Agizo lingine la Serikali ya Magufuli lapuuzwa

Agizo lingine la Serikali ya Magufuli lapuuzwa

Nimeona nimuandikie email kamishina wa Elimu kuhusu jambo hili na bila shaka atalishughulikia soon! Kimsingi fedha wamekiuka agizo..!

Nasubiri kuona majibu yake bwana Bhalalusesa au hatua atakayo ichukua.

Thanks, hopefully watajibu kuelezea ingawa nina mashaka kama kuna kitu watafanya hivi punde. Kelele hii inaweza saidia kwa wanafunzi wa miaka ijayo
 
mkuu watanzania wengi hamnazo kabisa.

Ha ha ha uwa najiuliza maswali mengi sana kuhusu maisha na uhalisia, huyu anampeleka mtoto shule mil 8 usikute ndugu zake kibao hata ada ya kayumba hawana. Yupo mtu atakuja kusema hapa inamusu nini, ajabu ni hii pamoja na kusoma feza bado mtoto anapata elimu anakuwa si bora zaidi ya kujua kingereza and worse enough wengi tutakutana UDSM, UDOM, SAUT, MZUMBE mzee wa njia za kayumba unawafukuza vibaya.
 
Thanks, hopefully watajibu kuelezea ingawa nina mashaka kama kuna kitu watafanya hivi punde. Kelele hii inaweza saidia kwa wanafunzi wa miaka ijayo
Asipo jibu mpaka kesho ntamforwadia pia katibu mkuu wizara..! Mi natumaini watafanyia kazi ..kama wataacha jambo hili lipite hivi hivi basi watakuwa wana muangusha Magufuli na bahati mbaya ni majuzi walitoa tamko kuzuia kupandishwa ada mpaka watakapo toa maelekezo!

Na hili ndilo tamko..la serikali
Ufundi imepiga marufuku
shule binafsi kuongeza gharama
za uendeshaji wa shule,
zikiwemo ada kwa mwaka wa
masomo unaoanzia mwezi
Januari mwaka ujao mpaka
watakapopata maelekezo
kutoka kwa Kamishna wa Elimu
nchini.

Kwa shule ambazo tayari
zimetangaza kuongeza gharama
na ada kwa mwaka wa masomo
wa 2016 bila kibali cha
Kamishna wa Elimu, Wizara
haitambui ongezeko hilo kwa
kuwa ni batili na hivyo
zimefutwa,? lilisema tangazo la
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi ambalo gazeti hili
lilipata nakala yake jana.
Wizara hiyo imesisitiza kuwa
ada zote kwa shule zisizo za
serikali zitabaki kama
zilivyokuwa zimeidhinishwa na
Kamishna wa Elimu. Shule
zinazohusika na tangazo hilo la
Serikali ni shule binafsi za
awali, msingi na sekondari.
Waraka wa Elimu Namba Nne
wa Mwaka 2008, uliweka
viwango vya ada vinavyotozwa
katika shule za msingi na
sekondari za serikali na zile
zisizo za serikali. Ada
iliyowekwa kwa shule za kutwa
zisizo za serikali ni Sh 150,000
na shule za bweni Sh 380,000
kwa mwaka kwa kila
mwanafunzi.
Waraka huo pia ulielekeza
kwamba ongezeko lolote la
ada, lazima lipate kibali cha
Kamishna wa Elimu kabla ya
kuanza kutumika. Tangazo hilo
linaeleza kuwa pamoja na
katazo hilo la Serikali,
imegundulika kuna baadhi ya
shule zisizo za serikali,
zimekuwa zikiongeza ada kila
mwaka pasipo kupata kibali cha
Kamishna wa Elimu.
?Utamaduni huu wa kuongeza
ada kila ifikapo mwishoni mwa
mwaka umekuwa ukisababisha
usumbufu mkubwa kwa wazazi
na walezi na hata baadhi yao
kushindwa kuendelea
kusomesha vijana wao katika
baadhi ya shule,? lilisema
tangazo hilo.
Kwa msimamo huo, wizara hiyo
imezitaka shule zote za binafsi,
kuwasilisha taarifa kwa Msajili
wa Shule aliyepo Idara ya
Ithibati ya Shule, kueleza kiasi
cha ada na gharama
kinachotozwa kwa sasa kabla ya
mwaka wa masomo 2016.
Shule hizo pia zinatakiwa
kuelezea kwa mara ya mwisho
tarehe ambayo shule husika,
ilipata kibali kutoka kwa
Kamishna wa Elimu kutoza
kiwango hicho cha ada. Taarifa
hizo zinatakiwa kufika ndani ya
wiki mbili kuanzia jana.
?Wathibiti ubora wa shule
waliopo sehemu mbalimbali
nchini wanaagizwa kulifuatilia
suala hili kwa karibu ili kila
shule itekeleze agizo hili na
kutoa taarifa zilizoelekezwa
katika tangazo hili. Hatua za
kinidhamu zitachukuliwa kwa
wamiliki ambao hawatatekeleza
maagizo haya,? ilisema taarifa
hiyo.
Pamoja na kukataza shule
kutopandisha ada, Wizara hiyo
imefafanua kuwa kwa sasa iko
katika hatua za mwisho za
utafiti na kuandaa mfumo wa
kielektroniki wa kutambua
gharama za kumsomesha
mwanafunzi katika elimu
msingi, ambayo ni elimu ya
awali, msingi na sekondari.
Kutokana na hatua hiyo, Wizara
ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
imewaomba wadau mbalimbali,
watoe ushirikiano kwa timu za
wataalamu wanaofanya kazi hii
ili kusaidia katika kuukamilisha
mfumo na hatimaye kuwa na
ada elekezi katika maeneo
mbalimbali.
Tamko hilo la wizara limetolewa
wakati tayari shule nyingi za
binafsi, zimeshatangaza
kupandisha ada kwa mwaka
ujao wa masomo kwa kisingizio
cha kupanda kwa gharama za
uendeshaji wa shule.
Ada kwa shule nyingi zisizo za
Serikali zinatofautiana na ziko
kati ya Sh 800,000 hadi Sh
5,000,000. Ada hizo ni nje ya
michango ya majengo,
mitihani, kitambulisho na
matibabu, jambo ambalo
limesababisha wazazi wenye
uwezo wa kifedha ndio ambao
wamekuwa wanasomesha
watoto wao kwenye shule hizo.
 
