Ahsanteni Sana Wagosi wa Kaya kwa kusikiliza Kero ya JMushi

Kuna watu wachache sana wameshiikilia hii Game.Na hao watu kwa kuwa wanafikiri kufanya biashara ni lazima uendekeze mapenzi tu ndio waorudisha nyuma watu wazima kama Wagosi wa kaya na wengineo wanaoona upande mwingine wa shilingi.

Watu hawa bila ya kuwaanzishia kampeni ya kuwarekebisha watuharibia muziki wetu vibaya sana.Ile timu ya wale wachambuzi wa nyimbo mpya Clouds ambapo ukitoa single yako unaipeleka pale na wao ndio wanaoamua ipigew redioni ama la nayo ni kimeo vibaya sana..
 
Wasanii wanamchango mkubwa sana katika jamii na wanasikika na kila rika.
Nakumbuka wakati wa kampeni hapo jirani Kenya walitumia sana wasanii kutoka Bongo nakumbuka Odinga aliwatumia wasanii kutoka Bongo siwakumbuki vizuri kuvuta hadhira na kuwaburudisha kisha yeye anamwaga cheche.
Kwa hapa Bongo nahisi wasanii wanaogopa sana kutunga nyimbo zenye ukweli wa ufisadi ili kuelimisha jamii wanawaogopa mafisadi kwani wanaweza kuwaharibia LIFE lao kwani nao wanamkono mlefu kama serikali.
Tunawaomba wasanii wasiogope wamwage tu cheche wakuwatetea tu waimbe nyimbo nyingi sana kuchukia ufisadi ikiwezekana lianzishwe tamasha la kuchukia UFISADI na kuzunguka mikoani kama wanavyo fanya kwenye FIESTA.Tunawaomba hao CLOUDS FM kama kweli na wao wapo kwenye vita hii ya kutokemeza ufisadi basi waandae tamasha hilo na wazunguke mikoani kuhamasisha jamii kupiga vita ufisadi kwa kutumia wasanii.
 
Mzozo your right.. i hope hata fina na kipanya nao watakua waliwekewa mtimanyongo sababu ya tabia yao ya kukemea maovu na uozo wa serikali hii na kwa bahati mbaya au nzuri kipindi chao kilikua kishapata wasikilizaji wengi sana..naona wazee wa kazi wakaona madogo wanataka kuwaharibia..mambo ndio yakawa ivyo mizengwe juu ya mizengwe mara mic haifanyi kazi mara sijui nini alimradi tu mazingira yao ya kazi yawe ya kukatisha tamaa..matokeo yake ndio ivyo kama tulivyoona..hatuwasikii tena.. i doubt hata hawa wasanii nao wanaogopa hivyo ivyo ....but we need to encourage them...... sijui tutafika?????!!!

Well njia inaweza kuwa mbovu yenye madimbwi na makorongo lakini mwisho wa Safari tutafika tu. Naamini katika hilo.
 
hicho kibao nimekiskia leo pia katika power breakfast.jamaa wamesema maneno yaliyo tulia.
na imeonyesha kuwa nao wanamchango mzuri sana kwenye hii vita.
Na wengine nao wajitokeze tupambane mpaka kieleweke.
 
ni kawaida ya hawa vijana kutoa nyimbo za namna hii, wimbo ni mzuri sana na umekuja kwa wakati muafaka.
Jinsi ya kuwaunga mkono ndo tuambiwe
 
ni kawaida ya hawa vijana kutoa nyimbo za namna hii, wimbo ni mzuri sana na umekuja kwa wakati muafaka.
Jinsi ya kuwaunga mkono ndo tuambiwe

Yah... kuwaunga mkono nikuwa support hasa kama uko nyumbani..nikupiga simu sana au ku sms sana iyo nyimbo iwe inapigwa kila saa...kama kuna mtu anaukumbuka mwimbo wa Profesa Jay unaitwa Chemshabongo...huo mwimbo ulikua unapigwa kila baada ya dk 30....na ukawa kama ndio mwimbo wa taifa..kila mtu akawa anaujua na ukauletea muziki wa kizazi kipya Heshima..hiyo yote ilitokana na mwamko walioupata wananchi baada ya kuusikiliza ule mwimbo simu na sms zikaanza kumiminika kuombwa upigwe kila mara.hatimaye wananchi wengi wakaufahamu na bongo flava ikaanza kupendwa....sasa bado naamini kabisa kama kweli tunataka nyimbo kama hizi zisipotee kwa urahisi..basi ni sisi wenyewe ndio tunajukumu ya kuziweka kwenye chati na kufanya zitambulike kwa taifa zima hata na nje ya mipaka..na kufanya iwe ndio aina ya nyimbo ambazo ni gumzo kwa taifa na sio za mapenzi tena .... kwa pamoja tutaweza.
 
AMANIGK... wewe ni yule GK wa East Coast?

MTM ningekua msanii wa Bongo Flava na Umri huu wa uzee ningebaki kuimba
style za Yeke Yeke.......
Hata hivyo nashukuru na kunifananisha na vijana wa sasa japokua huyo GK wa East Coast kwa sasa sipendi mwelekeo wake wa muziki! Niseme tu kapoteza Dira.

