Afisa TRA - mtoto wa miaka 2 kumiliki ghorofa

Afisa TRA - mtoto wa miaka 2 kumiliki ghorofa

TRA inatakiwa ifumuliwe yote,mifumo ya ukusanyaji kodi iende na ualisia.mwaka jana wakati natoka China nikiwa na vitu nimevinunua kwa matumizi binafsi,wakati nipo hapo airport ofisa wa TRA aliniambia wao awafuati risiti inasemaje,TRA wao wana fourfigure yakodi kwa kila kitu,yaani mfano TV LCD inch 32 TRA wanakutoza 150000, japo mimi china niliinunua 160,000.ajalishi bei wao wana fixed tax rates,kuna mwenzangu alimnunulia mdogo wake shera la harusi dola 50,lakini pale airport aliambia shela la harusi kodi ni 1million.
Hapo ilibidi tutumie akili kumkichwa tutoke na vitu vyetu!!!!!,sio siri Maofisa wa TRA ni matajiri kiasi kwamba pesa walizonazo zinaweza endesha nchi hii miaka 3.bila kutegemea bajeti ya wafadhiri.
Mwasibu mmoja wa TRA hapa Dar ,ana hoteli ya thamani ya 3 bilion pale msamvu Morogoro,bakia majumba masaki na kigamboni viwanja
 
TRA, TPA na Kwingineko ni baraa jamani. Hatuhitaji Kagame tunahitaji akina Mgimwa wengi zaidi. Kazi kweli kweli
 
Mtoto wa miaka 2 atafanya vipi kazi tra? Hen rekebisha Uzi wako

Mtoto wa kigogo wa TRA ndiye anamiliki, saasa unashangaa nini maana hata wafagizi wanamiliki majumba ya kifahari, na akaunti zao ni mamilioni
 
Kila mtu anakula kwa urefu wa kamba yake...usilale mlango wazi kwa bahati ya mwenzio...IF YOU ARE ALWAYS AFRAID TO TAKE RISKS YOU WILL ALWAYS WORK FOR PEOPLE WHO DOES.Sasa mnasema wanakula rushwa halafu hamtaki EFD ndo nini sasa?Kwasababu hizo mashine zitazuia mianya ya wao kula Rushwa.
 
Hii ni moja ya sababu zinazofanya maCCM yasikubali kuwepo kwa VITAMBULISHO VYA TAIFA maana vitawaumbua kwa kutunza takwimu zote ikiwamo mapato na umiliki wa mali. Hapo jamaa kammilikisha ghorofa mtoto wa miaka miwili ujue kuna aliyomilikisha ndugu zake, ndugu za mkewe/ mumewe na hata watu hewa au marehemu kibao. Hii nchi acha tu, mkiona tunasema itoeni CCM madarakani tuanze upya ili kila mtu aishi kihalaliha hamtaki. Tanzania ni zaidi ya ujuavyo...
 
TRA wana utaratibu ambao ni compulsory kwa kila mtumishi ku declare assets anazomiliki yeye na family yake katika kila mwaka wa fedha hata kama angeandika jina la bibi yake bado anatakiwa kudeclare hio asset sembuse mtoto wake.
 
Mtoto wa miaka 2 atafanya vipi kazi tra? Hen rekebisha Uzi wako

Yaani kinachotokea hapo ni kuwa jamaa anafanya tra lakini anazo na kajenga ghorofa na ili asibumburukiwe limesajiliwa kwa jina la mtoto wake wa miaka 2!
 
ajabu ya nini mtoto wa miaka 2 kumiliki gorofa...? huo ni urithi wa mzazi kesha katiwa sasa tatizo nini?
 
TRA wana utaratibu ambao ni compulsory kwa kila mtumishi ku declare assets anazomiliki yeye na family yake katika kila mwaka wa fedha hata kama angeandika jina la bibi yake bado anatakiwa kudeclare hio asset sembuse mtoto wake.

Mkuu umeamua kujitoa ufahamu hivi hivi kama hauko Tanzania au ndio mambo ya division five...

