Vijana acheni kutupangia nyimbo za kusikiliza kwenye magari yetu

TUKANA UONE

JF-Expert Member
Jan 3, 2018
1,816
5,151
Ukihitaji salamu nenda mbeya kwao Lucas mwashambwa ukamsaidie kulima Mtama mkimaliza atakusalimia,kwangu utaambulia chuya Ukawalishe bata!

Sijajua siku hizi vijana wana matatizo gani!

Kwa mujibu wa Cheti changu cha Kuzaliwa(Birth Certificate) ni kwamba,nimezaliwa Tarehe 10/11/1989,Hivyo hivi sasa nina umri wa Miaka 34.

Vijana wengi wa sasa hivi wana Umri wa Miaka 18 - 30,Hivyo watu wengi wenye Umri wangu Vijana wa Kileo wanatuita "Wazee"🤣

Daaaah!,Hii dunia inakimbia sana walahi!

Sasa kuna kipindi nilikuwa naelekea Mkoa wa Arusha,Wilaya ya Karatu na nikaona niegeshe pale Mbezi mwisho karibu na stendi ya Magufuli ili nijipatie Vichwa kadhaa niende navyo uelekeo huo ili nipate kampani ya stori za hapa na pale,kiukweli sikuwatoza kabisa pesa na nilifanya hivyo kama sadaka tu ya Mwisho wa Mwaka kwasababu kipindi kile kulikuwa na shida kubwa ya usafiri kuelekea Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro,Hivyo nilitaka watu wa kubadirishana nao mawazo!.

Kwenye Gari yangu nilikuwa nasikiliza nyimbo za Kikongo za miaka hiyo(Nyimbo zilizonikuza),Nilikuwa nina flash kabisa ya nyimbo hizo!.

Muhimu
Mimi huwa ni mdau wa Muziki wa kikongo kwasababu ni muziki mzuri na huwa unanikumbusha mambo mengi sana,mimi huwa sisikilizi muziki wa Vijana wa kitanzania kwasababu huwa sivutiwi na aina ya miziki wanayofanya vijana wa kibongo!.

Ukikuta nasikiliza miziki ya kibongo basi itakuwa ya wasanii wa zamani lakini siyo wa kizazi kipya!.

Basi bana,pale mbezi wapiga debe wakaniletea watu kadhaa na kumbe wale watu walikuwa wa familia moja ikiyokuwa inaelekea Kilimanajaro maeneo ya Boma ng'ombe.

Wakati tukiwa njiani maeneo ya maili moja nikiendelea kula ngoma zangu za Kikongo ninazo zi-Admire, kuna dogo akataka nitoe nyimbo nazosikiliza nimuwekee wimbo uliokuwa unaitwa "Utatoa hutoi".

Nikajaribu kuwelesha dogo lakini nikaona kama kakomaa huku nikiwaangalia wazazi wake kila mmoja yuko bize na simu yake,nikasema "Wewe hunijui"!.

Nikamuuliza yule dogo huo wimbo kaimba msanii gani,dogo akadakia fasta hata kabla sijamaliza kumuuliza ya kwamba kauimba msanii anayejiita Dula Makabila!.

Mimi nikamwambia huo wimbo sina na sidhani kama nitakuwa nao,baada ya kumwambia vile yule dogo nikamtazama kwenye "Rear View Mirror" akamshitua mama yake huku akimnong'oneza jambo fulani!.

Maza mtu naye bila aibu akaaanza kujiongelesha eti nimuwekee wimbo wa Asha Mashauzi unaitwa "Siyo levo yako".

Kwa Upole na Staha nilijaribu kuwaeleza hizo nyimbo walizotaka wao sina kwenye flash yangu nikitegemea Mama na Baba watajiongeza! Kumbe nilikuwa nimebeba kondoo na siyo binadamu!

Baada ya kuona kero zimekuwa za kutosha,tulipofika sehemu inaitwa Lugoba niliwashusha wote watafute usafiri mwingine ambao watabadili nyimbo kadiri wapendavyo!,Mimi huyooooooooo nikaondoka zangu nikawaacha pale!.

Ingawa walitka kuwa wabishi nikawaambia nitawapiga bomba endapo wangeendelea kukatalia kwenye gari yangu!

Hebu fikiria vijana wa kileo wanasikiliza wimbo unaitwa "Chapati" 🤣🤣🤣

Aiseeee!

Ukipewa lifti vumilia hata kama nyimbo zinazopigwa huzipendi,Vinginevyo ni mwendo wa kuwashusha tu!

NB: UKIONA UNAONEWA,NUNUA GARI LAKO!
 
Una tabia kama zangu kwa upande wa nyimbo.
Umenizidi mwaka mmoja, Bongo flavour huwa sisikilizi, angalau zile za 2009 kushuka chini.

Mimi nyimbo zangu ni kama Juwatta Jazz, Msondo Ngoma, DDC Mlimani nk. Hata gospel huwa napenda za nyuma kidogo.

