tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 21,838
- 18,250
Mtayarishaji maarufu wa muziki nchini Tanzania ambaye pia ni mchambuzi wa muziki kupitia show ya Bongo Star Search, ndugu Joakim Kimaro, maarufu kama Master J, amekiri kuwa 99% ya wasanii hapa nchini wanatumia bangi ndio maana wanapenda kuimba nyimbo zinazohamasisha ngono, uhalifu na matumizi ya bangi.
Amesema bila kuficha kuwa karibu wasanii wote wanaorekodi nyimbo kwenye studio yake ya utayarishaji wa muziki wanavuta bangi, cocaine, mirungi na dawa nyingine za kulevya. Hata hivyo ameishauri serikali kuwachukulia hatua wasanii hawa kwani inaonekana kama vile serikali inawaogopa. Pamoja na kuvuta bangi hadharani na hata kwenye video wanazorekodi na pia kuvaa nguo zenye picha za majani ya bangi, serikali haijawahi kuwachukulia hatua hata moja.
Chanzo: Said Fella, Master Jay wafunguka msako wa wasanii ‘mateja’
MAONI YANGU
Tatizo la wasanii kula bangi waziwazi limekuwa sugu hapa nchini. Kuna msanii mmoja (jina nimelisahau) amekuwa teja kabisa kwa sababu ya matumizi ya bangi na dawa za kulevya. Nilifikiri serikali ingeweza kumakamata huyu mtu na kumhoji anakaopata dawa ili kuwabaini wauzaji lakini imekaa kimya kana kwamba hakuna kinachoendelea hapa nchini.
Ikiwa mamlaka za serikali zitaendelea kuwaogopa hawa mateja kwa sababu wanawatumia kwenye kampeni za kisiasa, miaka michache ijayo vijana wengi watakuwa mateja kwa kuwa vijana hupenda kuiga kila kitu kutoka kwa wasanii kuanzia mavazi nyimbo za ngono na uvutaji bangi.
Nawasilisha.