Safari ya Wagosi wa Kaya kimuziki

101 East

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
1,040
2,121
WAGOSI WALIINGIA DAR KAMA BARUA YENYE STAMP NA CARE OF


Wagosi wa Kaya ni kikundi cha wanamuziki kutoka Tanzania, kilichoanzishwa mwaka 1996 na John Simba (Dr John) na Frederick Mariki (anayejulikana kama Mkoloni).

Walitoa nyimbo zinazojadili masuala yanayokabili jamii ya Tanzania kama hali ya hospitali, rushwa, ufisadi na viongozi kutowajibika.

Miaka 22 iliyopita, Wagosi wa Kaya, walisafiri kutoka Tanga hadi Dar es Salaam, mithili ya barua yenye stamp na care of.

Profesa Jay ndiye mwezesha safari. Akawagonga stamp Tanga. Akawaambia, mkifika Ubungo, ongozeni mpaka Sinza Mori. Care of ni Profesa Ludigo. MJ Production, Masaki, ndio main address.

Usafiri wa kufika Dar kutoka Tanga ni hisani ya rafiki wa kila mtu, Fredy Tayasar. Mfukoni walikuwa na Sh50,000, walizopewa na Rogers Mynas kwa ajili ya kulipia studio.

Mwonekano wao tofauti na utamaduni wa walichojinasibu kukifanya. Suruali za vitambaa na mashati ya bahama. Chini four angle shoes. Havioani na personalities za Hip Hop.

Ludigo ni Mnyamwezi minded. Alisimama getini na kikombe cha chai. Akawaambia Wagosi “simameni hapohapo”. Akawatazama juu mpaka chini. Akauliza: “Ninyi mnajua kurap kweli?”

Balaa lilikuja Ludigo alipowaambia wamchanie mistari palepale getini, nyumbani kwake. Wagosi walifungua Mzinga wa Nyuki. Tanga Kunani haikufika kati, Ludigo alitelekeza kikombe cha chai getini, akawaambia Wagosi; “Twendeni.”

Safari kutoka Sinza hadi Masaki MJ. Moja kwa moja studio. Pishi Tanga Kunani likaiva. CEO wa MJ, Master Jay, aliposikiliza pini, akasema “sichukui hela yenu”. Kisha, aliwaita major players wote wa Bongo Flava League kusikiliza divine kutoka Tanga.

Wimbo Tanga Kunani uligombewa studio. Kila mtu aliuchota ili akawe wa kwanza kuucheza redioni. Maulid Kitenge alishinda battle alipovunja sheria, akaucheza Tanga Kunani kwenye kipindi cha michezo, Spoti Leo, Radio One. Ni mwaka 2001.

Ile safari ina neema nyingi. Wagosi wa Kaya ni kurunzi lililomulika kila kero ya kijamii Tanzania. Usiongee “Wauguzi”, “Traffic” wala “Taxi Driver”, Wagosi walimlazimisha hadi “Kibaka” kuokoka.

Utumishi wao uliotukuka ndio sababu Bongo Flava Honors watawatunuku Wagosi wa Kaya plaque maalum, kutambua mchango wao wenye thamani kubwa kwenye ukuaji wa Bongo Flava na sanaa Tanzania.

Shughuli ni Oktoba 27, 2023. Alliance Francaise, Upanga. Siku hiyo, Wagosi watapiga shoo ya live band nyimbo zao zote.

Mwenyeji wa shughuli ni The Godfather, Sugu The Jongwe.

Mtunzi: Luqman MALOTO
@TheRealJongwe
20231020_083543.jpg
 
Hata wewe unawajua hawa wakali

Njoo chukua nyota zako, nakupa nyota 3 leo leo 🤪🙌
Ndiooo kipindi hiko nasoma
🤣🤣🤣
Acha kabisaa na yule Masai aliyekufa jmn!
Badae ndo akaja diamond hapo Niko Sekondary na wimbo kamwambie.....🤣
 
Ndiooo kipindi hiko nasoma
🤣🤣🤣
Acha kabisaa na yule Masai aliyekufa jmn!
Badae ndo akaja diamond hapo Niko Sekondary na wimbo kamwambie.....🤣
Hongera, pamoja na ratiba ya shule lakini bado ulitenga muda wa kufurahia maisha.

Ukipata nafasi weekend nipeleke Bendi nikafurahia maisha na Wazee wenzangu pale DDC Mlimani Park, maana huwa napata shida kuvuka barabara kwa Uzee huu 🤪
 
Hongera, pamoja na ratiba ya shule lakini bado ulitenga muda wa kufurahia maisha.

Ukipata nafasi weekend nipeleke Bendi nikafurahia maisha na Wazee wenzangu pale DDC Mlimani Park, maana huwa napata shida kuvuka barabara kwa Uzee huu 🤪
🤣🤣
Kipindi hiko shule in Sheria Kali lkn unatoroka🙌🙌

Hahaaa Kwa uzee upi ss ulio nao...
Wengi tuliosikiliza nyimbo hizi tuko kati ya 30+....km mkubwa sn labda 40-45

Ubaya sshv nilishahama huo upande , nasikiliza gospel tu Mzee 🤣
 
Back
Top Bottom