Afrika ilishaachwa na Mungu tangu kitambo

Mswaada wa kuanzisha MUNGU wa Afrika nakuandika Biblia ya Afrika chini ya Uafrika.

Ndugu zangu Waafrika, kwa wiki mbili hivi nilikuwa nimezama kwenye tafakuri pana sana juu ya imani ya mtu mweusi dhidi ya dini, Mungu wake, Nimebaini waafrika tunaamini kisicho chetu, tumemetelekeza kuendeleza imani yetu na Mungu wetu na badala yake tunamwabudu Mungu wa masimulizi ya Ukalidayo na kuamini dini za kuletwa kwa majahazi,

Hivyo kwa heshima ya Dini ya kale ya Kiafrika na Mungu wetu, nimeaamua kuanzisha Mchakato wa uandikaji wa Biblia ya Dini ya Kiafrika na Uundwaji na usimikwaji wa MUNGU wa Afrika.

Bibilia hii itaundwa kwa vitabu vikuu VITANO, ambavyo itakuwa ni mkusanyo wa vitabu vifuatavyo;

Afrika ya Mashariki, Afrika Magharibi, Afrika Kaskazini, Afrika ya Kati, Afrika Kusini. Mitume tutakaowafuata maono yao ni pamoja na Chifu Mkwawa, Kitabu A.Msh Tagk, Chifu Monziyno, Kitabu A.Magh Nigr. Nk.

Pia wataalamu na waamuzi mbali watakuwemo kama vile Ng'wanamalundi, Umuvuginza, nk.

Ninakaribisha maoni ya Uandikaji wa biblia hii. Kitaitwa kitabu cha uafrika, Tayari mchakato unaendelea, nakaribisha maoni ya wadau
.

Mkiambiwa chama chenu ni cha kidini mnarefusha midomo kama yule ndege mla nyoka.
sasa bandiko ziiiiima ni biblia.by the way,kama mliweza kumchagua mwanadamu ndiye awe mungu wenu
then leo hamshindwi kumtengeneza mungu mpya!!!!
 
Unajua utahira unaanza taratibu bila mtu kujigundua....
 
Mswaada wa kuanzisha MUNGU wa Afrika nakuandika Biblia ya Afrika chini ya Uafrika.

Ndugu zangu Waafrika, kwa wiki mbili hivi nilikuwa nimezama kwenye tafakuri pana sana juu ya imani ya mtu mweusi dhidi ya dini, Mungu wake, Nimebaini waafrika tunaamini kisicho chetu, tumemetelekeza kuendeleza imani yetu na Mungu wetu na badala yake tunamwabudu Mungu wa masimulizi ya Ukalidayo na kuamini dini za kuletwa kwa majahazi,

Hivyo kwa heshima ya Dini ya kale ya Kiafrika na Mungu wetu, nimeaamua kuanzisha Mchakato wa uandikaji wa Biblia ya Dini ya Kiafrika na Uundwaji na usimikwaji wa MUNGU wa Afrika.

Bibilia hii itaundwa kwa vitabu vikuu VITANO, ambavyo itakuwa ni mkusanyo wa vitabu vifuatavyo;

Afrika ya Mashariki, Afrika Magharibi, Afrika Kaskazini, Afrika ya Kati, Afrika Kusini. Mitume tutakaowafuata maono yao ni pamoja na Chifu Mkwawa, Kitabu A.Msh Tagk, Chifu Monziyno, Kitabu A.Magh Nigr. Nk.

Pia wataalamu na waamuzi mbali watakuwemo kama vile Ng'wanamalundi, Umuvuginza, nk.

Ninakaribisha maoni ya Uandikaji wa biblia hii. Kitaitwa kitabu cha uafrika, Tayari mchakato unaendelea, nakaribisha maoni ya wadau
.

Andika neno Frederick Nitsche na ufuatilie aliishia wapi kadiri ya mtazamo kama wako.
 
Mimi kinachonikera kuona picha za shetani wote ni weusi na eti malaika wote ni weupe sijawahi ona mweusi hebu nisaidiwe kwa hilo kueleweshwa
 
Ngoja niwashauri Waafrica wenzangu. Kuna watu wanadhani Ukristo ni dini ya Wazungu hivyo Wafrica tuna dini yetu, si kweli. Ukristo ni dini ya dunia.

Kwanini nasema ni duni ya dunia?.
Ni dini ya dunia kwa sababu chanzo chake si mzungu, chanzo cha Ukristo ni Mashariki ya kati, dini ilianzia pale na baadae ikahubiriwa kwenda kwenye mataifa mbalimbali. Hivyo hata hao Wazungu wamepokea dini kama tulivyoipokea Waafrica, yaani kwa kuhubiriwa. Tofauti kati yetu na wao ni kwamba wao wameipokea mapema kabla yetu. Hivyo chanzo ni Mashariki ya kati, Mashariki ya kati si Wazungu.

Kwa Wakristo.
Ukristo maana yake ni Ufuasi wa mafundisho ya Yesu. Kuna watu wanajichanganya kwa kusema Yesu ni Mzungu. Mimi nasema Yesu ni neutral, Yesu hana Kabila, nasema hana Kabila kwa sababu yeye hana Baba, yeye ana mzazi mmoja tu aliemzaa katika hali ambayo mpaka leo wanasayansi hawawezi kuielezea, hivyo hana kabila. Yesu alikuwa wa kipekee, mpaka sasa bado kuna debate maana muonekano wake haukuwa wa kawaida.
 
