Agizo lingine la Serikali ya Magufuli lapuuzwa

Agizo lingine la Serikali ya Magufuli lapuuzwa

Nitalipa lakini serikali ilikuwa inatafuta cheap popularity kwa kutangaza vitu ambavyo hawawezi simamia.
Hiyo ada kila mwaka inapanda, so kwa kuanzia ili amount to 5, ikaja 6, then 7, now 8.
Anayeanza form one analipa 9.05m

Kalipe tu acha ubahili hata ikipanda hadi mil 20 inaonekana wewe unazo za kutosha.
 
Watoto wanaosoma fedha ni wale vilaza tu.Tunakutana nao vyuoni tunatoka na dist.wao wanayoka na third claa na hata gentleman degree wengi wao.

Unahangaika kumpeleka feza labda kama ana akili za kubust.
Kwa hiyo huu ndio msingi wa mada?
 
Nakumbuka enzi hizo kuna rafiki yangu Mhindi alinieleza kuwa sie Watanzania-wabantu tuna matatizo. Ukipata fedha familia inajua na ukikosa fedha familia inajua vile vile. Akazidi kunieleza kuwa ndo maana tunanyanyaswa na wake zetu na siku nyingine kudharaulika na watoto. Akasema kwao wahindi akipata fedha familia haiwezi kujua maana kwa kawaida wao huwa na life style ambayo ni standard. Kama hana fedha familia inadunda na akipata fedha inaiweka benki si siku hiyo kununua kilo 10 za nyama ili kila mtu mtaani aone kuwa naye kapata fedha. Hili la Kaunga kulalama ni mfano hai maana kutegemea fedha za madili ili ukasomeshe watoto au kutunza familia huu ndiyo msala. Mtoto au familia inatunzwa na kipato halali
Si kila mtu anaye somesha watoto fedha ni mwizi...
Mada imegeuka mashambulizi binafsi
 
Si kila mtu anaye somesha watoto fedha ni mwizi...
Mada imegeuka mashambulizi binafsi
Chonde chonde sina silka ya kutukana au kusema kitu nisichokifahamu. Ukirudia andiko langu sikusema kuwa anayesomesha mtoto FEZA ni mwizi. Nilisema madili na madili yanaweza kuwa ni lunch allowance au zawadi, mishen town etc. Kwanza kabisa mtoto kusoma Feza lazima awe na akili zinachaji. Akiwa kiazi hata uwe na matrillion ya fedha watamfukuza tu. Nadhani ni mmoja aliyeweza kukaa FEZA Girls kwa cheo cha Baba yake ingawa kichwani zilikuwa ndembe ndembe. Mie nilitaka kujenga hoja ya kukumbusha kuwa tuwe waangalifu na vitu vya kupita, maana unaweza kujikuta katika wakati mgumu pindi maziwa yakikata.
 
Daaah!! Form one ada 8m, kwa dizaini hii sidhani kama watu wataacha kuiba.

Elimu imebinafsishwa kiasi kwamba sasa imefanywa ni zao la biashara jumla.
Serikali isipokuwa makini kuna muda utafika shule za private zitakuwa zinaipangia serikali mambo inayoyataka nabserikali itabidi iwasikilize kwa sababu haitakuwa na other alternative.

Kumbuka madereva wa mabasi ubungo Leo wakiamua wanaiamrisha serikali na serikali inafuatwa wanachosema coz reli walishauwa, makampuni ya umma ya usafirishaji walishayau so hawana alternative nyingine.

Daah! Umenikumbusha machungu. Yule katibu wa umoja wa madereva nchini kapoteza maisha. Haki kupatikana kwake ngumu sana.
 
Serikali ya JPM imeufyata baada ya wamiliki wa shule binafsi kuijia juu.
 
Mwaka jana walipandisha kutoka 6 to 7m, uliona tulikuja kulalamika? Wenye kuhamisha walihamisha.
Tumeilalamikia serikali kwasababu ilijitanabaisha kuwa ina uwezo wa kuratibu ada za private schools. So we are holding to their words. Nikiwa mdogo nilifundishwa kutoahidi kitu kama siwezi timiza.