Hili jambo ni nyeti sana ingawa wachangiaji wamelichukulia personal na kwa sura ya kiwivu wivu ya Watanzania.

Kama serikali haiwezi kuratibu karo za shule binafsi basi wafute tangazo lao ili tuendelee na mipango ya kulipa ada.

Pole Kaunga ila naamini serikali itatoa kauli

Afadhali umeona hilo. Hii Nchi ina Watu wenye wivu wa kijinga jinga, akisikia Mtoto analipiwa ada milioni kadhaa anafikiri
Mzazi ana pesa za kuchezea tu.
 
Kwanza wazazi/walezi tuliambiwa tusubiri tusilipe ada za shule za private mpaka tarehe 16 Dec 2015 serikali itakapotoa muongozo.

Baadaye serikali ikatoa agizo kwa shule za private zisipandishe ada kabla ya kujadiliana na wazazi na wizara kuhusu mabadiliko hayo.

FEZA SCHOOLS wamekiuka agizo hilo kwa kupandisha ada za sekondari bila kukaa na wazazi kutoka 7,250,000 hadi 8,300,000.

Na mbaya zaidi 1st instalment wanataka 4,050,000 (ada huwa inalipwa kwa instalment 3).
Sasa kama binti/kijana yuko form four utamuhamishaje? Shule nyingi hawapokei wanafunzi wa form four.

Muheshimiwa Rais, hii sio FEZA international.; ni shule inayofuata silabasi ya Taifa. Je hawa waturuki wako juu ya sheria?
Achana na feza mpeleke mtoto wa mwenge primary sao hawalipi ada
 
Kwani lazma asome fedha ..hili ni soko huria ..uwezi lipa we hama tu..tusimpe raisi mizigo icyokuwa na maana
 
Bado utakuta huyu aliyepita shule kama hii akifika chuo anapata mkopo na yule mwingine anayetoka zile shule zetu anabaki akisaga sole ya viatu kwenda board ya mikopo kuhangaikia hatima ya mkopo wake na mwisho ataishia kupokea mabomu ya machozi, maji ya washawasha na virungu kuondolewa katika ofisi za board.

Nimekubali, ndiyo maana wapo watu wakisikia mtu anapingana na CCM wanakuja juu sana. Hivi hii ndiyo nchi aliyoiacha Mwl. Nyerere kweli???, nchi ambayo kuna mtoto analipiwa 8 milioni na mwingine ada ya shule ya Kata kuipata atalazimika kuuza majogoo kadhaa!!!.

Mwenye nacho anaongezewa asiyekuwa nacho hata kile kidogo ananyanganywa
 
Hili jambo ni nyeti sana ingawa wachangiaji wamelichukulia personal na kwa sura ya kiwivu wivu ya Watanzania.

Kama serikali haiwezi kuratibu karo za shule binafsi basi wafute tangazo lao ili tuendelee na mipango ya kulipa ada.

Pole Kaunga ila naamini serikali itatoa kauli

Exactly my point Dark City, kwanini wanatoa tamko wasiloweza simamia?

Asante, JF imebeba watu wa aina zote.
 
Last edited by a moderator:
Km kuna mtumishi wa umma ana mtoto hapo FEZA, naamrisha TAKUKURU washighulike nao tuone uhalali.Au wanasubiri hadi Majaliwa atie timu.
 
Bado utakuta huyu aliyepita shule kama hii akifika chuo anapata mkopo na yule mwingine anayetoka zile shule zetu anabaki akisaga sole ya viatu kwenda board ya mikopo kuhangaikia hatima ya mkopo wake na mwisho ataishia kupokea mabomu ya machozi, maji ya washawasha na virungu kuondolewa katika ofisi za board.

