Agizo lingine la Serikali ya Magufuli lapuuzwa

Kaunga

JF-Expert Member
Nov 28, 2010
12,529
13,488
Kwanza wazazi/walezi tuliambiwa tusubiri tusilipe ada za shule za private mpaka tarehe 16 Dec 2015 serikali itakapotoa muongozo.

Baadaye serikali ikatoa agizo kwa shule za private zisipandishe ada kabla ya kujadiliana na wazazi na wizara kuhusu mabadiliko hayo.

FEZA SCHOOLS wamekiuka agizo hilo kwa kupandisha ada za sekondari bila kukaa na wazazi kutoka 7,250,000 hadi 8,300,000.

Na mbaya zaidi 1st instalment wanataka 4,050,000 (ada huwa inalipwa kwa instalment 3).
Sasa kama binti/kijana yuko form four utamuhamishaje? Shule nyingi hawapokei wanafunzi wa form four.

Muheshimiwa Rais, hii sio FEZA international.; ni shule inayofuata silabasi ya Taifa. Je hawa waturuki wako juu ya sheria?
 
Waziri wa Elimu/ Naibu wake Ebu Watoke Waziwazi Watujuze, Si Tuliambiwa Serikali Itatoa Ada Elekezi, lakini Ni kweli Wamefail

Mapema. Wizara ya Elimu na Mafunzo Ebu Toeni Tamko, Ili Mtuweke Huru.
 
Inashangaza kumpeleka mtoto shule ya mil 7 halafu unailalamikia serikali....

Karibuni st katumba...michango na ada hata laki 3 haifiki
 
Ha ha ha uwa najiuliza maswali mengi sana kuhusu maisha na uhalisia, huyu anampeleka mtoto shule mil 8 usikute ndugu zake kibao hata ada ya kayumba hawana. Yupo mtu atakuja kusema hapa inamusu nini, ajabu ni hii pamoja na kusoma feza bado mtoto anapata elimu anakuwa si bora zaidi ya kujua kingereza and worse enough wengi tutakutana UDSM, UDOM, SAUT, MZUMBE mzee wa njia za kayumba unawafukuza vibaya.
 
Wacha kulalamika wewe. Kama kwa miaka mitatu yote umeweza kusomesha mtoto kwa mil 7 leo mil 8 itakushinda? Kalipe bana mtoto akasome.

Mkuu, mwaka huu tunapata shida kwa sababu mianya yote imezibwa. Tulitegemea pesa ya sherehe ya UHURU tuzipige kiasi mgao tupate ada, mwishowe sherehe ikayeyuka, Safari za nje twende tupate per diem nazo zikayeyuka, Pale bandarini tupige uingizaji mizigo nayo ikayeyuka, Tuokote za wakwepa kodi ili waishi free nayo ikayeyuka, zile tulizificha katika ndoo chini ya uvungu wa kitanda nazo jamaa wakachukua, tulitegemea kodi ya nyumba zetu zile 73 daaaa jamaa akatushitukia!!!!!

DAAAAAAAA!!!!!!!!!!! hivi unafikiri mwaka huu watoto wataenda kweli kwa ADA YA mil.8.

Yaani tunatamani kuwarudisha shule za kata ingawa tunajisikia AIBU mtaani!!!!!!!

LAKINI TUNAANGALIA HUENDA NI UPEPO HUU UTAPITa, TUTARUDI KATIKA MISHEMISHE ZETU KAMA KAWA!!!!!!
 
Daaah!! Form one ada 8m, kwa dizaini hii sidhani kama watu wataacha kuiba.

Elimu imebinafsishwa kiasi kwamba sasa imefanywa ni zao la biashara jumla.
Serikali isipokuwa makini kuna muda utafika shule za private zitakuwa zinaipangia serikali mambo inayoyataka nabserikali itabidi iwasikilize kwa sababu haitakuwa na other alternative.

