Afrika ilishaachwa na Mungu tangu kitambo

Afrika ilishaachwa na Mungu tangu kitambo

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2010
Posts
17,026
Reaction score
20,511
Muigizaji wa filamu wa Marekani,Bruce Willis, katika filamu yakekuhusu Afrika, hasa Nigeria ilikofanyiwa uigizaji, ‘Tears of theSun', kuna wakati alikuwa akiagwana mchungaji mmoja mzungualiyekataa kuondoka eneo lamapigano, akiambiwa, "God be Withyou" (Bwana awe nanyi); Willisalisita kidogo na baadaye kusema,"God left Africa long timeago." (Mungu Alisha iacha Afrikakitambo." Na msaidizi wake, Red,aliunga mkono kwa kusema"Yeah" (ni kweli)."Tears of the sun" ni kama ilitabirikinachotokea sasa kati ya wananchina Boko Haram.

Ingawa mrengo namuktadha ni tofauti lakini ukweli nikwamba kama kuna Mungu basiBoko Haram wanathibitisha kuwaAlisha iacha kitambo. Afrika ni nchiambapo viongozi, na siyo BokoHaram, Lord Resistance Army,Seleka, au Antibalaka, au Al-Shabaabpeke yako, wanaonyesha kuwaMungu amewakasirikia. Hayupo nao.Na kuwa kuongezeka au makundiyanayoakisi kutokuwapo kwa (neemaza) Mungu inatokana na uongoziambao haumjali Muumba.Huko Nigeria, wakati wananchiwanaendelea kuuwawa kwa idadikubwa na Boko Haram wakindeleakuonyesha kutishika, serikaliinaendelea na uchaguzi kama vilehakuna kitu kinachotokea, nawanasema huko wanakouawauchaguzi hautafanyika. Wanauawakunyimwa haki yao ya kuishi, nawanaambiwa kura nayo siyo hakiyao.

Viongozi wamepandishamashetani ya kuwa viongozi, nawanaona kuuawa kwa wananchiwengine sio kigezo cha kutoshelezakuahirisha uchaguzi.Kwa tatizo hilo ni la watu wa kasikazini, na sie wengine hatumo.Afrika ilimwasi Mungu, kwani tabiaya kutojali haki za wananchi wenzaoni ishara mojawapo. Familia zaviongozi, viongozi wenyewe,maswahiba wao, hawaoni hayakuwalinda waovu wanaoiba mali zaumma. Matajri wengi wa Afrika nahasa viongozi, wanatokana na kuibafedha za umma ama kudhulumu hakiza raia.

Grace Mugabe anadaiwakuua wananchi wenzake kwakuwaachia wanyama maeneoambayo wananchi walikuwawakiishi, ili waondoke na yeye awezekuanzisha bustani yake ya wanyamakwa ajili ya utalii. Kuna Munguhapo? Na sidhani kama GraceMugabe anawaona wananchi haowanaofukuzwa kikatili kwenye ardhiyao kama nao ni watoto wa Mungu.Afrika imejawa na viongozi wengiambao kila uchao wanawaza namnagani watatumia fursa zao za uongozikujimilikisha utajiri.

Kwa sasa hatuioni Afrika ambayo viongozi ni wale wa miaka kabla ya kipindi hikicha mageuzi ya kiuchumi, ambapowakati huo (viongozi) walikuwawakipanga namna ya kuwakomboaWaafrika wenzao kiuchumi.Nyakati zile za Jaramogi OdingaOginga, Nyerere, Kwameh Nkrumah,Murtala Mohamed na ThomasSankara.

Huu ni wa wakati ambapoviongozi wengi huwa wanapanganamna gani watashirikiana wao kwawao kuitafuna nchi; wanapangakushirikiana na mafisadi wenzao wandani (baadhi ya wafanyabiashara),kuihujumu nchi; wakishirikiana namashirika ya nje na nchi za njekutafuta utajiri wetu.Inanishangaza sana kuona viongoziwakienda kanisani au misikitini, hukujana yake tu wamekuwa wakifanyamikutano ya siri na wanaouza dawaza kulevya, wakijua kuwa taifa lilewalilioapa kulilinda dhidi ya uovundilo wanaloliangamiza kwa dawaza kulevya.

Kwa mfano, unakuwajewaziri unayeahidi ajira 100 halafujioni unakuwa na kikao na wauzaunga? Hizo ajira 100 zitafanywa nanani? Hao vijana hawana kazi, badounataka kuwadhulumu kidogowanachokipata kwa kuwauzia dawaza kulevya wasijimudu kabisa.Mungu anaweza kuwa yupo hapo?Kiongozi anaapa kuwa atalinda nchina watu wake, na vyote vilivyomo.

Lakini mara baada ya igizo la kiapo,kiongozi anataka kujua wapi atapatasoko la siri la dhahabu, meno yatembo, vipusa, na kadhalika, iliaweze kujitajirisha na kuwalindawalio nje au ndani ya serikali yake.Afrika ilishamuudhi Mungu na yeyeameshaitelekez, na Bruce Willishajakosea kabisa. Afrika hii ambayoina utajiri lakini haitaki kuwa tajiriisipokuwa inataka tu viongozi wakepekee wawe tajiri hawana sababu yakusema Mungu atatujalia! Munguhawezi kuijaalia nchi ambayo kilauchao viongozi wao wanafikirianamna gani wataifilisi nchi yao.

Mungu alishaliacha bara hili.

