Afrika ilishaachwa na Mungu tangu kitambo

Afrika ilishaachwa na Mungu tangu kitambo

Andika neno Frederick Nitsche na ufuatilie aliishia wapi kadiri ya mtazamo kama wako.

usitishe watu wewe..Nitzsche alikuwa mzee wa totoz na alipata mental breakdown kwa sababu ya kaswende na ndiyo ugonjwa uliomuua baada ya kusambaa kwenye mfumo wake wa fahamu(neurosyphilis)kwavile wakati huo hakukuwa na matibabu ya kaswende
lingine?
 
Anza na mchakato wa kubadirisha jina la africa kwanza maana lina maana mbaya sana na mimi silipendi balaa. Ukifanikiwa kubadiri jina la bara mengine yatakuwa mepesi sana.
 
dini ya babu yako ilikuwa ni kutambika uchi na kuua kila mwenye macho mekundu!

Dini ya babu yako ilikuwa ikitokea mafuriko au mitetemeko ya ardhi wanamtoa mtoto kafara kwa kumchinja.! Au kumzika akiwa hai.

Dini ya babu yako mwanamke ilikuwa marufuku kula vyakula vinono manake mwanamke alikuwa ni chombo cha starehe tu.

Sasa km unaitaka dini ya namna hio anza kupiga marufuku nyumbani kwenu dada zako na wazee wako wa kike wasile chochote kuanzia mayai, nyama, pilau n.k.
Washindie mihogo mikavu tu na maji.
Ukifanikiwa hilo anza mazoezi ya kutembea uchi.
Halafu utatupa taarifa unaendelea vipi.

1.hata hizi za wazungu na waarabu nazo walikuwa wanatoa kafara kwa kuchinja wanyama.hatuambiwi kama walikuwa wamevua au wamevaa.hata kama wangevua ilimradi haina madhara bado ni imani. 2.kafara za watu hata kwene dini za wazungu na warabu zilikuwepo.ibrahm alitaka kumchinja mwanae eti atoe sadaka. 3.dini za wazungu na warabu zinanyanyasa wanawake mpaka leo isipokua shule imeokoa
 
kahtaan!
Usituletee uongo hapa sheikh, unasemaje uongo upo kwenye swaumu, no evidence no right to speak umemwambia mtu hapo juu, mbona wewe wafanya kama alivofanya, watu wote wa dini mnafanana katika kila kitu haswa kunyoshea watu vidole badala ya kundule.
Wewe walewale, tulia sindano zikuingue, wajifanya kuona errors za Yesu za kwako kipofu.
 
mzee wa funny ni aje!
Embu tupe maana ya hilo neno
 
Kabla ya kuandika huu uzi,mtoa mada alibidi afikirie au kusoma historia za zamana yaani mababu zetu....wana jamvi tunabidi tutambue,hakujawah kuwa na mungu wa waafrika bali miungu ya makabila, Afrika haijawah kuwa na tamaduni moja hasa katika mambo ya kijadi na kimila....wachaga walikuwa na mungu wao,wasukuma,wahaya kadhalika na kila kabila...

Somehow hizo practice bado zinaexist kwa sababu matokeo yake yanaonekana dhahiri unlike hizi dini zetu za sasa....kwa mfano.....unaumwa sana au unapata mikosi sana katika maisha yako,njia nyingi zimeshindwa kutatua tatizo,solution ya mwisho ni kurudi kijijini kwa wazee wa ukoo,utafanyiwa tambiko,au utaenda kutembelea kaburi la waanzilishi wa ukoo na vitu kama hivyo.....haya mambo si ya kuandika biblia sababu tunamiungu inayotofautiana jinsi ya kuiabudu na kuiomba....

kitu ambacho mtoa mada labda angesema na nikamsupport ni sisi kurudi kwa mababu zetu na kuwauliza habar za mizimu au miungu ya makabila yetu,jinsi ilivyofanya kazi na kuleta matokeo mazur kwa jamii...kwa kufanya hvyo hizi historia zitatembea kutoka kizazi kimoja mpaka kingine mpaka ifikie wakat watu wawe na uwezo wa kujudge dini ipi inawafaa kutokana na kuwa na knowledge ya kupembua mazuri ya upande mmoja na mapungufu ya upande wa pili.
 
Kufa Msalabani lilikuwa ni Fumbo kubwa, si wote wanaelewa fumbo hili. Wewe unadhani wale waliomuua msalabani angetaka kuwawajibisha angeshindwa?. Pole sana

Wazungu waliwachukua babu zetu mateka/watumwa na wengine waliuawa wakiambiwa kufa kwa yesu ni fumbo na wewe ukaamini hadi unafikia hatua ya kujitoa ufahamu.
 
Mswaada wa kuanzisha MUNGU wa Afrika nakuandika Biblia ya Afrika chini ya Uafrika.

Pia wataalamu na waamuzi mbali watakuwemo kama vile Ng'wanamalundi, Umuvuginza, nk.

Ninakaribisha maoni ya Uandikaji wa biblia hii. Kitaitwa kitabu cha uafrika, Tayari mchakato unaendelea, nakaribisha maoni ya wadau
.


Ungesubiri kidogo hadi baada ya OCT.2015 kwa sasa kama unavyofahamu imebaki miezi mitatu tuwe kwenye Uchaguzi kwa hiyo akili na muda tumeziazima kwa ajili ya UKAWA na dhani wewe nawe mdau pia.

