Afisa TRA - mtoto wa miaka 2 kumiliki ghorofa

Afisa TRA - mtoto wa miaka 2 kumiliki ghorofa

Napingana nae hapo anapotaka Kodi isikatwe katika mauzo,sisi watumishi tunakatwa Kodi katika basic sio take home!Walipe kodi wasilete usanii

Mkuu,

Una mapato Tshjs 100Mil, na matumizi Tshs 80Mil, unafikiri sahihi ni kukatwa kodi wapi? Kwenye Tshs 100Mil au Profit ya Tshs 20Mil??
 
Hizi tuhuma si za kweli. Wafanyabiashara wana bifu na TRA kwa ajili ya EFD. Kwa taarifa tu mali za mtumishi ye yote wa TRA huwa anazitangaza kwa mamlaka na serikali wakati anapoajiriwa, na kila mwaka wa utumishi wake TRA. Na anatangaza mali zote anazomiliki yeye mwenyewe, mke wake au pamoja na mke wake na hata kama umetoa zawadi kwa mtu. Mali hizi zinahakikiwa na vyombo vingine vya serikali kila mwaka, Hilo ghorofa ambalo amemilikishwa mtoto kama lipo lazima limeorodheshwa na kuhakikiwa. Nawasilisha.
Umechomoka toka kizani jamaa anamwagia mchanga kitumbua chenu???
 
Huu ndio ukweli, kuna bwana mdogo ninaemfahamu, ndani ya miaka miwili liweza kufanya vitu ambavyo katika miaka yangu 20 ya utumishi sikuwahi kuvifanya licha ya kwamba namzidi mshahara zaidi ya mara mbili. Nilishangaa sana. Lazima hawa watu wachunguzwe na tume huru na ikithibitika utajiri walionao wao au jamaa zao haundani na kipato chao, vitwaliwe na serikali kwa manufaa ya umma na wao washtakiwe kwa kujipatia mali isivyo halali

Kisa huyo bwana mdogo kakuzidi kipato pole sana
 
Kisa huyo bwana mdogo kakuzidi kipato pole sana
Kimising sikuwa na maana hiyo, si kwamba amenizidi kipato kwani nafahamu fika kuzidiana kipato ni suala lililo beyond na uwezo wetu wa kawaida wa kutafuta. Suala liko hivi, huyu alishindwa kuendelea na kidato cha tano, kwa maana akaishia kidato cha 4, then akajiunga na certificate course kisha akaajiriwa TRA(usiniulize certificate aliajiriwaje TRA miaka hiyo). Baada ya miaka 2, aliweza kumiliki gari tatu, nyumba tatu (moja ghorofa) nk. Namjua vizuri kuwa hana alternative ya kupata kipato cha namna hii kwani historia yake na familia yake naijua. Sasa wewe unaweza kutumia logic kama mtu wa namna hii anaweza ku-justify kipato cha namna hii nje ya mazingira yake ya kazi. Sina husda chembe na mtu huyu (kwani mimi pia ni mfaidika wa hali aliyonayo) ila nina husda na watu wa namna hii ambao wewe na mimi jamaa zetu wanakufa kwa kukosa aspirini kule kibondo na kwingineko.

 
Mtoto wa miaka 2 atafanya vipi kazi tra? Hen rekebisha Uzi wako

Wewe kweli komeka ulitakiwa uwe shule ya vidudu(chekechea) kama umeshindwa kuelewa hili, huenda wewe ndio urekebishe sentensi yako hapa ...Hen rekebisha Uzi wako
 
TRA wana utaratibu ambao ni compulsory kwa kila mtumishi ku declare assets anazomiliki yeye na family yake katika kila mwaka wa fedha hata kama angeandika jina la bibi yake bado anatakiwa kudeclare hio asset sembuse mtoto wake.

Hebu fikirisha kichwa kidogo kumiliki maana yake nini? nyumba imeandikwa jina la mtoto wake sasa yeye anamiliki vipi hapo?
 
ajabu ya nini mtoto wa miaka 2 kumiliki gorofa...? huo ni urithi wa mzazi kesha katiwa sasa tatizo nini?

Respect kwako kabanga, huwa nakuaminia sana ila hapa nadhani kidogo umeteleza, huyo mzazi aliyemrithisha kwa kipato gani halali cha kuweza kuijenga hiyo nyumba? Logic behind ni kuwa mzazi kajificha mgongoni mwa huyo mtoto.
 