HAMKUJA si kwa sababu serkali imesema LA mwaka jana mianya ilikuwa haijazibwa mbona ongezeko kwa mwaka ni lile lile 1 Mil
 
HAMKUJA si kwa sababu serkali imesema LA mwaka jana mianya ilikuwa haijazibwa mbona ongezeko kwa mwaka ni lile lile 1 Mil

Kama issue ni mianya hata hiyo 7m tunayoikamatia serikali tusingeweza lipa.
 
Wezi wa mitihani number moja Tanzania ni hawa feza ila zungukeni safari ni moja cuhas muhas udom udsm nk
 
Hii sio point..swala ni kwamba Feza wamekiuka agizo la serikali kutopandisha ada...!
Ndiyo maana nasema maagizo ni lazima yawe na logic ya kiutekelezaji. Tuko kwenye mfumo wa biashara huria inabidi tuheshimu kanuni zake. Udhibiti katika mfumo huo una mipaka yake.
 
Sijaona jambo hili kwenye tamko lile ....

Kumradhi...nilidahani hawa (FEZA) nao wamo humu
WIZARA ya Elimu, Sayansi na Ufundi imetoa waraka wa elimu kuhusu elimumsingi bila malipo na kutoa orodha ya shule za msingi 11 za Serikali ambazo hazihusiki na utoaji wa elimu bure uliotangazwa na Rais John Magufuli. Elimumsingi inajumuisha elimu ya awali, ya msingi na sekondari ambayo itaanza Januari mwakani.
Katika Waraka Elimu Namba 6 wa Mwaka 2015 kuhusu utekelezaji wa elimu bure kwa shule za msingi na sekondari, wizara hiyo imetaja shule hizo kuwa ni Shule ya Msingi Olympio (Dar es Salaam); Shule ya Msingi Diamond (Dar es Salaam); Shule ya Msingi Oysterbay (Dar es Salaam); Shule ya Msingi Iringa (Iringa) na Shule ya Msingi Mkapa (Mbeya).
Nyingine ni Shule ya Msingi Angaza (Mbeya); Shule ya Msingi Nuru (Mbeya); Shule ya Msingi Lupilisi (Ruvuma); Shule ya Msingi Tanga (Tanga); Shule ya Msingi Arusha (Arusha) na Shule ya Msingi Kisimani iliyoko mkoani Arusha.
Wizara hiyo pia imesema waraka huo hauzihusu shule zinazomilikiwa na mashirika ya umma ama taasisi za umma ambazo zinaendeshwa kwa taratibu sawa na shule za binafsi. Katika waraka huo, wizara hiyo imetoa majukumu yanayotakiwa kufanywa na Wizara hiyo, Tamisemi, wakurugenzi wa manispaa na halmashauri ya wilaya, wakuu wa shule, bodi za shule, wazazi na wananchi.............

Shule 11 kutohusika elimu bure
 
Kwanza wazazi/walezi tuliambiwa tusubiri tusilipe ada za shule za private mpaka tarehe 16 Dec 2015 serikali itakapotoa muongozo.

Baadaye serikali ikatoa agizo kwa shule za private zisipandishe ada kabla ya kujadiliana na wazazi na wizara kuhusu mabadiliko hayo.

FEZA SCHOOLS wamekiuka agizo hilo kwa kupandisha ada za sekondari bila kukaa na wazazi kutoka 7,250,000 hadi 8,300,000.

Na mbaya zaidi 1st instalment wanataka 4,050,000 (ada huwa inalipwa kwa instalment 3).
Sasa kama binti/kijana yuko form four utamuhamishaje? Shule nyingi hawapokei wanafunzi wa form four.

