Agizo lingine la Serikali ya Magufuli lapuuzwa

Agizo lingine la Serikali ya Magufuli lapuuzwa

Wacha kulalamika wewe. Kama kwa miaka mitatu yote umeweza kusomesha mtoto kwa mil 7 leo mil 8 itakushinda? Kalipe bana mtoto akasome.
Mkuu miaka Ya Nyuma per diem na posho kibao zilikwepo, sasa hivi zimefutwa kwa hiyo kuna kuyumba kidogo kiuchumi
 
Kwanza ufuatiliwe uliwezaje kupata ada hiyo 7 million kihalali kabla ya kuwaulizia feza schools ambao wanafanya biashara halali.Hulazimishwi kwenda pale. Iacheni serekali ifanye mambo mengine. Mbona huuulizie kwanini sehemu nyingine soda ni 2000 na bia 8000.Unaenda kwa hiari unalipa.Huweze acha.

Nawe umeishiwa sasa! Lini ktk nchi hii ulisikia elimu ikiwa ni biashara?
Jamani siyo kila kitu uchangie! Unalinganisha soda na elimu!
 
uwezi kulipia izo ela peleka mwanao panapokulingana bwana izi ni enzi za kiubepali
 
Ha ha ha uwa najiuliza maswali mengi sana kuhusu maisha na uhalisia, huyu anampeleka mtoto shule mil 8 usikute ndugu zake kibao hata ada ya kayumba hawana. Yupo mtu atakuja kusema hapa inamusu nini, ajabu ni hii pamoja na kusoma feza bado mtoto anapata elimu anakuwa si bora zaidi ya kujua kingereza and worse enough wengi tutakutana UDSM, UDOM, SAUT, MZUMBE mzee wa njia za kayumba unawafukuza vibaya.

Ni maamuzi mabaya na mengi yanatokana na ulimbukeni. Kipindi kilichopita, wizi ulishamili na wasio hata ufahamu wakapata pesa. Njia ya kujionyesha ilikuwa ni matumizi ya kipuuzi kama haya ya kulipa mil. 7 sekondari.

Bila hata hiyo nyongeza isiyo halali, hapakuwa na sense ya kulipa mil. 7 kwa shule ya TZ inayomilikiwa na mturuki ambaye hata kwao wako nyuma kielimu kulingana na nchi zingine za ulaya.
 
kwa kweli nimelipa kama kuingia wako juu kidogo kama M4.5 arround hapo then baadae ni m4.3 lakini ukisha lipa hiyo hakuna cha uniform, hela ya chakula, kalamu, sijui madaftari, hakuna chochote unalipa tena, kama ni form one kuna laki2 za pre form one wanasoma kama week 3 hivi then mtihani

Fika wako Bunju beach pale kuna mwalimu anaitwa Ustadh Salumu atakuelekeza yote au nitakutafutia namba ya simu ila kwa form one umechelewa maana mwaka huu wakipata wanafuzi wengi sana ikabidi wafanye test kuwapunguza wengine maana darasa lao ni wanafuzi 45 tu

Ahsante mkuu kwa taarifa, kijana wangu bado yupo std six, nitajitahidi kufika pale nikaone mazingira, nikiwa b.moyo road naingilia wapi kwa gar?
 
Hii sio point..swala ni kwamba Feza wamekiuka agizo la serikali kutopandisha ada...!

Mada yake unaweza ijibu kwa kadiri Ya kipengere ulichokipenda, kwa mfano mwingine anaweza jibu sehemu ya uhamisho, mwingine akajibu kupuuzwa kwa agizo
 
Mabadiliko ni wewe. Usisubirie magufuli. Badilikeni kwa kuwapeleka watoto shule za kawaida. La sivyo kalipe.Hongera .Na wanapokuwa wa kwanza kitaifa mbona huongei.
Huwa mnachekesha sana tena sana huwa zikiletwa mada za kuwashauri watu wapeleke watoto wao shule za serikali nyie ndio huwa wa kwanza kupinga na kusema hamuwezi kuwapeleka huko maana hakuna elimu bora lakini mwenzenu kajikongoja kampeleka pazuri anapo ona leo mnaanza kumshauri eti ampeleke shule za kawaida!