Tra waache rushwa, lakini wafanyabiashara walipe kodi wamezoea kukwepakwepa!! Mbona sisi wafanyakazi hatuna vipato vikubwa tunalipa(tunakatwa mpaka senti ya mwisho). Walipe kwanza halafu mengine baadaye.
 
wafanyabiashara waache ubabaishaji,wao ndio wenye mazoea ya kuwapa rushwa hao wafanya kazi wa TRA,serikali imeamuwa kuanzisha hizi mashine ili kupambana na wezi wao wanajifanya kugoma na kudai eti mtoto wa miaka miwili anamiliki nyumba,kama kama wao wasingekuwa wanakwepa koda na kutoa rushwa kwa hao watu wa TRA hizo nyumba wangezinunulia kwa pesa ipi?
engmtolera wanasema huwezi jua kina cha maji bila kutumbikiza mguu, fanya biashara kumbana na TRA nadhani utakuja na lugha tofauti, kimsingi sidhani kama watu wanapinga kulipa kodi halali tatizo TRA ni wababe, mfano mtu ana kiduka mtaji wake sh milioni mbili leo anaambiwa anunue mashine ya hesabu ya shilingi laki 8 hivi inaleta maana kweli?

Pia hawa TRA huwa wanakadiria kodi mwanzoni mwa mwaka kwa matarajio kuwa mwisho wa mwaka watabalance, imetokea umepata hasara mwaka huo na ile Provisional Tax ushalipa maana yake umetoa sehemu ya mtaji kulipa kodi hapo utaendeleaje na biashara wakati umeshakula mtaji?

Kimsingi TRA hawajatoa elimu ya kutosha kwa mlipa kodi na ndio maana kila siku wanafukuzana na walipa kodi kama pimbi
 
Last edited by a moderator:
Tatizo ni rushwa na washamba, hakuna biashara zenye kuheshimiana kama za magendo. Kama kila siku unakula kwa mgongo wangu inabidi siku ninapokwama unilinde, kinyume na hapo ni kama hayo ya kumwagiana mboga na maugali.
 
Wafanyakazi wa TRA wananyodo sana, wanapindisha sheria kukandamiza wafanyabiashara. Wengi wanapenda rushwa kwa kulazimisha vitu visivyo takiwa.
Mbaya zaidi wakikuta hujui ABCD kuhusu kodi wanakufanya kama taahira
 
The whole system imekuwa corrupted kuanzia pale ikulu hadi serikali za mitaa. Ukiifumua TRA peke yake haitasaidia hata kidogo.
 
Nchi hujengwa na wananchi takukuru yenyewe haitakithi au kukabiliana na mambo bila ya wananchi kutoa taarifa, safi sana kwa taarifa hiyo lakini je suluhisho ni nini kwani hata kama muhusika atabanwa na kutiwa nguvuni bado kesi atashinda tu.
 
Kila mtu anakula kwa urefu wa kamba yake...usilale mlango wazi kwa bahati ya mwenzio...IF YOU ARE ALWAYS AFRAID TO TAKE RISKS YOU WILL ALWAYS WORK FOR PEOPLE WHO DOES.Sasa mnasema wanakula rushwa halafu hamtaki EFD ndo nini sasa?Kwasababu hizo mashine zitazuia mianya ya wao kula Rushwa.

.............aiseeh ! mbona unaongea kifisadi fisadi !!??😕:A S 13:
 
Tra waache rushwa, lakini wafanyabiashara walipe kodi wamezoea kukwepakwepa!! Mbona sisi wafanyakazi hatuna vipato vikubwa tunalipa(tunakatwa mpaka senti ya mwisho). Walipe kwanza halafu mengine baadaye.

.....hiyo mashine peke yake ni chanzo cha rushwa, tena wanachukuwa ofisini peupe !.........ukikutwa umejisahau tu kutoa risiti, duuh umekwishaa !
kuna maeneo kama kwenye Hardware na Spare za magari, duuh uko ndo hawalipi kodi kabisaaa na TRA hawaendi. Wamekazania visupermarket na viduka vya blue band na sukari !:A S-frusty:
 
wote hao ni wa sanii. wako baadhi ya tra wana chochea mgomo chini chini wana faidika na vitabu vya risiti feki. Na wafanyabiashara wanaona efd itawabana kukwepa kodi. Nchi hii anae umia nakodi ni mtumishi yake haikwepeki
 
Hizi tuhuma si za kweli. Wafanyabiashara wana bifu na TRA kwa ajili ya EFD. Kwa taarifa tu mali za mtumishi ye yote wa TRA huwa anazitangaza kwa mamlaka na serikali wakati anapoajiriwa, na kila mwaka wa utumishi wake TRA. Na anatangaza mali zote anazomiliki yeye mwenyewe, mke wake au pamoja na mke wake na hata kama umetoa zawadi kwa mtu. Mali hizi zinahakikiwa na vyombo vingine vya serikali kila mwaka, Hilo ghorofa ambalo amemilikishwa mtoto kama lipo lazima limeorodheshwa na kuhakikiwa. Nawasilisha.

.......duuh ! aiseeh..! ume overdose piriton nini ??:A S 13:
 
Back
Top Bottom