 
1.hata hizi za wazungu na waarabu nazo walikuwa wanatoa kafara kwa kuchinja wanyama.hatuambiwi kama walikuwa wamevua au wamevaa.hata kama wangevua ilimradi haina madhara bado ni imani. 2.kafara za watu hata kwene dini za wazungu na warabu zilikuwepo.ibrahm alitaka kumchinja mwanae eti atoe sadaka. 3.dini za wazungu na warabu zinanyanyasa wanawake mpaka leo isipokua shule imeokoa

Kijana lzm utambue nini unaandika kabla ya kugusa "send"!
Kafara ya wanyama ni kitu cha kawaida kabisa ktk maisha yetu.

Suala la Ibrahim tayari umeshasema "ALITAKA kimchinja" sio alimchinja mwanae.

Wewe hakuna anaekukatazs kuabudu makaburi na mawe km babu zako. Na kutembea UCHI mbele ya Wazee wako na dada zako Lkn lzm utambue Kukaa uchi Ni kosa la jinai. Na ile tabia ya kuua watu wenye macho mekundu waliokuwa wanaifanya babu zako pia ni kosa la jinai.
Na kuvuta bangi kitu ambacho ni moja ya ibada za babu zako ni kosa la jinai vilevile.
Pombe za kienyeji hali kadhalika ni kosa la jinai.

Kwa hivyo Utakuta kila mtakachokifanya km walivyofanya babu zenu siku hizi ni Makosa ya jinai.

Mtatujazia Jela zetu kwa huu upuuzi. Jela zenyewe nafasi hakuna.
 
Sidhani kama jambo hili litafanikiwa, we jua Mungu ni mmoja tuu, na nje ya hapo ni miungu ambayo usingi kwao ni ndoto,maana ushindi ushaenda kwa huyu Mungu mkuu. Kama huyo mungu wa Africka au popote angekuwa na uwezo asinge shindw na Mungu huyu anaetajwa na kila nafsi iwe kwa kutaka ama pasi kutaka anatajika tuu ndie mshindi Yehova
 
Nikafikiri unataka KUAFRIKISHA UKRISTO kumbe unajitafutia kamradi kako kama alichofanya Kanye West. Kiriba kilekile unabadilisha mvinyo tu. Tafuta model yako, jina la unachotaka kukifanya na system ambayo itaonesha utofauti na UAFRIKA halisi na sio kuanza kutuambia ati UTAANDIKA BIBLIA ya dini ya Kiafrika.
 
Mswaada wa kuanzisha MUNGU wa Afrika nakuandika Biblia ya Afrika chini ya Uafrika.

Ndugu zangu Waafrika, kwa wiki mbili hivi nilikuwa nimezama kwenye tafakuri pana sana juu ya imani ya mtu mweusi dhidi ya dini, Mungu wake, Nimebaini waafrika tunaamini kisicho chetu, tumemetelekeza kuendeleza imani yetu na Mungu wetu na badala yake tunamwabudu Mungu wa masimulizi ya Ukalidayo na kuamini dini za kuletwa kwa majahazi,

Hivyo kwa heshima ya Dini ya kale ya Kiafrika na Mungu wetu, nimeaamua kuanzisha Mchakato wa uandikaji wa Biblia ya Dini ya Kiafrika na Uundwaji na usimikwaji wa MUNGU wa Afrika.

Bibilia hii itaundwa kwa vitabu vikuu VITANO, ambavyo itakuwa ni mkusanyo wa vitabu vifuatavyo;

Afrika ya Mashariki, Afrika Magharibi, Afrika Kaskazini, Afrika ya Kati, Afrika Kusini. Mitume tutakaowafuata maono yao ni pamoja na Chifu Mkwawa, Kitabu A.Msh Tagk, Chifu Monziyno, Kitabu A.Magh Nigr. Nk.

Pia wataalamu na waamuzi mbali watakuwemo kama vile Ng'wanamalundi, Umuvuginza, nk.

Ninakaribisha maoni ya Uandikaji wa biblia hii. Kitaitwa kitabu cha uafrika, Tayari mchakato unaendelea, nakaribisha maoni ya wadau
.

Your thinking ability is too low.
 
What??? Am I reading it right?! Mungu wa Africa! Kwani huyu Mungu si mwenyewe wa ukweli ?! Nitaendelea kusubiri ile ahadi aliyotuachia Yesu kwamba atarudi!
 
Nikafikiri unataka KUAFRIKISHA UKRISTO kumbe unajitafutia kamradi kako kama alichofanya Kanye West. Kiriba kilekile unabadilisha mvinyo tu. Tafuta model yako, jina la unachotaka kukifanya na system ambayo itaonesha utofauti na UAFRIKA halisi na sio kuanza kutuambia ati UTAANDIKA BIBLIA ya dini ya Kiafrika.

Nimependa huo msamiati KUAFRIKISHA UKRISTO
 
Asante mkuu....naamini umepata na wazo lililobebwa na hilo neno.

Swadakta! Maelezo yangu ya post #10 yanaweza kuwa summarized kwa msamiati huo tu na ukawa umetosheleza kile nlichokikusudia kwa asilimia kubwa tu
 
Wapi yesu kasema KUWENI WAKRISTO?

Au Wapi Bibilia imesema UKRISTO ni DINI?
Kutoa mawazo kichwani bila reference za mashiko ni safi sana km unaongea na Familia yako lkn hapa jukwaani hapafai.

Hapa bila Source unatafuta kuadhirika tu mkuu.

Ukristo umeletwa na MGIRIKI Aitwae PAULO. na Huko Bongo aliyetuletea UKRISTO sisi Ni MZUNGU aliyekuja na Meli ya Kwanza ya KUBEBA watumwa Iitwayo JESUS SHIP Mwaka 1534.

Mkuu Ukinijibu swali hili na mimi nitakujibu.

Wapi Mungu kasema Mbinguni kuna kufanya ngono na Mabikra?
Wapi Mungu kasema mbinguni kuna mito ya Pombe na Ulevi?
 
Back
Top Bottom