Agizo lingine la Serikali ya Magufuli lapuuzwa

Agizo lingine la Serikali ya Magufuli lapuuzwa

Wiki tatu zilizopita kulikuwa na uzi humu ukisema. Watoto watatu John Pombe wamehamishiwa huko FEZA, kama sikosei.
(Naomba kusahihishwa kama sipo sahihi). Sasa sijui naye atajichunguza!

Hujakosea wapo huko, ila sijui kama kuna uchunguzi hapa
 
Basi hizo shule za kata zihesabu maumivu tu
cc Nyani Ngabu Dark City Nguruvi3 ...

Mkuu kila mtu nji hii ni jipu kwa upande wake. Solution ni kutumbuana kwa zamu ila mie niwe wa mwisho.

Inanikumbusha enzi za utoto. Tukikosea dingi anasema tuchapane fimbo tatu. Ukiwa wa mwisho unafanya kweli kwa sababu mwenzako hana nafasi tena.
 
Serikali yetu ingekuwa ina watu wanaojua ku deal na ishu kama hizi basi hili swala wangelinyamazia tu, suluhisho ni kuboresha shule zake tu, tena ingewezekana ningekaribisha uwekezaji wa shule nyingi kama feza na ada iwe kubwa hivyohivyo ili tupunguze mzigo wa watu wanaoitegemea serikali. Jambo hili lingewapelekea kutunga sheria nzuri sana za elimu ya juu hasa kwenye mikopo, kwa kifupi tu wangepitisha sheria inayopiga marufuku kutoa mikopo kupitia bodi yake kwa mtu aliyesoma shule ada inazidi ya degree anayotaka kusoma, hapa tungeweza kuwasaidia watanzania wanastahil kukopeshwa, anayehitaji mkopo kwa hawa watu waliosoma ada mil 8 wakakope benk na sio serikal. Ifike hatua serikali ifanye biashara pia, na hizi shule kama zinatoza ada kubwa serikali ikakusanye kodi.
 
Karibuni huku kwa st. Kayumba schools.safari hii ni bure tu. Hizo feza schools muwaachie akina mwanaasha - - -
 
Huwa mnachekesha sana tena sana huwa zikiletwa mada za kuwashauri watu wapeleke watoto wao shule za serikali nyie ndio huwa wa kwanza kupinga na kusema hamuwezi kuwapeleka huko maana hakuna elimu bora lakini mwenzenu kajikongoja kampeleka pazuri anapo ona leo mnaanza kumshauri eti ampeleke shule za kawaida!

Ukweli ni kwamba Elimu kwenye shule zetu za serikali imebadilika sana na si nzuri tena labda zile special!

Mtu kulipa M7 haimaanishi sasa basi watu waendelee kukiuka maaigizo ya serikali..nilitegemea tujikite kuhoji ni kwanini agizo la serikali lime kiukwa?

Kwani unafikiri kila mtu anafanya kazi serikalini? Leo hii mnageuka kuwatetea wanao kiuka maagizo ya serikali? Feza wanatakiwa kufata sheria za nchi ..nilitegemea sote tuungane kuhoji kwanini wana kihuka maagizo ya serikali?
Kinyume na hapo mnamshambulia mtoa mada..mnatakiwa kujua si kila anaye lipa ada M7 ni mwizi na fisadi..!

Ningekushauri utafute utaratibu mwingine kwani Katibu mkuu, Mchome, kama wiki mbili zilizopita aligeuka na kusema wizari haijawahi kutoa ahadi ya kutaja ada elekezi kwa sekondari za binafsi.

Aanze na uchunguzi kwa wote wanaosomesha watoto wao huko lazima kuna majipu kibao

Wiki tatu zilizopita kulikuwa na uzi humu ukisema. Watoto watatu John Pombe wamehamishiwa huko FEZA, kama sikosei.
(Naomba kusahihishwa kama sipo sahihi). Sasa sijui naye atajichunguza!

Hujakosea wapo huko, ila sijui kama kuna uchunguzi hapa

Basi hizo shule za kata zihesabu maumivu tu
cc Nyani Ngabu Dark City Nguruvi3 ...

Watoto wa mkulu wapo huko FEZA. Akili mkichwa
 
Last edited by a moderator:
This is too much
jadili mada na sio mtoa mada
hujui unacho zungumza

Mada gani !? Even you .you need a deliverency from that boss behavior. Or otherwise understood that when your blessed is for you to bless others whether spiritual or riches .
 
Mada gani !? Even you .you need a deliverency from that boss behavior. Or otherwise understood that when your blessed is for you to bless others whether spiritual or riches .

Ungeandika kiswahili ungeeleweka vizur sana ila hiyo lugha unayotumia ni kubwa kuliko wewe.
 
Watoto wa mkulu wapo huko FEZA. Akili mkichwa

Inawezekana waliuliza direct Ikulu kuhusu ada elekezi
na pengine wameona since watoto wa Ikulu wako hapo
mahitaji ya security yataongezeka hivyo waongeze pia ada...
 
Inashangaza kumpeleka mtoto shule ya mil 7 halafu unailalamikia serikali....

Karibuni st katumba...michango na ada hata laki 3 haifiki

Nimependa hii

Si ndio walioguswa na hapa kazo tu, pesa hakuna za kuchezea tena, sasa inabidi zitoke mifukoni.
 
