Museveni: Nkifika mbinguni nitapewa kitengo Cha kuchoma moto wavivu

Museveni: Nkifika mbinguni nitapewa kitengo Cha kuchoma moto wavivu

Labani og

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2020
Posts
23,033
Reaction score
33,020
Rais wa Uganda, , amesema bara la Afrika lina watu wengi waliopata utajiri mkubwa kwa njia za dhuluma badala ya kufanya kazi halali, akisisitiza kuwa vitendo hivyo haviwezi kuwa msingi wa maendeleo ya kweli.

1782989011572.jpg

Akizungumza katika hafla ya hadhara, Museveni alisema anawafahamu baadhi ya watu waliojitajirisha kwa kuwaonea na kuwadhulumu wengine, akieleza kuwa utajiri unaopatikana kwa njia hizo hauna baraka wala uhalali mbele za Mungu.

"hata Mimi Nitakapokuwa Mbinguni Nitakuwa nikihusika katika kuwachoma moto wote waliojipatia utajiri bila kazi"- Alisema

Kwa kauli iliyozua mijadala, Museveni alisema kuwa atakapokwenda mbinguni anataka kushiriki kuwachoma moto watu wote waliojipatia utajiri mkubwa kupitia dhuluma na unyonyaji, akisisitiza kuwa haki lazima itendeke kwa wale waliowaumiza wengine kwa ajili ya kujinufaisha.

Rais huyo alihimiza viongozi na wananchi kujenga utajiri kupitia kazi, uzalishaji na uadilifu badala ya kutumia madaraka, hila au dhuluma dhidi ya wengine. Alisisitiza kuwa maendeleo ya Afrika yatapatikana pale ambapo mali zitapatikana kwa jasho na si kwa kuwaibia au kuwaonea wananchi.

Maoni Yako ni yapi?
 
Back
Top Bottom