Nimekubali, ndiyo maana wapo watu wakisikia mtu anapingana na CCM wanakuja juu sana. Hivi hii ndiyo nchi aliyoiacha Mwl. Nyerere kweli???, nchi ambayo kuna mtoto analipiwa 8 milioni na mwingine ada ya shule ya Kata kuipata atalazimika kuuza majogoo kadhaa!!!.

Mkuu hadi nimedondosha chozi
 
Kwanza wazazi/walezi tuliambiwa tusubiri tusilipe ada za shule za private mpaka tarehe 16 Dec 2015 serikali itakapotoa muongozo.

Baadaye serikali ikatoa agizo kwa shule za private zisipandishe ada kabla ya kujadiliana na wazazi na wizara kuhusu mabadiliko hayo.

FEZA SCHOOLS wamekiuka agizo hilo kwa kupandisha ada za sekondari bila kukaa na wazazi kutoka 7,250,000 hadi 8,300,000.

Na mbaya zaidi 1st instalment wanataka 4,050,000 (ada huwa inalipwa kwa instalment 3).
Sasa kama binti/kijana yuko form four utamuhamishaje? Shule nyingi hawapokei wanafunzi wa form four.

Muheshimiwa Rais, hii sio FEZA international.; ni shule inayofuata silabasi ya Taifa. Je hawa waturuki wako juu ya sheria?
Kwani mlilazimishwa kupeleka wanafunzi hapo? Shule ni private na gharama zake pia ni private. Kama mnataka shule za bure ziko za umma
 
Mil.8 Ni kama dola 4000 za marekani,hiyo Ni kama Ada ya Chuo kikuu marekani.
waturuki waligundua Tanzania Ni nchi ya mafisadi ela watapata kirahisi wakitumia maarifa na kweli wametumia maarifa wanavuna ela kwa wingi.
 
Kwanza wazazi/walezi tuliambiwa tusubiri tusilipe ada za shule za private mpaka tarehe 16 Dec 2015 serikali itakapotoa muongozo.

Baadaye serikali ikatoa agizo kwa shule za private zisipandishe ada kabla ya kujadiliana na wazazi na wizara kuhusu mabadiliko hayo.

FEZA SCHOOLS wamekiuka agizo hilo kwa kupandisha ada za sekondari bila kukaa na wazazi kutoka 7,250,000 hadi 8,300,000.

Na mbaya zaidi 1st instalment wanataka 4,050,000 (ada huwa inalipwa kwa instalment 3).
Sasa kama binti/kijana yuko form four utamuhamishaje? Shule nyingi hawapokei wanafunzi wa form four.

Muheshimiwa Rais, hii sio FEZA international.; ni shule inayofuata silabasi ya Taifa. Je hawa waturuki wako juu ya sheria?
Mkuu kumbe ulikuwa unalipa 7m/=? Hiyo ni kubwa mno, anzisheni mchakato wa kuisusia hiyo shule.
 
Kwanza wazazi/walezi tuliambiwa tusubiri tusilipe ada za shule za private mpaka tarehe 16 Dec 2015 serikali itakapotoa muongozo.

Baadaye serikali ikatoa agizo kwa shule za private zisipandishe ada kabla ya kujadiliana na wazazi na wizara kuhusu mabadiliko hayo.

FEZA SCHOOLS wamekiuka agizo hilo kwa kupandisha ada za sekondari bila kukaa na wazazi kutoka 7,250,000 hadi 8,300,000.

Na mbaya zaidi 1st instalment wanataka 4,050,000 (ada huwa inalipwa kwa instalment 3).
Sasa kama binti/kijana yuko form four utamuhamishaje? Shule nyingi hawapokei wanafunzi wa form four.

Muheshimiwa Rais, hii sio FEZA international.; ni shule inayofuata silabasi ya Taifa. Je hawa waturuki wako juu ya sheria?
Sina kumbukumbu kama hili ni agizo la magufuli. vinginevyo najua ni maelekezo ya wizara husika katika kutumbua majpu yanayo wahusu
 
Yan hiyo hela unaweza kusomesha watu wawili masters mzumbe university, hela yetu haiwezi kuwa haina thamani kiasi hicho aisee, duhh!
 
Nina uhakika aliyeanzisha thread hii hajui maana ya ada. Zipo huduma mtoto anapata shuleni ambazo zinaongezeka kulingana na bei ya bidhaa sokoni kama chakula na malazi Magufuli hakuongelea hizo aliongelea ada kwa kimombo tunaita tuition fees soma vizur karatasi uliyopewa utaelewa. Mi nipo shule ada ni laki saba na nusu lakin mwanafunzi analipa milion sita na laki nane. Hembu jiulize kwanini New Africa Hotel bia ni 4000 wakati Yenu bar ni 2500???
 
Kwani mlilazimishwa kupeleka wanafunzi hapo? Shule ni private na gharama zake pia ni private. Kama mnataka shule za bure ziko za umma
Hii sio point..swala ni kwamba Feza wamekiuka agizo la serikali kutopandisha ada...!
 
Kikwete watoto wake wamesoma hapo hajalalamika unakuja kulalamika wewe kwani umelazimishwa kupeleka Mtoto wako hapo?
 
Back
Top Bottom