Ndugu zangu
wana JF,
Kama ilivoelekezwa hapo awali, Katibu mkuu wa Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo Dr. Wilbroad Slaa anaendelea na ziara yake nchini. Leo hii,
Dr. Wilbroad Slaa akiambatana na ujumbe wake wameanza ziara ya kichama
Mkoani Singida. Awali, Dr. Slaa alipanga kufanya mkutano Kiomboi leo
jioni. Hata hivyo, katika hali isiyo ya kawaida, Mbunge wa Iramba
magharibi, Mwigulu Nchema aliialika timu ya Simba kucheza na timu ya
Kiomboi bila kiingilio. Hii ilikuwa ni strategy ya makusudi ya kupunguza
mahudhurio katika mkutano wa CHADEMA. Lakini pamoja na mbinu hiyo
mufilisi, mkutano wa CHADEMA ulioanza majira ya saa nane Mchana
ulifurika kupita kawaida, na wananchi walibaki katika hali ya utulivu
mpaka pale Dr. Slaa alipomaliza kuhutubia na kupanda Helikopta kuelekea
Singida Mjini kwenye mkutano mwingine. Katika mechi hiyo ambayo
ilichelewa sana kuanza kutokana na gari waliyokuwa wamepanda timu ya
Simba kupata matatizo ya kiufundi njiani ambayo imemalizika hivi punde,
Simba S.C ilifanikiwa kuwakung'uta mahasimu wao kwa mabao matatu pasipo
majibu.
Ndugu yangu Mwigulu, siku baada ya siku mambo yanazidi kukuendea vibaya.
Huoni umuhimu wa kujirekebisha na kutimiza majukumu yako ya kibunge?
Hizi gharama za kuwaleta Simba S.C hapa Kiomboi zingeweza kuwaleta
Kindai Shooters au Magic F.C kutoka pale Singida Mjini na bado zikatosha
kuwasaidia wananchi wa Urughu pale wanaojifungulia majumbani mpaka leo
kwa kukosa kituo cha afya.. Badala yake, ulijitafutia utukufu kwa
kuileta Simba yenye jina na uwezo mkubwa, sio ili kuwaburudisha wananchi
au ili kujipima kimchezo, bali ili uizuie CHADEMA.
Sina shaka mfululizo wa kushindwa kwako kutakufundisha jambo.
"Akili ndogo vs. Akili kubwa"..
Naomba kuwasilisha.
Binafsi mkuu nilikuwepo pia huyu mwigulu ni mtu wa ajabu sana, Pamoja na kusomba watu na malori Ndago, Kiteka na Shilui haikumsadia sana katika hilo.