? Hebu jitahidini kufikiri kwa kutumia kichwa bana, hayo ma------ shughuri yake ni nyingineMkuu jitahidi uanze kushabikia bavicha club ndiyo inakufaa,
kwani slaa akienda sehemu kazi zingine za pale hazifanyiki basi mwambieni aanzishe bendi ili aanze kufanya makongamano kama anataka kuangaliwa.
Ndugu zangu wana JF,
Kama ilivoelekezwa hapo awali, Katibu mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Dr. Wilbroad Slaa anaendelea na ziara yake nchini. Leo hii, Dr. Wilbroad Slaa akiambatana na ujumbe wake wameanza ziara ya kichama Mkoani Singida. Awali, Dr. Slaa alipanga kufanya mkutano Kiomboi leo jioni. Hata hivyo, katika hali isiyo ya kawaida, Mbunge wa Iramba magharibi, Mwigulu Nchema aliialika timu ya Simba kucheza na timu ya Kiomboi bila kiingilio. Hii ilikuwa ni strategy ya makusudi ya kupunguza mahudhurio katika mkutano wa CHADEMA. Lakini pamoja na mbinu hiyo mufilisi, mkutano wa CHADEMA ulioanza majira ya saa nane Mchana ulifurika kupita kawaida, na wananchi walibaki katika hali ya utulivu mpaka pale Dr. Slaa alipomaliza kuhutubia na kupanda Helikopta kuelekea Singida Mjini kwenye mkutano mwingine. Katika mechi hiyo ambayo ilichelewa sana kuanza kutokana na gari waliyokuwa wamepanda timu ya Simba kupata matatizo ya kiufundi njiani ambayo imemalizika hivi punde, Simba S.C ilifanikiwa kuwakung'uta mahasimu wao kwa mabao matatu pasipo majibu.
Ndugu yangu Mwigulu, siku baada ya siku mambo yanazidi kukuendea vibaya. Huoni umuhimu wa kujirekebisha na kutimiza majukumu yako ya kibunge? Hizi gharama za kuwaleta Simba S.C hapa Kiomboi zingeweza kuwaleta Kindai Shooters au Magic F.C kutoka pale Singida Mjini na bado zikatosha kuwasaidia wananchi wa Urughu pale wanaojifungulia majumbani mpaka leo kwa kukosa kituo cha afya.. Badala yake, ulijitafutia utukufu kwa kuileta Simba yenye jina na uwezo mkubwa, sio ili kuwaburudisha wananchi au ili kujipima kimchezo, bali ili uizuie CHADEMA.
Sina shaka mfululizo wa kushindwa kwako kutakufundisha jambo.
"Akili ndogo vs. Akili kubwa"..
Naomba kuwasilisha.
Mtakodisha sana Simba na itabidi muwalete hata Manchester kwa sababu mikutano itakuwa zaidi ya 170 (angalau 10 kila kata) kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwakani. Itabidi mkubali siasa za kistaraabu na za akili. Siasa za kijinga na fitina hazina nafasi katika karne ya leo. Poleni sana.