Kuna muda nikijisikia huwa nakula instruments tu za nyimbo za vitabuni au tenzi za rohoni.
 
Mkuu Vijana wa miaka yetu hawezi kusikiliza huu uchafu wa wasanii wa wasasa!

Huwa Na-Enjoy sana nyimbo za miaka yangu zilizonikuza na sitaki kabisa kwenye gari yangu kusikiliza nyimbo za vijana wa kileo wala Unga!

Eti niache Kumsiskiliza Yondo sister,Nimon tokilala,Mbilia beli na Tshala Muana eti niende kumsikiliza Zuchu,Are you Serious motherfuckers?

Zuchu atasikilizwa na watoto wehu wenzie
 
Una tabia kama zangu kwa upande wa nyimbo.
Umenizidi mwaka mmoja, Bongo flavour huwa sisikilizi, angalau zile za 2009 kushuka chini.

Mimi nyimbo zangu ni kama Juwatta Jazz, Msondo Ngoma, DDC Mlimani nk. Hata gospel huwa napenda za nyuma kidogo.

Kuna muda nikijisikia huwa nakula instruments tu za nyimbo za vitabuni au tenzi za rohoni.
Instrumental za Tenzi za Rohoni safi sana
 
Halafu mkuu wewe una huruma sana, mimi ningeendelea kusikiliza nyimbo zangu, natumia sana T1, hiyo family ningeishusha mikumi national park au kitonga pass, kwangu mimi hawa kenges wameunajisi muziki wa kitanzania, tumepoteza kabisa uasili wetu, hawa almasi na tembo na wengineo wanachopiga huwezi kutofautisha ni mziki wetu au kutoka gethos za Harlem, sikiliza jirani zetu, muziki wa kizazi kipya bado una beat za uasili wao
 
Mkuu hii miziki ya sasa ya vijana wa Kitanzania nadhani ni mwendawazimu tu ndiyo atakuwa anaisikiliza.

Miziki haina radha wala ujumbe wowote,mi miziki ya wasanii wa Tanzania ninayosikiliza ni kutoka kwa wasanii wa kitambo maana bado ina radha na inaujumbe mzuri!.
 
Halafu mkuu wewe una huruma sana, mimi ningeendelea kusikiliza nyimbo zangu, natumia sana T1, hiyo family ningeishusha mikumi national park au kitonga pass, kwangu mimi hawa kenges wameunajisi muziki wa kitanzania, tumepoteza kabisa uasili wetu, hawa almasi na tembo na wengineo wanachopiga huwezi kutofautisha ni mziki wetu au kutoka gethos za Harlem, sikiliza jirani zetu, muziki wa kizazi kipya bado una beat za uasili wao
Asingeweza kuwashusha huko kwa maana ukiwa unaenda mikoa ya Kaskazini haupiti mikumi.
 
Dunia ya leo imekosa nidhamu kabisa. Watu hawana uoga na vitu vya watu na wala hawajui tofauti ya hisani na stahiki.

Kulikuwa na kijana ninaishi nae karibu. Ilikuwa kaajiriwa maeneo ya posta kwa vile na mimi shughuli zangu nafanyia mjini ikawa kila nikikutana nae njiani nampa lift.

Mazoea yakajenga tabia kufikia kijana kunipigia simu asubuhi kuwa nimsubiri anatoka ama jioni kunambia nimsubiri kituoni. Mwanzo niliona sawa ila iligeuka kuwa kero pale anaponiweka mpaka dk 20 eti kachelewa kuamka.

Nilipofika ukomo wa hisani yangu kwake ni pale alipokuja kunigongea asubuhi moja kuniuliza mbona nimechelewa na simu sipokei. Nikamwambia nina dharula zangu hivyo siendi mjini siku hiyo.
Bwana mdogo akaanza kufoka, kwanini sikumjulisha kabla ili afanye mpango mwingine wa usafiri. Aliongea kama vile ilikuwa ni wajibu wangu kumpeleka kila siku.

Yule dogo ilikuwa hajawahi kuona upande wangu mwingine. Daima aliniona mtu mkimya. Nilimbadilikia na matusi na kumtoa mbio kwangu kama mwizi.

Hiki kizazi cha sasa kimekosa staha na aibu, asubuhi iliyofuata bado alikuwa na ujasiri wa kunipigia kuuliza kama naenda mjini.
Nilimwambia naenda ila bila yeye, afanye mpango wa usafiri wake tu.
 
Yaani tabia yako ya yangu kuhusu muziki zinafanana 100% ila kasoro mie sina gari kwa hiyo nikisafiri lazima nibebe earpod au earphone maana nyimbo wanazowekaga kwenye mabasi sizielewi kabisa. Mtu anaacha kusikiliza 100 kilos au Kinshasa za Ferre Gola 'le padre' eti anasikiliza sijui chapati.
 
Back
Top Bottom