Aibu kubwa! Msomi unakosaje kazi ya kufanya nchi hii yenye kila aina ya rasilimali?

Shida siyo kwa wasomi bali elimu wanayofundishwa......."collar job based"
yani na elimu yetu tulime, umuhimu wa kusoma upo wapi

Hii ndio shida, mfumo wa elimu na mfumo wa ajira havina mawasliano

Unampeleka mtoto kukaa darasani miaka 17 halafu akitoka huko hamna kazi.... anaishia kuja kumwomba msaada yule ambae hakukaa darasani kabisaaa na kuanza kujifunza kwake kulima na kufuga🙄🙄
 
Hivi wewe ambaye unajiita umesoma halafu inalalamika kuwa huna kazi, unafahamu kwamba unajidhalilisha?

Acha wakose kazi vijana wa Ulaya na Marekani huko lkn siyo hapa Tanzania. Ardhi yenye rutuba isiyohitaji mbolea imejaa tele kwann usijiajiri kwenye kilimo?

Ardhi ya bure ipo tele katika mikoa ya Tabora, Katavi, Tanga, Ruvuma, n.k.

Kwani lazima ukae mjini? Mbona watanzania zaidi ya 80% wamejiajiri ktk kilimo tena wengi wao hawana madigrii kama ninyi lkn maisha yanasonga na ni watulivu wala hawapigi kelel za kukosa ajira.

Wengi wenu mmesomeshwa na wazazi wenu ambao ni wakulima wasiokuwa na elimu. Hawajawahi kuajiriwa na yeyote maisha yao yote.

Mmerogwa na nani ninyi mnaoenda shule? Kama hizi shule na vyuo mnavyoenda ndiyo vinawapeni huu ujinga mm nashauri zifutwe.

Kuna vijana chungu nzima walioishia darasa la saba wanaendeleza maisha kwa kilimo na shughuli nyingine hatusikii wakililia ajira. Wewe msomi umesoma halafu unalia. Usingesoma je? Jinga kabisa!

View attachment 1974112
NATANGAZA! KWA YEYOTE ANAYEHITAJI MAONO AU USHAURI AFANYE NINI ILI AJIKWAMUE NA UMASIKINI AJE DM! Note this, hapa hakuna uganga uganga uje DM ukiwa na akili timamu na mwenye hofu ya MUNGU!
 
Hii ndio shida, mfumo wa elimu na mfumo wa ajira havina mawasliano

Unampeleka mtoto kukaa darasani miaka 17 halafu akitoka huko hamna kazi.... anaishia kuja kumwomba msaada yule ambae hakukaa darasani kabisaaa na kuanza kujifunza kwake kulima na kufuga🙄🙄
watu wanadhani kulima ni kazi rahisi 😂
 
Hela iliyotupwa kwenye ndege ingewekezwa kwenye miundombinu ya umwagaliaji na chain nzima ya kilimo ingemaliza tatizo la ajira na la machinga na bodaboda kupoteza mda mijini.
Na wala tusingetegemea kukopa Ili kuendesha nchi.
Wakoloni waliendesha nchi kwa kilimo na wakafanya makubwa Sana.Soko la mazao huko duniani hatuwezi lijaza hata KILA mtza akilima mazao.
Tatizo sera mbovu.
Ni aibu sana kwa mito kwa mito kumwaga maji bahari yapotee bure inatakiwa maji ya mito yaishie mashambani.
Tatizo la kilimo cha Tanzania liko kwenye soko siyo uzalishaji. Kwasasa hatuhitaji miundombinu ya umwagiliaji tunahitaji masoko. Kwasabb huko Mbeya Katavi na Ruvuma mahindi yanaoza kwa kukosa wanunuzi.
 
Hii ndio shida, mfumo wa elimu na mfumo wa ajira havina mawasliano

Unampeleka mtoto kukaa darasani miaka 17 halafu akitoka huko hamna kazi.... anaishia kuja kumwomba msaada yule ambae hakukaa darasani kabisaaa na kuanza kujifunza kwake kulima na kufuga🙄🙄
Njia ya sasa,baada ya form 4 ni bora kwenda veta kuliko form6
 
Tatizo la kilimo cha Tanzania liko kwenye soko siyo uzalishaji. Kwasasa hatuhitaji miundombinu ya umwagiliaji tunahitaji masoko. Kwasabb huko Mbeya Katavi na Ruvuma mahindi yanaoza kwa kukosa wanunuzi.
Badili mazao sio wote lazima mlime mahindi,sageni unga unga haukosi soko.
Masoko tele nje ya nchi sio lzm uuzie nchini tu.
 
huyo RC ashawahi kulima hata bustani? kilimo kinahitaji mtaji na masoko ya mazao, una lima mahindi sumbawanga halafu serikali inakukataza usiyapeleke zambia ni akili hiyo?
 
Badili mazao sio wote lazima mlime mahindi,sageni unga unga haukosi soko.
Masoko tele nje ya nchi sio lzm uuzie nchini tu.
Hapa unamuangalia mkulima mkubwa tu. Lkn huyu maskini hawezi kufanya hii michakato ya kusaga na kuuza nchi za nje.
 
yani na elimu yetu tulime, umuhimu wa kusoma upo wapi
Umuhimu wa kusoma ni kuongeza maarifa ili utatue changamoto za maisha.
kama umesoma ili upate kazi na bado una changamoto ya uchumi basi jua hauna akili na kweli hakuna umuhimu wa kusoma.
 
