Agizo lingine la Serikali ya Magufuli lapuuzwa

Agizo lingine la Serikali ya Magufuli lapuuzwa

Serikali yetu ingekuwa ina watu wanaojua ku deal na ishu kama hizi basi hili swala wangelinyamazia tu, suluhisho ni kuboresha shule zake tu, tena ingewezekana ningekaribisha uwekezaji wa shule nyingi kama feza na ada iwe kubwa hivyohivyo ili tupunguze mzigo wa watu wanaoitegemea serikali. Jambo hili lingewapelekea kutunga sheria nzuri sana za elimu ya juu hasa kwenye mikopo, kwa kifupi tu wangepitisha sheria inayopiga marufuku kutoa mikopo kupitia bodi yake kwa mtu aliyesoma shule ada inazidi ya degree anayotaka kusoma, hapa tungeweza kuwasaidia watanzania wanastahil kukopeshwa, anayehitaji mkopo kwa hawa watu waliosoma ada mil 8 wakakope benk na sio serikal. Ifike hatua serikali ifanye biashara pia, na hizi shule kama zinatoza ada kubwa serikali ikakusanye kodi.

Ninasomesha mtoto wa marehemu dada yangu ambaye baba yake alimtelekeza tangu tumboni UDSM hakupata mkopo hata asilimia.005 na A level alisoma shule moja na Joseph John Pombe Magufuli (si FEZA) ni mwaka wa 3 sasa.

Na serikali hiyo hiyo ilisema yatima watapewa kipaumbele. So serikali sio ya kuitegemea sana
 
Mnalalamika wakati mmeyataka wenyewe, hizo shule ni kama Samaki Samaki Bar, unauziwa bia ilr ile ya TBL kwa bei mara tatu kwa kupenda sifa tu... Mbona shule za Seminari zinatoa elimu bora kwa bei ya kitonga?
 
Sisi ndio tulitoa agizo au kiherehere cha serikali?
Kabla ya kauli ya serikali ulishaniona nikilalamika?
 
MWANAO ALIPO ANZA FORM ONE HUKUJUA HILO hukujiuliza je likitokea plan B itakuwaje, MHAMISHE KUNA SHULE ZA MILIONI 2 AU 3 MTAANI HUKU WATAMPOKEA HATAKAMA NI FORM FOUR, KWA KUWA AMETOKA KWENYE SPOON FEEDING
 
MWANAO ALIPO ANZA FORM ONE HUKUJUA HILO hukujiuliza je likitokea plan B itakuwaje, MHAMISHE KUNA SHULE ZA MILIONI 2 AU 3 MTAANI HUKU WATAMPOKEA HATAKAMA NI FORM FOUR, KWA KUWA AMETOKA KWENYE SPOON FEEDING INTERNATIONAL SCHOOL
 
Mnashangaa Ada ya FEZA wakati Kuna BRAEBURN arusha Ada ni us dola 12,000/= kwa mwaka?watu wana hela jamani.
 
Muwe mnafikiria anachofanya Magufuli ni sanaa kwa watz,hawez kuendelea na hii mipango,mbona kahamishia watoto Feza,ina maana hajui huko fees ni kubwa au kwa kuwa serikali ndiyo inalipa?
 
Mkuu, mwaka huu tunapata shida kwa sababu mianya yote imezibwa. Tulitegemea pesa ya sherehe ya UHURU tuzipige kiasi mgao tupate ada, mwishowe sherehe ikayeyuka, Safari za nje twende tupate per diem nazo zikayeyuka, Pale bandarini tupige uingizaji mizigo nayo ikayeyuka, Tuokote za wakwepa kodi ili waishi free nayo ikayeyuka, zile tulizificha katika ndoo chini ya uvungu wa kitanda nazo jamaa wakachukua, tulitegemea kodi ya nyumba zetu zile 73 daaaa jamaa akatushitukia!!!!!

DAAAAAAAA!!!!!!!!!!! hivi unafikiri mwaka huu watoto wataenda kweli kwa ADA YA mil.8.

Yaani tunatamani kuwarudisha shule za kata ingawa tunajisikia AIBU mtaani!!!!!!!