Ukweli ni kwamba Elimu kwenye shule zetu za serikali imebadilika sana na si nzuri tena labda zile special!

Mtu kulipa M7 haimaanishi sasa basi watu waendelee kukiuka maaigizo ya serikali..nilitegemea tujikite kuhoji ni kwanini agizo la serikali lime kiukwa?
 
Kwanza ufuatiliwe uliwezaje kupata ada hiyo 7 million kihalali kabla ya kuwaulizia feza schools ambao wanafanya biashara halali.Hulazimishwi kwenda pale. Iacheni serekali ifanye mambo mengine. Mbona huuulizie kwanini sehemu nyingine soda ni 2000 na bia 8000.Unaenda kwa hiari unalipa.Huweze acha.
Kwani unafikiri kila mtu anafanya kazi serikalini? Leo hii mnageuka kuwatetea wanao kiuka maagizo ya serikali? Feza wanatakiwa kufata sheria za nchi ..nilitegemea sote tuungane kuhoji kwanini wana kihuka maagizo ya serikali?
Kinyume na hapo mnamshambulia mtoa mada..mnatakiwa kujua si kila anaye lipa ada M7 ni mwizi na fisadi..!
Acha kelele wewe kwani nani alikutuma umpeleke mtoto wako kwenye shule za gharama wakati syllabus ni zilezile??
 
mbona unalialia sanaa kwan shule za kata huzioniiii...unapenda vizuri unaogopa gharama...mbona hata ukienda kwenye hotel za kimataifa soda inauzwa 5000...uswahilin 700...usikae kulaumu nenda sehemu ambapo unauwezo napo
 
Lipa lai moja mtoto anapata elimu na huduma nyingine zenye hadhi ya laki moja. Lipa milioni nane mtoto atapata huduma na elimu ya milioni nane. Kupanga ni kuchagua. Ada ya Feza haijaongezeka ila kuna baadhi ya huduma michango imeongezeka kulingana na kuongezeka kwa bei za bidhaa sokoni.

Nifafanulie tafadhali michango ipi na kutokana na bei iliyopanda kwa % ngapi? Haya ndio mlitakiwa kujadiliana na wazazi ili tuone tunafanyaje?
Je ni Tshirts?
Au ni mikate?
Au mishahara ya wapishi wakituruki?
 
Kwanza wazazi/walezi tuliambiwa tusubiri tusilipe ada za shule za private mpaka tarehe 16 Dec 2015 serikali itakapotoa muongozo.

Baadaye serikali ikatoa agizo kwa shule za private zisipandishe ada kabla ya kujadiliana na wazazi na wizara kuhusu mabadiliko hayo.

FEZA SCHOOLS wamekiuka agizo hilo kwa kupandisha ada za sekondari bila kukaa na wazazi kutoka 7,250,000 hadi 8,300,000.

Na mbaya zaidi 1st instalment wanataka 4,050,000 (ada huwa inalipwa kwa instalment 3).
Sasa kama binti/kijana yuko form four utamuhamishaje? Shule nyingi hawapokei wanafunzi wa form four.

Muheshimiwa Rais, hii sio FEZA international.; ni shule inayofuata silabasi ya Taifa. Je hawa waturuki wako juu ya sheria?

Unampeleka mwanao Feza kwani wewe ni Masamaki !?
 
Kiasi hicho cha ada ya mwaka mmoja hapo FEZA ina maana wazazi wataweza kuwasomesha watoto wao elimu ya chuo ktk nchi ya Uholanzi kwa mwaka kama ada ya tuition, fanyeni hima wakimaliza hapo FEZA wapelekeni ngambo wakapate exposure na elimu Uholanzi UK student numbers surge in Netherlands - BBC News na kuwapa nafasi watoto wa walalahoi nafasi nyingi kujiunga ktk vyuo vikuu na mikopo ya elimu ya juu.

