Aibu kubwa! Msomi unakosaje kazi ya kufanya nchi hii yenye kila aina ya rasilimali?

Kama kilimo kingekuwa kinalipa,basi mikoa ya Kanda ya ziwa,nyanda za juu kusini ingeongoza kwa kipato kimkoa na mchango kwenye pato la Taifa,lakini unajua mkoa unaoongoza?ni Dar es salaam,mkoa ambao hauna shughuri kubwa za kilimo lakini unachangia asilimia 80 ya pato la Taifa!!
Kwa kila shilingi 100 inayoingizwa kwenye mfuko wa Taifa,asilimia 80 inatoka Dar!!hiyo mikoa inayolima ipo wapi??
Hoja zako kwamba vijana wakiomaliza vyuo waende mikoani,wakamate ardhi(ambayo ipo bwelele)walime,zimekaa kinadhalia tu na ni story za kwenye makaratasi hazina uhusiano na Hari halisi iliyopo kwenye mazingira yao.
Huwezi kutoka hapa ukaenda Katavi,ukachukua ardhi,ukaanza kulima mahindi,ukavuna!na uka piga pesa ndeefu!?
Mfuko wa mbolea unauzwa 100000Tsh,gunia la mahindi linauzwa 20000Tsh!
gunia la bangi ni 1.2m(unnecessary needs), gunia ya mahindi elfu 20000, nchi ina vituko hii...nlilima mahindi nimeyaweka ndani bei mbovu ukiuza hasara..na nna fanya kazi sa hali ipoje kwa wanaotegemea kilimo cha mahind ?.. mleta post hajui game lipoje kaweka na post inayohusu RC wa mwanza ambaye ye mwenewe mfanyakazi wa kaz ya kupewa..kmmmk....ccm mbwa sanaa
 
Shukran sana mkuu Sexless , Gairo napaelewa. Chakwale na Iyogwe nadhani ndio zipo ukanda mmoja.

Ngoja tukalime viazi vitamu, huwa vinakubali sana maeneo hayo na wala huwa hawatumii mbolea, ni kulima matuta, kupanda mbegu, kupalilia na kusubiri mavuno tu.
Acha watu waendelee kupaka piko na kujichubua nyuso hapa mjini. Tutakutana uzeeni
 
Umesema vema sana, yaani ukiangalia comments za watu unagundua kwamba huyu anaelewa anachokisema, lakini mwingine labda kwa sababu ya hali nzuri aliyonayo kiuchumi( kwa kubebwa ) anaona ni rahisi sana hiyo shughuli.

Nawambieni vijana wengi ideas zipo, lakini unaanzaje ndiyo kasheshe hususani financial means
Unatafuta uchochoro tu wa kujifichia. Hicho kifaa unachotumia kuingia humu jf ni mtaji tosha kabisa. Muda unaotumia kujaribu na kushindwa utalishwa na wanaokulisha hivi Sasa ambapo umekaa kwao ukisubiri ajira ambazo hazipo
 
Mim kama msomi nisiye na ajira ,uzi huu umeniuma..ila najifunza.
Ndugu yangu hapa pa kukusanya mbolea ya kuenea heka tano utatumia kichwa,au nguvu kazi watu au chombo cha moto cha kukodi.
Kutumia kichwa hutamaliza kwa haraka peke yako,kama utahitaj kukod nguvu kaz ,ni bora kununua ya viwabdan mana gharama hazikwepeki.

Hii comment imekaa kinadharia,
Ndugu yangu kilimo siyo sawa na betting inayoanza siku ama muda mchache kabla ya mchezo.

Kuna muda wa miezi 3 mpaka 5 ya kuandaa mashamba. Vijijini tunaishi kijamaa, hivyo baiskeli tunaazimana tu wala hazikodishwi. Au waweza kuinunu (sh elfu 70) ukaitumia kusombea samadi miezi mitano. Acheni kukaa mjinini mnaishia kujichubua usoni na kupaka piko tu
 
jamaa yangu mbona sasa unazungumzia hela hela mara hela kidogo....hakuna kilimo rahisi duniani cha kutumia nguvu zako tu bila hela karne hii... jaribu kutoa mbinu nyingine....Dunia ya sasa inahitaji kianzio kwa maana ya hela uweze kutafuta uelekeo....hata udalali tu wa vyumba nao unahitaji mtaji....
Ukiwa na nia inawezekana kabisa. Omba fedha toka kwa hao wanaokulisha na kukuvisha miaka yote hii ambayo unasubiria qjira.

Ama uza hicho kifaa kinachokuwezesha kuingia humu jf. Pia save hiyo hela ya bando utapata mtaji wa kilimo. Kilimo hwkihitaji mtaji mkubwa ndiyo maana hata bibi ywngu ni mkulima
 
Siyo kweli, hiki ni kinatumika Kama kichaka tu Cha kufichia udhaifu wa wasomi.

Wale wanaomaliza SUA wamesoma miaka 4 Mambo ya kilimo mbona hawajiajiri kwenye kilimo?

