Wapi yesu kasema KUWENI WAKRISTO?
Au Wapi Bibilia imesema UKRISTO ni DINI?
Kutoa mawazo kichwani bila reference za mashiko ni safi sana km unaongea na Familia yako lkn hapa jukwaani hapafai.
Hapa bila Source unatafuta kuadhirika tu mkuu.
Ukristo umeletwa na MGIRIKI Aitwae PAULO. na Huko Bongo aliyetuletea UKRISTO sisi Ni MZUNGU aliyekuja na Meli ya Kwanza ya KUBEBA watumwa Iitwayo JESUS SHIP Mwaka 1534.
Mkuu Ukinijibu swali hili na mimi nitakujibu.
Wapi Mungu kasema Mbinguni kuna kufanya ngono na Mabikra?
Wapi Mungu kasema mbinguni kuna mito ya Pombe na Ulevi?
Mswaada wa kuanzisha MUNGU wa Afrika nakuandika Kitabu cha dini ya Afrika chini ya Uafrika.
Ndugu zangu Waafrika, kwa wiki mbili hivi nilikuwa nimezama kwenye tafakuri pana sana juu ya imani ya mtu mweusi dhidi ya dini, Mungu wake, Nimebaini waafrika tunaamini kisicho chetu, tumemetelekeza kuendeleza imani yetu na Mungu wetu na badala yake tunamwabudu Mungu wa masimulizi ya Ukalidayo na kuamini dini za kuletwa kwa majahazi,
Hivyo kwa heshima ya Dini ya kale ya Kiafrika na Mungu wetu, nimeaamua kuanzisha Mchakato wa uandikaji wa Biblia ya Dini ya Kiafrika na Uundwaji na usimikwaji wa MUNGU wa Afrika.
Kitabu hiki kitaundwa kwa vitabu VITANO, ambavyo itakuwa ni mkusanyo wa vitabu vifuatavyo;
Afrika ya Mashariki, Afrika Magharibi, Afrika Kaskazini, Afrika ya Kati, Afrika Kusini. Mitume tutakaowafuata maono yao ni pamoja na Chifu Mkwawa, Kitabu A.Msh Tagk, Chifu Monziyno, Kitabu A.Magh Nigr. Nk.
Pia wataalamu na waamuzi mbali watakuwemo kama vile Ng'wanamalundi, Umuvuginza, nk.
Ninakaribisha maoni ya Uandikaji wa biblia hii. Kitaitwa kitabu cha uafrika, Tayari mchakato unaendelea, nakaribisha maoni ya wadau.
attack hoja zake usijikite zaidi kwenye personality yake atakudharau.Yericko Njaa inakupeleka pabaya kijana.
Umefilisika mawazo ya miundo mbinu mpk unafikiria kuwaiga kina babu wa loliondo.
Wenzako waliwahi, we unakuja kushtuka 2015! ?
Mi nakushauri uanze na Kioski cha sigara kwanza halafu tafuta na Fundi viatu kaa nae hapo. Hutokosa hela ya kula.
Mtaji ekfu 50 inatosha. Na km huna njoo nikusaidie usije athirika kwenye ubongo kabla ya saa.
Aisee..! kwa hiyo Mungu wa Afrika ataitwa nani??
KUANZISHA???!!! MUNGU!!???......nadhani ni vema kutafakari upya.
Dini ya babu yako ilikuwa ni Kutambika uchi na Kuua Kila mwenye macho mekundu!
Dini ya babu yako ilikuwa ikitokea Mafuriko au mitetemeko ya Ardhi wanamtoa mtoto kafara kwa kumchinja.! Au Kumzika akiwa hai.
Dini ya babu yako Mwanamke ilikuwa marufuku kula vyakula vinono manake mwanamke alikuwa ni chombo cha starehe tu.
Sasa km unaitaka dini ya namna hio anza kupiga marufuku nyumbani kwenu dada zako na wazee wako wa kike wasile chochote kuanzia mayai, nyama, pilau n.k.
Washindie mihogo mikavu tu na maji.
Ukifanikiwa hilo anza mazoezi ya kutembea Uchi.
Halafu utatupa taarifa unaendelea vipi.
Hizo dini za wazungu ndo zimewafundisha hivyo?
Je, zisingekuja hizo dini ungekuwa unaabudu wapi? Akili ya kukosoa ungeitoa wapi?
Ndio maana Binaadamu kila akiishi anajifunza mengi na Kuregebisha maisha yake.
Babu yako na wangu walikuwa wanajisaidia Maporini na kuchambia majani. Leo tuna vyoo vya kisasa vya kutumia maji.
Sasa wewe unataka kunirudisha porini! Hio ndio busara?