Chenge anajaza fomu za mali kila mwaka lakini tulijua kuwa ana akauti Jersey kupitia kwa wapelelezi wa UK. Hizo fomu za kujaza mali unazomiliki ni sawa na CONDOM tu, ukiishamaliza kuitumia wakati wa kuijaza, inaenda kuwekwa kwenye faili na kupigwa vumbi milele. Hakuna mtu anayejishugulisha kufuatilia nini kinaendelea. Hakuna hata mtu mmoja anayejaza hizo fomu kwa taarifa za ukweli, kuanzia wajazishaji fomu, wakaguaji wake na wajaza fomu wote wanajaza taarifa za uongo. Nchi hii kuanzia raisi hadi waziri mkuu mpaka mfagizi wa ofisi ni mwizi na mwongo, wewe unaleta utaahira wa fomu za mali hapa kama unaongea na division five wenzio
 
Halafu jamaa wengine wanajifanya kunywa kwenye kontena eti wasijulikane ..
 
Mkuu umeamua kujitoa ufahamu hivi hivi kama hauko Tanzania au ndio mambo ya division five...

Chenge anajaza fomu za mali kila mwaka lakini tulijua kuwa ana akauti Jersey kupitia kwa wapelelezi wa UK. Hizo fomu za kujaza mali unazomiliki ni sawa na CONDOM tu, ukiishamaliza kuitumia wakati wa kuijaza, inaenda kuwekwa kwenye faili na kupigwa vumbi milele. Hakuna mtu anayejishugulisha kufuatilia nini kinaendelea. Hakuna hata mtu mmoja anayejaza hizo fomu kwa taarifa za ukweli, kuanzia wajazishaji fomu, wakaguaji wake na wajaza fomu wote wanajaza taarifa za uongo. Nchi hii kuanzia raisi hadi waziri mkuu mpaka mfagizi wa ofisi ni mwizi na mwongo, wewe unaleta utaahira wa fomu za mali hapa kama unaongea na division five wenzio

Yawezekana kweli nina division Five but a little advice as a colleague ukitaka kujua what goes on in a sytem u have to be in the system hayo mengine unayoongelea ni siasa na mimi sio mwanasiasa kama hufaham utaratibu wa kudeclare assets TRA its better uombe kuelimishwa zaidi ya kutoa maneno ya kejeli.
 
acha lawama za kitoto mkuu hata ungekuwa upo kwenye system usingeyaacha hayo mahela yakupite burebure
 
Nafikiri kuna haja ya kuifumua TRA na ajira zake kuwa za mkataba.Baadhi ya wafanyakaze wa TRA wana maisha ambayo ukiyapima kipato chake na maisha yake avilingani.Unamkuta mfanyakazi anamiliki BMW X5,X3,Nissan Murano na Prado latest tena vijana wadogo ndio wanamiliki,mbona nashindwa kuelewa au mishahara yao mikubwa
 
Ujue waTZ baadhi tumejaa unafki tu,ivi kwani kuna kosa gani mali yangu halali nikamwandika mwanangu kama urithi????ujue muache ujuha
 
Yawezekana kweli nina division Five but a little advice as a colleague ukitaka kujua what goes on in a sytem u have to be in the system hayo mengine unayoongelea ni siasa na mimi sio mwanasiasa kama hufaham utaratibu wa kudeclare assets TRA its better uombe kuelimishwa zaidi ya kutoa maneno ya kejeli.

Mkuu usitufanya wananchi wajinga. Tulijionea wenyewe watumishi wa TRA akina Mutarika walivyokuwa wanatamba na hela za rushwa na maV8 yao bila kuguswa na mtu we uje hapa kutuzuga kuwa mnazo fomu za kujaza mali. Nyie TRA kuanzia mfagiaji hadi mkurugenzi mkuu wote ni wezi, nyie ndio mnachochea wafanyabiashara kugoma. Mmevuruga uchumi wa nchi big time
 
maofisa wa tra ni wezi sana, kupata kazi tra inaonekana dili sana.
 
Back
Top Bottom