Kumbuka madereva wa mabasi ubungo Leo wakiamua wanaiamrisha serikali na serikali inafuatwa wanachosema coz reli walishauwa, makampuni ya umma ya usafirishaji walishayau so hawana alternative nyingine.
 
Inashangaza kumpeleka mtoto shule ya mil 7 halafu unailalamikia serikali....

Karibuni st katumba...michango na ada hata laki 3 haifiki

Mwaka jana walipandisha kutoka 6 to 7m, uliona tulikuja kulalamika? Wenye kuhamisha walihamisha.
Tumeilalamikia serikali kwasababu ilijitanabaisha kuwa ina uwezo wa kuratibu ada za private schools. So we are holding to their words. Nikiwa mdogo nilifundishwa kutoahidi kitu kama siwezi timiza.
 
Manina.. yani elimu ya sekondari ada kubwa kuliko ada ya kumsomesha daktari au Engineer chuo kikuu!!! Kweli i miss them days
 
  • Thanks
Reactions: nao
Huko mmetaka wenyewe. Huku kwa akina Kayumba hamkutaka kwakuwa mnadai elimu si bora. Sasa kitu kizuri na bora zaidi unataka kwa gharama dhaifu? Nadhani serikali ilijichanganya kuahidi kuwapa ada elekezi.
 
Watu mmeweza kulipa hayo mamilioni leo hii mnalia lia nini
Kwani mlilazimishwa kupeleka watoto wenu hapo?
 
Wacha kulalamika wewe. Kama kwa miaka mitatu yote umeweza kusomesha mtoto kwa mil 7 leo mil 8 itakushinda? Kalipe bana mtoto akasome.
Nitalipa lakini serikali ilikuwa inatafuta cheap popularity kwa kutangaza vitu ambavyo hawawezi simamia.
Hiyo ada kila mwaka inapanda, so kwa kuanzia ili amount to 5, ikaja 6, then 7, now 8.
Anayeanza form one analipa 9.05m
 
ujalazimishwa kumpeleka mwanao uko wewe mwisho wako wa kujikuna ni kisogo unataka ukutie utosi kweli.

mwamishie kata kama vipi wao huwa wanapokea
 
Bado utakuta huyu aliyepita shule kama hii akifika chuo anapata mkopo na yule mwingine anayetoka zile shule zetu anabaki akisaga sole ya viatu kwenda board ya mikopo kuhangaikia hatima ya mkopo wake na mwisho ataishia kupokea mabomu ya machozi, maji ya washawasha na virungu kuondolewa katika ofisi za board.

Nimekubali, ndiyo maana wapo watu wakisikia mtu anapingana na CCM wanakuja juu sana. Hivi hii ndiyo nchi aliyoiacha Mwl. Nyerere kweli???, nchi ambayo kuna mtoto analipiwa 8 milioni na mwingine ada ya shule ya Kata kuipata atalazimika kuuza majogoo kadhaa!!!.
 
Kwanza wazazi/walezi tuliambiwa tusubiri tusilipe ada za shule za private mpaka tarehe 16 Dec 2015 serikali itakapotoa muongozo.

Baadaye serikali ikatoa agizo kwa shule za private zisipandishe ada kabla ya kujadiliana na wazazi na wizara kuhusu mabadiliko hayo.

FEZA SCHOOLS wamekiuka agizo hilo kwa kupandisha ada za sekondari bila kukaa na wazazi kutoka 7,250,000 hadi 8,300,000.

Na mbaya zaidi 1st instalment wanataka 4,050,000 (ada huwa inalipwa kwa instalment 3).
Sasa kama binti/kijana yuko form four utamuhamishaje? Shule nyingi hawapokei wanafunzi wa form four.

Muheshimiwa Rais, hii sio FEZA international.; ni shule inayofuata silabasi ya Taifa. Je hawa waturuki wako juu ya sheria?

Magufuli aliagiza lini, wapi?!
Hicho kilikuwa na kiherehere na nidhamu yj woga ya katibu mkuu!
 
Back
Top Bottom