Mi naimba mnanda mkubwa
 
hicho kibao nimekiskia leo pia katika power breakfast.jamaa wamesema maneno yaliyo tulia.
na imeonyesha kuwa nao wanamchango mzuri sana kwenye hii vita.
Na wengine nao wajitokeze tupambane mpaka kieleweke.

Tatizo ndio hilo...waoga..mashairi wanayo ila ndio ivyo..wanaogopa wakitoa watapoteza hela nyingi ya maandalizi na mwisho wa siku nyimbo inazimika kama mshumaa...ujue kuna vibaraka waufisadi nao kwenye radio stations....vita hii bado ni ngumu
 
Hii ndio mbaya sasa...inabidi tuwaweke na mdj wetu sasa maana ma dj wa kibongo nao mapenzi mengi hawajui hata mambo yanavyokwenda kwenye nchi yao na hata hawajisumbui kutaka kujua wao ni mapenzi na starehe ..hii ndio shida...sipati picha Clouds fm dj anakua Jmushi na East afrika fm dj anakua Mzozo wa mizozo nafikiri hapo tutafika tunakokutaka

Kusaga ndiye OWNER na yeye aongee na vijana wake kwasababu tunamwambia ukweli kuwa huu ni wakati muhimu kabisa kama miaka ile ya 1950's na 1960's.
Wakati ambako kuna msuguano mbaya kati yetu na sera za IMPERIALISM.
Hivyo tuweke balance na ujumbe ndo huo.
 
Mungu asaideie kwamba na KuSAGA na yeye awe ni Mpinga ufisadi..lakini sioni hilo...na kama na yeye ni kibaraka wa ufisadi basi hii ni shughuli pevu...unaweza ukashangaa ukakuta nyimbo kama izo zinapigwa usiku tu tena wa saa saba.
 
si umeona sasa....mizengwe ishaanza..jana sijausikia tena siku nzima toka asubuhi..nilikua na earphones siku nzima na simu yangu lakini u cant beleive such a good song wanaibania wanapiga nyimbo ya matonya eti inaitwa Taxi Bubu'' ni ya mapenzi hiyo nafikiri ndio wanaifanyia promo sasa ivi....hivi hawa jamaa sio watanzania nini??????
 
Mi nlishasema ipeni mwezi tu hiyo nyimbo!!!!!
 
Hii ni shida kubwa sasa..kwanini juhudi hizi za wazi kabisa za kusaidia nchi yetu zinakwamishwa na watanzania wenzetu??????? inamaana hawa hawakerwi na matukio ya ufisadi wa wazi kabisa...naanza kuingiwa na fikra sasa za JF kuanzisha kituo chake cha radio..naona hayo yatakua ni mapinduzi halisi.
 
Wapo baadhi wanaimba kuhusu UFISADI lakini wengine wanaimba kwa kuogopa sikiliza
MR POLITICIAN-NAKAAYA
NIJAJE-JOH MAKINI
NAN'GATUKA-PROF J
 
Wapo baadhi wanaimba kuhusu UFISADI lakini wengine wanaimba kwa kuogopa sikiliza
MR POLITICIAN-NAKAAYA
NIJAJE-JOH MAKINI
NAN'GATUKA-PROF J

Dah hii nijaje ya Joe Makini sijawahi kuisikia hii
 
si umeona sasa....mizengwe ishaanza..jana sijausikia tena siku nzima toka asubuhi..nilikua na earphones siku nzima na simu yangu lakini u cant beleive such a good song wanaibania wanapiga nyimbo ya matonya eti inaitwa Taxi Bubu'' ni ya mapenzi hiyo nafikiri ndio wanaifanyia promo sasa ivi....hivi hawa jamaa sio watanzania nini??????

mmmh!! mbona you suond like Jmushi!! are you the same person....................
 
mmmh!! mbona you suond like Jmushi!! are you the same person....................

Haijalishi anavyo sound..Kama ni mwanamapinduzi we think the same.
Kusaga mwenyewe ndiyo wa kuingilia kati kwenye hili ili na yeye tusimfikirie kuwa ni fisadi.
Huyu jamaa ana influence kubwa sana kwenye jamii hasa hasa vijana na kama hataki nyimbo za kuwaelimisha vijana zaidi ya kumwandalia Rostama Azizi jukwaa the ni lazima tutajiuliza maswali!
Kwani kitendo kile ni ku counter balance malalamiko yetu hapa jf!
Kusaga usi idharau jf!
 
Ndio hao hao wenye mielekeo mibaya isiyoridhisha!
Unajuwa hata Kusaga mwenyewe alikuwa ana usemi wake "kULA RAHA MPAKA mUNGU ACHUKIE"
Sasa anatakiwa ajuwe kuwa this is God's time na akiyumba kwenye vita ya kumtetea myonge basi amuulize Rostama aliyemuandalia Press Conference!
Kuna matajiri wengine wana ROHO MBAYA SANA NA NDIO MAANA BONGO NI HOVYO TU!
Kwanini wasihakikishe kuwa wanapiga nyimbo base on requests?
Nashangaa sana ninapoambiwa kuwa eti pesa kiasi flani kinatosha kukupa air time kiasi flani.
Yote hayo Kusaga anayafumbia macho kwasababu hata yeye ni CORRUPT!
Nyie kina Venture pigeni hiyo miziki ya kizalendo na kama mmeshapokea pesa za mafisadi mtakipata.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom