Afisa TRA - mtoto wa miaka 2 kumiliki ghorofa

Afisa TRA - mtoto wa miaka 2 kumiliki ghorofa

Sheria yetu ya kodi ina matatizo sana, hayo majamaa ya TRA yanawasubua sana wafanyabiashara kuwawekea vitu visivyo vya kweli ili wawahonge

Kutoka kwenye kipindi cha clouds fm live - PB na Gerald Hando. MWENYEKITI WA WAFANYA BIASHARA AWACHANA MAAFISA WA TRA. Anasema anaushahidi mtoto wa afisa wa TRA miaka 2 anamiliki ghorofa. Je Kama ni kweli hao maafisa wanapata hela zao kihalali, na amesema anaushahidi mfanyabiashara mmoja hulipa mil 60 kama kodi lakini hupewa risiti ya mil5.
Je Tanzania tutafika. Takukuru tusaidieni.

TANZANIA YA MWAGA MBOGA MIMI NAMWAGA UGALI

Source: CLOUDS FM POWER BREAKFAST NA GERALD HANDO
 
Haya sasa wameanza kutajana, Afisa wa TRA "anasaidia" MFANYABIASHARA kukwepa kodi kwa ujira fulani, kwa hiyo tatizo ni kwa wafanyabiashara wenyewe wanaokwepa hizo kodi na kutoa rushwa, kwa nini usilipe kodi by the book ili huyo afisaa asiguse senti yako?!!!..Lakini hata hivyo serikali imesikia kilio chenu wajasiriamali, NUNUENI MASHINE muepukane na usumbufu huo wote, kila siku unakagua mwenyewe unajua serikali inakudai kiasi gani, hakuna rushwa hakuna longolongo hakuna kukadiriana!

Kumbe wewe huijui nchi hii. Ukijifanya kifaru hutaki kutoa rushwa basi afisa akukadiria kodi mara 10 ya kodi halali na ukilipa hutaweza kushindana na wenzio waliolipa mil 60 wakaandikiwa mil 5, pia hutaweza kushindana na akina ridhiwani ambao wao na mitandao yao hawaguswi kabisa
 
Kuna makubwa yanakuja nyie subirini!mfumo wa ulipaji kodi tanzania unasikitisha!

TRA ni pazuri kufanya kazi kama assesor wa kodi basi Jk na mwanae wanapojimegea kule Wewe unajimegea huku, Patel akiingiza mzigo anaotakiwa kulipa kodi M200 unamwambia lipa M100 ila M50 lete ninywee bia
 
Mkuu huyo jamaa ana hasira na wafanyabiashara tu kwa sababu yeye analipa kodi( haijalishi hata km kwake ni kubwa kuliko alivyopaswa kulipa) anataka na wafanyabiashara nao walipe kodi hata km itakuwa kubwa kiac gani pasi kujua kwamba threats wa kodi ktk nchi yetu ni serikali( matumizi mabaya na wizi) na TRA( wizi) sasa yeye anaacha kupingana na threats anapingana na mlipakodi mwenzie: Napata kunbuka msemo usemao vita vya panzi furaha kwa kunguru: by the way kodi inalipwa kwenye profit na sio mauzo mf VAT
 
Hiyo mbona kawaida sana hata hayo ma mashine zao wafanyabiashara watawadanganya tu mtu atauziwa kitu cha m 5 mfanyabiashara ataforge na kusema kamuuzia cha laki nne wabongo hatuna utamaduni wa kudai risiti.
 
Back
Top Bottom