Inawezekana waliuliza direct Ikulu kuhusu ada elekezi
na pengine wameona since watoto wa Ikulu wako hapo
mahitaji ya security yataongezeka hivyo waongeze pia ada...

Walinzi si wanapelekwa na vijana wetu wa Kikosi maalumu. vilevile?
 
Anzieni uchunguzi wa nani fisadi kwa kuchunguza watumishi wanaosomesha watoto wao shule binafsi zenye kutoza ada ya zaidi ya milioni tatu mtawanasa wengi
 
Inawezekana waliuliza direct Ikulu kuhusu ada elekezi
na pengine wameona since watoto wa Ikulu wako hapo
mahitaji ya security yataongezeka hivyo waongeze pia ada...
Mkuu the Boss

Hili swala la ada elekezi ni kutokana na kufanya mambo bila mpangilio.

Kwamba, kumekuwa na utumbuaji wa majipu basi kila kitu kutumbua tu.
Ni suala la kutumia maarifa tu gharama zinajirekebisha zenyewe

Watu wengi wana afford hizo shule za mamilioni kwasababu kuna pesa iliyokuwa inazagaa.
'Busara' za kifedha zinasema, unapokuwa na pesa nyingi zisizokuwa katika mpangilio 'wa kiuchumi' lazima kuna inflation

Shule binafsi wanajua wapo wanao afford wakipandisha. Na wengi ndio wale wa makontena na madili mengine
Kama serikali ingefanikiwa kudhibiti hele za madili na rushwa, shule binafsi zingepanga bei kwa nguvu ya soko

Hivyo hoja si kukabiliana ana kwa ana na soko huria bali namna gani kutakuwa na udhibiti wa fedha haramu, chafu

Watabaki wenye uwezo na hao watakabiliana na soko la shule binafasi, na shule hizo zitaangalia mwenendo wa soko lao

Labda nikupe mfano tu

Dili kama za Escrow, kuna watu wameibuka na milioni 50 at least,wengi sana.
Bandari na TRA achilia makando kando mengine
Hawa wakiambiwa shule ada ni milioni 25 kwa term moja, wana afford maana wanachoangalia ni mchongo mwingine

Shule binafasi zinatumia mtiririko huo huo kupata kitu. Ukidhibiti mtiririko, unawalazimisha wamiliki warudi katika soko halisi

Hakuna sababu ya kuwawekea bei na kupambana nao, improve the system mambo yananyooka yenyewe
 
kwa kuwa umemsomesha hadi anaingia F4 lipia tu sehemu iliyobaki au rais kakata mirija???
 
Yani unatoa million 8 kwa ajili ya Kingereza? Maana sioni cha ziada zaidi ya Kingereza kwenye hiyo shule.
 
Kwanza wazazi/walezi tuliambiwa tusubiri tusilipe ada za shule za private mpaka tarehe 16 Dec 2015 serikali itakapotoa muongozo.Baadaye serikali ikatoa agizo kwa shule za private zisipandishe ada kabla ya kujadiliana na wazazi na wizara kuhusu mabadiliko hayo.FEZA SCHOOLS wamekiuka agizo hilo kwa kupandisha ada za sekondari bila kukaa na wazazi kutoka 7,250,000 hadi 8,300,000.Na mbaya zaidi 1st instalment wanataka 4,050,000 (ada huwa inalipwa kwa instalment 3). Sasa kama binti/kijana yuko form four utamuhamishaje? Shule nyingi hawapokei wanafunzi wa form four. Muheshimiwa Rais, hii sio FEZA international.; ni shule inayofuata silabasi ya Taifa. Je hawa waturuki wako juu ya sheria?
Shule yenyewe inaitwa FEZA, unategemea wataenenda tofauti na maana ya hilo jina?.
 
Watu mmeweza kulipa hayo mamilioni leo hii mnalia lia nini
Kwani mlilazimishwa kupeleka watoto wenu hapo?
Dr.Magufuli amekaba mianya ya kupata pesa,ndio maana wanakuja kulalamika hapa Jamii forum
 
Kwanza wazazi/walezi tuliambiwa tusubiri tusilipe ada za shule za private mpaka tarehe 16 Dec 2015 serikali itakapotoa muongozo.

Baadaye serikali ikatoa agizo kwa shule za private zisipandishe ada kabla ya kujadiliana na wazazi na wizara kuhusu mabadiliko hayo.

FEZA SCHOOLS wamekiuka agizo hilo kwa kupandisha ada za sekondari bila kukaa na wazazi kutoka 7,250,000 hadi 8,300,000.

Na mbaya zaidi 1st instalment wanataka 4,050,000 (ada huwa inalipwa kwa instalment 3).
Sasa kama binti/kijana yuko form four utamuhamishaje? Shule nyingi hawapokei wanafunzi wa form four.

Muheshimiwa Rais, hii sio FEZA international.; ni shule inayofuata silabasi ya Taifa. Je hawa waturuki wako juu ya sheria?
Kwa hiyo unataka ada ishuke toka milioni 7 hadi laki 3.3? bila shaka ww ni sehemu ya majipu yanayotumbuliwa TRA/bandarini/mfanyabiashara mkwepa kodi, sasa mnaisoma namba!
 
Back
Top Bottom