LAKINI TUNAANGALIA HUENDA NI UPEPO HUU UTAPITa, TUTARUDI KATIKA MISHEMISHE ZETU KAMA KAWA!!!!!!
Nakumbuka enzi hizo kuna rafiki yangu Mhindi alinieleza kuwa sie Watanzania-wabantu tuna matatizo. Ukipata fedha familia inajua na ukikosa fedha familia inajua vile vile. Akazidi kunieleza kuwa ndo maana tunanyanyaswa na wake zetu na siku nyingine kudharaulika na watoto. Akasema kwao wahindi akipata fedha familia haiwezi kujua maana kwa kawaida wao huwa na life style ambayo ni standard. Kama hana fedha familia inadunda na akipata fedha inaiweka benki si siku hiyo kununua kilo 10 za nyama ili kila mtu mtaani aone kuwa naye kapata fedha. Hili la Kaunga kulalama ni mfano hai maana kutegemea fedha za madili ili ukasomeshe watoto au kutunza familia huu ndiyo msala. Mtoto au familia inatunzwa na kipato halali
 
Ndio maisha yetu Watanzania. Kwa kipato cha mfanyakazi wa hali ya chini katika akaunti zetu mshahara ukiingia tunaenda kuzitoa zote na hakuna akiba inayobaki kwani kamshahara ni kadogo.

Hivyo lazima familiya itajua kuwa leo baba / mama kafulia hana kitu mfukoni na siku ukizipata ndipo unafanya vitu kuwaridhisha watoto.
 
Elimu ni biashara, dunia nzima ipo hivyo tofauti na nchi za kicomunist.

Naomba niwe mpole tu maana kumbe tunatofautiana viwango. Nakushauri utumie googles, tafuta maana ya social services. Ukiipata nchi iliyoiweka elimu ktk shughuli za biashara nipe pm.
 
kila shule ina ubora wake na uwezo wake wa kufundisha, ndo maana wazazi wanaangalia ni wapi panawafaa zaidi kuwapeleka wtoto wao, na oia wana jua uwezo walionao ndo maana wana wapeleka huko bila kujali kua kua shule za bi nafuu( kabla hazijawa bure) za serikali. Sana kama wanona haziwafai kwa hilo ongezeko kiduchu basi wawatoe na wale wtakaoweza kulipa basi na waendelee. Serikali haiwezi ingilia kila jambo la binafsi hata kama linaingilia kwa namna moja ama nyingine. Kwanza cheki mazingira tu ya hiyo shula yanavyo ring bells ndo utajua gharama yake, uwezo wa walimu na halli ya ufundishaji pia.
 
kila shule ina ubora wake na uwezo wake wa kufundisha, ndo maana wazazi wanaangalia ni wapi panawafaa zaidi kuwapeleka watoto wao, na pia wanajua uwezo walionao ndo maana wana wapeleka huko bila kujali kua kuna shule za bei nafuu( kabla hazijawa bure) za serikali. Sana kama wanaona haziwafai kwa hilo ongezeko kiduchu basi wawatoe na wale watakaoweza kulipa basi na waendelee. Serikali haiwezi ingilia kila jambo la binafsi hata kama linaingilia kwa namna moja ama nyingine. Kwanza cheki mazingira tu ya hiyo shule yanavyo ring bells ndo utajua gharama yake, uwezo wa walimu na halli ya ufundishaji pia.
 
Nakubaliana nawe 100%, mwaka jana nilimtembelea rafiki yangu ambaye anakaa Uingereza. Kwa muda mrefu alikuwa amewaacha watoto wake wakisoma katika shule za kawaida huku Tanzania.Akanieleza imebidi awahamishie watoto wake Tusiime kabla ya kuwahamishia Uingereza. Nikamwuliza ni kwa nini anafanya hivyo, akasema kuwa iwapo watakwenda huko na kiwango cha chini wataingia katika shule za viwango vya chini na hata University watakwenda katika shule za namna hiyo hiyo. Matokeo yake hawawezi kupata ajira nzuri na hata maarifa ya kutosha kufanya kazi binafsi. Haitatokea hata wakati mmoja watu wote wakawa na kipato kinachofanana. Cha msingi Serikali iboreshe shule zake na hizo shule za private zitafunga zenyewe au zitashusha bei kwani hakuna atakayezikimbilia. " Chema chajiuza kibaya chajitembeza"
 
Watoto wanaosoma fedha ni wale vilaza tu.Tunakutana nao vyuoni tunatoka na dist.wao wanayoka na third claa na hata gentleman degree wengi wao.

Unahangaika kumpeleka feza labda kama ana akili za kubust.
 
Back
Top Bottom