Ahadi za Makamu wa Rais Tanzania kwa Wananchi wa Jimbo la Arumeru Magharibi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

MBUNGE NOAH SAPUTU - AHADI ZA MAKAMU WA RAIS KWA WANANCHI WA JIMBO LA ARUMERU MAGHARIBI​

Makamu wa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdori Mpango, ametoa maagizo kwa Mamlaka husika kupitia Mawaziri wenye dhamana kutatua kero zinazowakabili wananchi wa halmashauri ya Arusha, zilizowasilishwa Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi Mhe. Noah Lembis Saput.

Mhe. Mpango ametoa maagizo hayo, wakati akiwahutubia wananchi hao, mara baada ya kuweka jiwe la msingi barabara ya Mianzi - Olemringarika, eneo la Ngaramtoni kata ya Olturumet, halmashauri ya Arusha.

Hata hivyo Mhe. Dkt. Mpango ametoa pole kwa wahanga wote wa changamoto hizo na kumuagiza Mkurugenzi wa TARURA nchini kusimamia matengenzo ya barabara za ndani za zilizoharibiwa na mvua kubwa zilizonyesha katika msimu huu wa mvua zikikata mawasiliano kwa baadhi ya maeneo na kusababisha adha kubwa kwa wakazi wa maeneo hayo.

Aidha amemuagiza Meneja wa TARURA mkoa wa Arusha kuangalia salio la bajeti na kudhibiti korongo lililo pembeni ya kanisa Katoliki Ngaramtoni, korongo linalotishia usalama wa jengo hilo na waumini wa kanisa hilo.

Dkt Mpango ameiagiza Mamlaka ya Chakula NFRA kuangalia upya namna ya kuenendelea kutoa chakula cha ruzuku kwa watu wenye uhaba wa chakula, changamoto iliyosababishwa na ukame uliyakabili eneo kubwa katika jimbo hilo.

Kadhalika, amemtaka pia Waziri wa Maji kwa kushirikina na Mkurugenzi wa RUWASA kuongeza nguvu ya kusimamia miradi ya maji katika jimbo hilo, miradi ambayo imetaarifiwa na Mhe. Mbunge huyo kutekelezwa kwa muda mrefu bila kukamilika.

Na mwisho kabisa, amemuagiza Waziri mwenye dhamana TAMISEMI kufanyia kazi ombi la kuigawa wilaya ya Arumemeru kutokana na ukubwa wa eneo hilo na wananchi kupata adha ya kufika ofisi ya mkuu wa wilaya na kupata huduma, ombi ambalo lilitolewa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha, Comredi Steven Zelothe Steven.

"Kuna gharama kubwa katika kugawa na kuongeza maeneo ya kiutawala, lakini Mkoa na TAMISEMI fanyieni kazi upya na kuangalia uwezekano wa kugawa wilaya hiyo kwa dharura kwa kuzingatia vigezo vinavyohitajika kuwa wilaya" Amefafanua Mhe. Dkt. Mpango
 

Attachments

  • FwbJ7ViWABQ4bn_.jpg
    FwbJ7ViWABQ4bn_.jpg
    67 KB · Views: 1
  • FwbJ7ioXsAAyFgs.jpg
    FwbJ7ioXsAAyFgs.jpg
    42.1 KB · Views: 2
  • FwahCBpaIAI9JgI.jpg
    FwahCBpaIAI9JgI.jpg
    48.7 KB · Views: 2
Back
Top Bottom