Kuna graduates kibao wamejiajiri kwenye bodaboda na machinga. Kwenye syllabises zao kuna umachinga na bodaboda?

Graduates wengi wana mentality kwamba kilimo ni kazi ya wasiosoma. Ndiyo maana mnatoa visingizio kibao
Hakuna mtu ambaye ni mjinga wa kuacha biashara inayolipa.
Boda boda inalipa na iko wazi pesa ya fasta fasta mkononi tu! Hukosi elf 10 p

1634247222227.png
 
Kilimo kingelipa kusingekuwepo na machinga mijini.
Machinga wapo kwasabb ya fikra potofu kwamba kilimo ni cha watu wasiosoma ama wazee tu.

Kumbuka Dangote(tajiri na 1 Afrika) katoboa maisha kupitia kilimo.
 
Ukiwa na nia inawezekana kabisa. Omba fedha toka kwa hao wanaokulisha na kukuvisha miaka yote hii ambayo unasubiria qjira.

Ama uza hicho kifaa kinachokuwezesha kuingia humu jf. Pia save hiyo hela ya bando utapata mtaji wa kilimo. Kilimo hwkihitaji mtaji mkubwa ndiyo maana hata bibi ywngu ni mkulima
Unafurahisha genge ....!
 
Kilimo cha biashara siyo aina ya mazao yanayolimwa bali ni malengo uliyojiwekea. Unaweza kulima maharagwe, mahindi, mpunga ama viazi kwa lengo la kuuza ili kupata pesa. Tayari hicho kinakuwa kilimo cha biashara.

njoo basi huku kanda ya ziwa upime kama utapata hayo malengo ya kibiashara
 
Unajua uwekezaji wa maua wewe, biashara hiyo mfano halisi TANZANIA/Mount Meru FLOWERS Arusha anashare Mzee Sarakikya mkuu wa jeshi mstaafu na mzungu na Mama mmoja anaitwa mama Uriyo, ni uwekezaji wa billions bro
uwekezaji kwenye maua ndio nimesema ni mfano wa kilimo biashara...nisome tena!
 
Unatafuta uchochoro tu wa kujifichia. Hicho kifaa unachotumia kuingia humu jf ni mtaji tosha kabisa. Muda unaotumia kujaribu na kushindwa utalishwa na wanaokulisha hivi Sasa ambapo umekaa kwao ukisubiri ajira ambazo hazipo
Sa
Unatafuta uchochoro tu wa kujifichia. Hicho kifaa unachotumia kuingia humu jf ni mtaji tosha kabisa. Muda unaotumia kujaribu na kushindwa utalishwa na wanaokulisha hivi Sasa ambapo umekaa kwao ukisubiri ajira ambazo hazipo
Sasa nikiuza kifaa hiki madini ya JF nitakuwa nayapata wapi?
Sema nitafute namna nyigine ya kupata mtaji na sio kuuza kifaa cha ujuzi aaaah!!!
 
Issue sio kazi..., issue ni kama kazi zilizopo / zinazofanyika zinampatia mtu kipato.....

Huwezi kutegemea mtu mmoja awe producer, marketing, human resource na market researcher, hilo halipo..., wakulima wamelima zao mahindi kule alafu utegemee wao wao ndio waingie kitaa kufatufa masoko (wakati kuna walanguzi wanawatazama na serikali inawakataza wasiuze nje mazao yakiwa machache na kuwasahau yakiwa mengi)...

Kujiajiri na kuwa street smart sio elimu ya shule ni they way mtu alivyo (attitude) na inahitahi uvumilivu na discipline, aina ya watu hao ni wachache kama 10% katika population na ni hao ndio wanaweza kufungua fursa za wengi ambao wanaishi pay-check to pay-check so long as wanapata malazi, mavazi na chakula (middle income) hilo sio tatizo...

Ofcourse kuna tatizo na elimu yetu pia its not fit for purpose....

 
Machinga wapo kwasabb ya fikra potofu kwamba kilimo ni cha watu wasiosoma ama wazee tu.

Kumbuka Dangote(tajiri na 1 Afrika) katoboa maisha kupitia kilimo.
Kama kilimo kingelipa kwa kutumia nguvu nani anapenda kukaa barabarani kuganga Ili apate 2000 au 3000 kwa siku.
Kilimo ni pesa,akili,maarifa na ujuzi.
 
Hela iliyotupwa kwenye ndege ingewekezwa kwenye miundombinu ya umwagaliaji na chain nzima ya kilimo ingemaliza tatizo la ajira na la machinga na bodaboda kupoteza mda mijini.
Na wala tusingetegemea kukopa Ili kuendesha nchi.
Wakoloni waliendesha nchi kwa kilimo na wakafanya makubwa Sana.Soko la mazao huko duniani hatuwezi lijaza hata KILA mtza akilima mazao.
Tatizo sera mbovu.
Ni aibu sana kwa mito kwa mito kumwaga maji bahari yapotee bure inatakiwa maji ya mito yaishie mashambani.
 
Back
Top Bottom