Wapi yesu kasema KUWENI WAKRISTO?

Au Wapi Bibilia imesema UKRISTO ni DINI?
Kutoa mawazo kichwani bila reference za mashiko ni safi sana km unaongea na Familia yako lkn hapa jukwaani hapafai.

Hapa bila Source unatafuta kuadhirika tu mkuu.

Ukristo umeletwa na MGIRIKI Aitwae PAULO. na Huko Bongo aliyetuletea UKRISTO sisi Ni MZUNGU aliyekuja na Meli ya Kwanza ya KUBEBA watumwa Iitwayo JESUS SHIP Mwaka 1534.
 
Ni heri mimi na Wakristo wenzangu tuonekane machizi au Mazuzu kwa Kumshangilia Yesu Kristu Mungu Wetu na Mwokozi wetu kuliko Kuonekana mjanja kwa ku-support Imani Zisizokuwa na Kichwa wala miguu wala Kiwiliwili.

Hiyo ya kwenu mliyoletewa ina kichwa,miguu na kiwiliwili sio??😀😀😀 kweli wazungu wametubaka akili.
 
Ngoja niwashauri Waafrica wenzangu. Kuna watu wanadhani Ukristo ni dini ya Wazungu hivyo Wafrica tuna dini yetu, si kweli. Ukristo ni dini ya dunia.

Kwanini nasema ni duni ya dunia?.
Ni dini ya dunia kwa sababu chanzo chake si mzungu, chanzo cha Ukristo ni Mashariki ya kati, dini ilianzia pale na baadae ikahubiriwa kwenda kwenye mataifa mbalimbali. Hivyo hata hao Wazungu wamepokea dini kama tulivyoipokea Waafrica, yaani kwa kuhubiriwa. Tofauti kati yetu na wao ni kwamba wao wameipokea mapema kabla yetu. Hivyo chanzo ni Mashariki ya kati, Mashariki ya kati si Wazungu.

Kwa Wakristo.
Ukristo maana yake ni Ufuasi wa mafundisho ya Yesu. Kuna watu wanajichanganya kwa kusema Yesu ni Mzungu. Mimi nasema Yesu ni neutral, Yesu hana Kabila, nasema hana Kabila kwa sababu yeye hana Baba, yeye ana mzazi mmoja tu aliemzaa katika hali ambayo mpaka leo wanasayansi hawawezi kuielezea, hivyo hana kabila. Yesu alikuwa wa kipekee, mpaka sasa bado kuna debate maana muonekano wake haukuwa wa kawaida.

Waliipokea kwanza wakaiedit ndio wakatuletea sisi waafrika.
 
Dini za mababu zetu zilienda wapi? Nani aliziua? Kwasababu gani? Mbona walikuwa wanaabudu miaka nenda miaka rudi? Na walichoomba walifanikiwa?

Siamini kama dini zilizoletwa na wazungu ni sahihi kwa bara letu. Inabidi turudi kwenye dini za mababu zetu.

Dini ya babu yako ilikuwa ni Kutambika uchi na Kuua Kila mwenye macho mekundu!

Dini ya babu yako ilikuwa ikitokea Mafuriko au mitetemeko ya Ardhi wanamtoa mtoto kafara kwa kumchinja.! Au Kumzika akiwa hai.

Dini ya babu yako Mwanamke ilikuwa marufuku kula vyakula vinono manake mwanamke alikuwa ni chombo cha starehe tu.

Sasa km unaitaka dini ya namna hio anza kupiga marufuku nyumbani kwenu dada zako na wazee wako wa kike wasile chochote kuanzia mayai, nyama, pilau n.k.
Washindie mihogo mikavu tu na maji.
Ukifanikiwa hilo anza mazoezi ya kutembea Uchi.
Halafu utatupa taarifa unaendelea vipi.
 
Shetani ni roho ambayo inapomwingia binadamu anakuwa na mawazo kama haya. Kujifanya kunadi kuanzisha dini mpya ili atoke kivingine.
Ipo roho ya Mungu na ya shetani tu. Hiyo dini itaongozwa na roho ipi?
 
Alafu kwenye huu uzi hatutaki wadini sijui waduni maana wanatuchafulia uzi wetu! Kama vipi muende majukwaa ya dini.
 
Dini ya babu yako ilikuwa ni Kutambika uchi na Kuua Kila mwenye macho mekundu!

Dini ya babu yako ilikuwa ikitokea Mafuriko au mitetemeko ya Ardhi wanamtoa mtoto kafara kwa kumchinja.! Au Kumzika akiwa hai.

Dini ya babu yako Mwanamke ilikuwa marufuku kula vyakula vinono manake mwanamke alikuwa ni chombo cha starehe tu.

Sasa km unaitaka dini ya namna hio anza kupiga marufuku nyumbani kwenu dada zako na wazee wako wa kike wasile chochote kuanzia mayai, nyama, pilau n.k.
Washindie mihogo mikavu tu na maji.
Ukifanikiwa hilo anza mazoezi ya kutembea Uchi.
Halafu utatupa taarifa unaendelea vipi.

Acha chuki na dini za babu zetu😡
 
Back
Top Bottom