Muheshimiwa Rais, hii sio FEZA international.; ni shule inayofuata silabasi ya Taifa. Je hawa waturuki wako juu ya sheria?
Aaaaah naona posho zimefutwa mnaanza kulalama
 
Ndiyo maana nasema maagizo ni lazima yawe na logic ya kiutekelezaji. Tuko kwenye mfumo wa biashara huria inabidi tuheshimu kanuni zake. Udhibiti katika mfumo huo una mipaka yake.
Hawa unao jaribu kuwatetea wameshindwa kuheshima sheria inayo wataka kuwa na mashauriano na wazazi kabla ya kuongeza ada..
 
kila shule ina ubora wake na uwezo wake wa kufundisha, ndo maana wazazi wanaangalia ni wapi panawafaa zaidi kuwapeleka watoto wao, na pia wanajua uwezo walionao ndo maana wana wapeleka huko bila kujali kua kuna shule za bei nafuu( kabla hazijawa bure) za serikali. Sana kama wanaona haziwafai kwa hilo ongezeko kiduchu basi wawatoe na wale watakaoweza kulipa basi na waendelee. Serikali haiwezi ingilia kila jambo la binafsi hata kama linaingilia kwa namna moja ama nyingine. Kwanza cheki mazingira tu ya hiyo shule yanavyo ring bells ndo utajua gharama yake, uwezo wa walimu na halli ya ufundishaji pia.

Nakubaliana nawe 100%, mwaka jana nilimtembelea rafiki yangu ambaye anakaa Uingereza. Kwa muda mrefu alikuwa amewaacha watoto wake wakisoma katika shule za kawaida huku Tanzania.Akanieleza imebidi awahamishie watoto wake Tusiime kabla ya kuwahamishia Uingereza. Nikamwuliza ni kwa nini anafanya hivyo, akasema kuwa iwapo watakwenda huko na kiwango cha chini wataingia katika shule za viwango vya chini na hata University watakwenda katika shule za namna hiyo hiyo. Matokeo yake hawawezi kupata ajira nzuri na hata maarifa ya kutosha kufanya kazi binafsi. Haitatokea hata wakati mmoja watu wote wakawa na kipato kinachofanana. Cha msingi Serikali iboreshe shule zake na hizo shule za private zitafunga zenyewe au zitashusha bei kwani hakuna atakayezikimbilia. " Chema chajiuza kibaya chajitembeza"

Nahisi munasikitisha. Mmoja, Fredilluu hajui nini maana ya shule ya sekondari maana sasa anasifia hata ukuta na kengere ya shule. Baadaye atasema kuna maua. OK! Huyu mwingine, Laurano, yeye anamkumbuka rafiki wa Uingereza, eti ili watoto wasome huko ilibidi wingie Tusiime! Yote hayo ndo udhaifu wa kutojua tu. Kawaida, elimu inatakiwa iwe ya gharama tofauti ktk ngazi za colleges. Nchi zote utaonekana hujijui, kama utakuwa unatafuta shule za gharama kubwa ktk primary au sekondari.

Sababu moja muhimu ni kwamba elimu za chini zote, ni jukumu la serikali na wamiliki binafsi wanafanya kwa kuruhiwa na serikali, ndiyo maana wanaongozwa hata kwa mitaala. Sasa nikisoma maandishi yenu mukisifia eti kama unaweza fanya hivi au vile, that is nonsense. Upende usipende lazima mwanao asomeshwe mambo fulani. Elimu inajenga Taifa na siyo familia yako, ndo maana wizara inaongoza.

Laurano, muulize rafiki yako. Tusiime alifuata lugha, na hapo naunga mkono maana Uingereza ni kiingereza. Muulize huko Uingereza kama kuna upuuzi huu wa FEZA. Muulize ada za shule inayoitwa Gordonstoun, shule ambayo sehemu kubwa ya familia ya malkia wamesoma hapo. Je, kuna upuuzi wa ada za milion 7?

Naamini ili ujue jinsi mwanao atakavyosoma, lazima nawe uwe umesoma. Kama hukusoma utapeleka kokote hata huko kwa milioni 20.
 
Back
Top Bottom