Chanzo: Nipashe
 
Well. Tuanze na tasnia ya filamu, inakuwaje hadi mzungu aje Afrika kuigiza maisha yetu? Wasanii wa afrika wanajua kuigiza mapenzi tu?? Blood diamong, last king of scotland etc. tasnia ya filamu ina mengi ya kufanya zaidi ya hapa.

Uongozi wa sasa umejawa na wizi na ufisadi na yote hii imechangiwa na ubinafsi wa hali ya juu.

Afrika kuna shida aisee.
 
Wazungu hao washenzi tu na wanafiki wa kisasa! Hao boko haram, Al shabab, Lra wanatoa silaha wapi kama sio kwao???? It is their wish hata tufe wote ili watubebee madini, gesi, twiga na pundamilia... Then wanakuja kuigiza upuuzi mnawashabikia(am referring to the source) no wonder wanamfanya shetani mweusi (arch angel) huku hao malaika wengine ni Wazungu!!!!ujinga ujinga tu.
 
Africa ni nchi iliyobarikiwa sana.Na shetani utafuta sehemu ilipo baraka na kuizimisha.Lakin Africa bado tunao watu wachache ambao wanendelea kumlilia Mungu ili aliponye bara hili na nguvu za yule mwovu shetan,na siku chache uovu huu utaisha.Africa hatuna barafu,tuna majira yanyoeleweka,unajua sasa ni asubuhi na sasa ni jioni,kwa wenzetu jua siku nyingine lina chwea usiku saa tano.Africa tuna mbuga za wanyama,hatuna barafu.Africa ndiko alijificha Yesu wakati wa Herode.Kwakweki Africa tumebarikiwa.Siku za mwisho tutaona mengi,vita kila sehemu,mauji ya Albino,Boko halamu nk.Lakina tunaelezwa kuwa tukiyaona haya tuchangamke mwisho wa miishyo yote umekaribia.
 
Biblia imetabiri kuwa Mungu ataikumbuka Africa katika siku za mwisho, Nikweli sisi ni bara lenye laana, maana tulitokana na mtoto wa Nuhu aliye laaniwa laana kali kwa kosa la kumdhalilisha baba yake, lakini Mungu ameahidi kutukumbuka siku za mwishoni. Isaya 19: 1-
 
umenikumbusha movie ya blood diamond kuna sehem leonardo di carpio alikuwa anaulizwa na yule demu mwandishi wa habari kuhusu wanayoyafanya (kubadilishana na waasi silaha kwa almas) kwamba haoni km hawampendezi mungu! di carpio akamjibu....." you talk about god, god has arleady left africa long time ago,
 
Mkuu Yericko mie ninachoamini si kuwa mwenyezi MUNGU ameamua atuache sie Waafrika tuteseke, bali sie binadamu wenyewe ndio tumeamua kumuasi Mwenyezi Mungu kwa tamaa zetu hadi kufikia kuuwa wenzetu tujipatie mali.
 
mungu yupi aliiwacha afrika ??? Mungu wa agano la kale au mungu wa agano jipya ??
 
Well. Tuanze na tasnia ya filamu, inakuwaje hadi mzungu aje Afrika kuigiza maisha yetu? Wasanii wa afrika wanajua kuigiza mapenzi tu?? Blood diamong, last king of scotland etc. tasnia ya filamu ina mengi ya kufanya zaidi ya hapa.

Uongozi wa sasa umejawa na wizi na ufisadi na yote hii imechangiwa na ubinafsi wa hali ya juu.

Afrika kuna shida aisee.

bajeti ya hizo filamu unaziweza au unasema tu? blood diamonds pekee inaweza kuwa ni bajeti ya tz ya mwaka huu
 
Mwandishi wa hiyo makala ni kiongozi wa vilaza...

Najuta kuifungua hii thread...
 
Hiyo sehemu naikumbuka sana.......na sio hiyo tu kuna movie nyingi sana wazungu wanaikandia Africa mfano sikumbuki vizuri ni series gani nilikuwa naangalia lkn kuna sehemu bibi mmoja alimnunulia mjuu wake gari kama zawadi ya birthday lkn mama mtoto akaja juu akisema zawadi ni kubwa sana maana binti bado mdogo, bibi Akasema it's just a car..........Mama Akasema unaona ni kitu kidogo wakati kuna watu huko Africa wanatembea bila viatu.
Mimi lawama zangu ni kwa viongozi wa Africa,nadhani shetani amewekeza kwao........sijaona kiongozi wa Africa mwenye kusema hii Nchi yangu,wananchi wangu ndio waajiri wangu napaswa kuwaheshimu na kusikiza kutoka kwao......sio Africa.......wakishachukua madaraka ni kama tumepeana Mkono wa kwaheri,wao na familia zao umaskini Basi tena wanasahau waliowaweka pale.
 
mungu yupi ?
Baba, Mwana, Roho mtakatifu Ama Allah
 
Wazungu hao washenzi tu na wanafiki wa kisasa! Hao boko haram, Al shabab, Lra wanatoa silaha wapi kama sio kwao???? It is their wish hata tufe wote ili watubebee madini, gesi, twiga na pundamilia... Then wanakuja kuigiza upuuzi mnawashabikia(am referring to the source) no wonder wanamfanya shetani mweusi (arch angel) huku hao malaika wengine ni Wazungu!!!!ujinga ujinga tu.[/QUOTE
Tutaishia kutukana na kulaumu wazungu tu... Kwani sisi kili zetu zipo mat.a.koni hadi yote haya wawe wanatufanyia na tunakubali kuuana kama wadudu?
 
Back
Top Bottom