There are tuition fees of 2,000 euros (around ?1,400) per year and students from the UK can apply for support for this.
But they cannot get financial support for living costs, so parents will have to pay for accommodation or students need to get part-time jobs.
The typical room cost is about 360 euro (?254) per month, says the university.
 
Kuna suluhisho moja tu, ukipitia shule inayozidi ada ya chuo kwa mwaka basi ni marufuku kuomba mkopo, kwanini serikali ihangaike na hawa watu? Dawa ni ndogo tu, kuanzia admission mpaka mikopo priority iwe wale walipitia kwenye shule za ada ndogo tuone kama mtathubutu na mkifanya hivyo mtaepusha zile dhuruma zenu za kujipatia mikopo na kuwaacha watoto wa mlalahoi akikosa tena na kuacha kuendelea na masomo
 
Inashangaza kumpeleka mtoto shule ya mil 7 halafu unailalamikia serikali....

Karibuni st katumba...michango na ada hata laki 3 haifiki


Na bado mtoto huyo akifikia elimu ya chuo kikuu kilio cha mkopo wa 100% unaliliwa kwa nguvu zote.
 
Mwaka jana walipandisha kutoka 6 to 7m, uliona tulikuja kulalamika? Wenye kuhamisha walihamisha.
Tumeilalamikia serikali kwasababu ilijitanabaisha kuwa ina uwezo wa kuratibu ada za private schools. So we are holding to their words. Nikiwa mdogo nilifundishwa kutoahidi kitu kama siwezi timiza.

Sasa Dada yangu Kaunga unadhani Feza Schools watashusha ada toka 8.3M hadi 350K?

Mwisho wa siku mkiwalazimisha watawaambia tumefunga huduma Tanzania, wachukueni watoto wenu.

Wewe lipa hiyo ada tu manake hakuna kitakachobadilika.

Na sio Feza tu, shule zote binafai nchi nzima hata zile wanazolipa hata 1.5M, hawatakubali kushusha na zaidi watazidi kupandisha.
 
Nawe umeishiwa sasa! Lini ktk nchi hii ulisikia elimu ikiwa ni biashara?
Jamani siyo kila kitu uchangie! Unalinganisha soda na elimu!

Elimu ni biashara, dunia nzima ipo hivyo tofauti na nchi za kicomunist.
 
Mwaka jana walipandisha kutoka 6 to 7m, uliona tulikuja kulalamika? Wenye kuhamisha walihamisha.
Tumeilalamikia serikali kwasababu ilijitanabaisha kuwa ina uwezo wa kuratibu ada za private schools. So we are holding to their words. Nikiwa mdogo nilifundishwa kutoahidi kitu kama siwezi timiza.
Ningekushauri utafute utaratibu mwingine kwani Katibu mkuu, Mchome, kama wiki mbili zilizopita aligeuka na kusema wizari haijawahi kutoa ahadi ya kutaja ada elekezi kwa sekondari za binafsi.
 
kwanza wazazi/walezi tuliambiwa tusubiri tusilipe ada za shule za private mpaka tarehe 16 dec 2015 serikali itakapotoa muongozo.

Baadaye serikali ikatoa agizo kwa shule za private zisipandishe ada kabla ya kujadiliana na wazazi na wizara kuhusu mabadiliko hayo.

Feza schools wamekiuka agizo hilo kwa kupandisha ada za sekondari bila kukaa na wazazi kutoka 7,250,000 hadi 8,300,000.

Na mbaya zaidi 1st instalment wanataka 4,050,000 (ada huwa inalipwa kwa instalment 3).
Sasa kama binti/kijana yuko form four utamuhamishaje? Shule nyingi hawapokei wanafunzi wa form four.

Muheshimiwa rais, hii sio feza international.; ni shule inayofuata silabasi ya taifa. Je hawa waturuki wako juu ya sheria?
shule za bure zipo unalalamika nini? Kwani lazima asome feza?
 
​nyie mnataka lueta ujinga wenu,kwani mtoto wako lazima asome Feza?
 
Back
Top Bottom