Kama kilimo kingekuwa kinalipa,basi mikoa ya Kanda ya ziwa,nyanda za juu kusini ingeongoza kwa kipato kimkoa na mchango kwenye pato la Taifa,lakini unajua mkoa unaoongoza?ni Dar es salaam,mkoa ambao hauna shughuri kubwa za kilimo lakini unachangia asilimia 80 ya pato la Taifa!!
Kwa kila shilingi 100 inayoingizwa kwenye mfuko wa Taifa,asilimia 80 inatoka Dar!!hiyo mikoa inayolima ipo wapi??
Hoja zako kwamba vijana wakiomaliza vyuo waende mikoani,wakamate ardhi(ambayo ipo bwelele)walime,zimekaa kinadhalia tu na ni story za kwenye makaratasi hazina uhusiano na Hari halisi iliyopo kwenye mazingira yao.
Huwezi kutoka hapa ukaenda Katavi,ukachukua ardhi,ukaanza kulima mahindi,ukavuna!na ukapiga pesa ndeefu!?
Mfuko wa mbolea unauzwa 100000Tsh,gunia la mahindi linauzwa 20000Tsh!
Hapo ndipo umuhimu wa elimu unahitajika kusolve hizo changamoto, na sio utegemee ukae ofisini.

Vijana waliosoma Tanzania ni mzigo kwa taifa sababu hawajui jinsi ya kutumia elimu wala umuhimu wake zaidi ya ajira.
Wakati marekani wanatengeneza rockets na space stations pia kugundua vitu vipya kusolve humanity's great problems kama climate changes kwa elimu hiyo'hiyo.

Acha waendelee kuzeeka masikini wakitumia instagram na ujinga mwengine.
 
Kilimo cha mdomo rahis kweli sio cha shambani. Ukodishe shamba kama huna, utafute vibarua, ununue mbegu, mbolea hii inayopanda kila siku, madawa, sumu za wadudu, booster. Hapo bado hujaibiwa
Hapo ndipo umuhimu wa elimu unapohitajika kusolve hizo problems.
Hakuna kitu rahisi duniani, na vitu ambavyo unaona rahisi vimehangaikiwa vilevile hivyo ukitaka rahisi basi jua vina gharama kubwa.
 
sasa maana ya wao kusoma mpaka vyuo vikuu iko wapi?.... huko huko shule ya msingi si tungewafundisha tu skills za maisha + hicho kilimo then tuwaache waje mtaani...
Mkuu unasoma ili unongeze maarifa, upanue uwezo wako wa kufikiri ili uweze kutafuta solutions kwenye maisha na sio kupata ajira.

Hii inaonesha jinsi gani mfumo wa elimu ulivyo mbovu Tanzania, no wonder why graduates wengi akili zao wanazijua wenyewe wachache ndio wanajua wanachokitafuta.
 
usilolijua ni usiku wa giza kama umefanikiwa kwenye chochote kila shukuru sana mungu alafu mwambie muumba tafadhali usije nipitisha kwenye kikombe cha mateso..
Mateso kama yapi mkuu kula ugali na dagaa au kukaa kwa wazazi na shemeji.
You see hayo unayoita mateso kuna uwezekano mkubwa ni maisha ya watu kila siku na hawalalamiki sababu technically hayaakisi maana ya neno mateso.
 
Hela iliyotupwa kwenye ndege ingewekezwa kwenye miundombinu ya umwagaliaji na chain nzima ya kilimo ingemaliza tatizo la ajira na la machinga na bodaboda kupoteza mda mijini.
Na wala tusingetegemea kukopa Ili kuendesha nchi.
Wakoloni waliendesha nchi kwa kilimo na wakafanya makubwa Sana.Soko la mazao huko duniani hatuwezi lijaza hata KILA mtza akilima mazao.
Tatizo sera mbovu.
Ni aibu sana kwa mito kwa mito kumwaga maji bahari yapotee bure inatakiwa maji ya mito yaishie mashambani.
Wanasubiri mvua

Hakuna watu wavivu kama Watanzania
 
Nimesoma comments nimeona tatizo ni mfumo wa elimu
kwamba hawa graduates waliaminishwa ukisoma na ukamaliza basi utapata ajira na utakuwa na maisha mazuri kununua gari na blah blah fairy tales nyingine.
lakini baada ya kukutana na uhalisia wa maisha kila kitu wanakiona kigumu.

Kingine ni Uvivu.
zile fake fairy tales zimewabrain wash na kuwafanya wahisi kila kitu ni rahisi hivyo baaada ya kukutana na uhalisia wa maisha ambapo kila kitu ni kigumu then wakashindwa kupambana na maisha kitu ambacho kinawafanya wawe masikini na kuendelea kuhudumiwa.

Mwanaume kuwa na mindset hii ni kitu kibaya it's illegal, Mwanaume mtu mzima kuhudumiwa ni kitu ambacho siwezi kuimagine na kwa wanawake wanaishia you know!...mitandaoni.

I gotta life tip and Here is the life tip: maishani hakuna kitu rahisi, na kila ambacho unakiona ni rahisi kilipiganiwa na kuhangaikiwa vilevile hivyo tambua ukitaka rahisi basi jua kina gharama kubwa zaidi, everything has a price. and as always it ends up in tragedy..

Nawatakiwa kuhudumiwa kwema.
 
Mwaka 2007 kuna kitabu nilisoma na nikaambiwa ili ufanikiwe unahitaji MTAJI, kitabu kikasema tena namna RAHISI KABISA ya kupata mtaji ni kwa kutumia ARDHI

Na nikaambiwa utajiri (maana ndiyo mnapenda kuita ndiyo mafanikio) unapatikana popote iwe ni mjini au kijijini

Mpaka leo bado nakubaliana na kitabu hiki na ni kweli kwa asilimia 100.
 
Back
Top Bottom