Afadhali daladala kuliko UDART

Afadhali daladala kuliko UDART

Kwa hiyo unafurahia vurugu za daladala? Kusimama ovyo kila sehemu bila kufuata vituo rasmi. Kwenda bila kuzingatia muda wa safari? Ama kweli wewe ni Tabutupu
tatizo lako umesoma hiyo post kama mtoto wa darada la kwanza.
 
unacho kisema ni kweli hata mimi nimeona. wameajili watu wa chini sana ili wawalipe bei ndogo. madereva wengi ni wale wa kuunga japo wana leseni.

Kinacho udhi zaidi kuna kituko kimetokea huko kimara, basi limetika katiakoo asubuhi na dereva alikua hataki kupakia watu wanao geuza hasa vituo vya baruti, kona , bucha , na korogwe.

Alipo fika bucha akasimamamisha gari mwanzo kabisa mwa kituo sehemu ambayo haina milango ili walioko ndani ya kituo wasiiongine na akawambia abiria wanao shuka bucha watetemkie mlango wa kushoto ulioko karibu na dereva upande ambao magari mengine yanapita.

Huyu dereva nimeshindwa kumwelewa ameamua kuweka maisha ya abiria kwenye hatari ili tuu asipakie wale wanao geuza wakati kazi yake yeye ni kuendesha gari, kufungua milango na kipakia.

Elimu ya watanzania nadhani bado tupo nyuma, naonea huruma wageni wanao dhani kuna usafiri wa BRT dar es salaam.
Kwa nini ugeuze.Huo ndio ushamba ambao ni kikwazo kikubwa katika utaratibu huu mzuri
 
Kwa nini ugeuze.Huo ndio ushamba ambao ni kikwazo kikubwa katika utaratibu huu mzuri
wewe ndio mshamba, hayo magari unapanda popote na unaenda popote. kazi ya dereva ni kutaja vituo, kufungua milango na kufunga full stop. usilete mawazo ya daladala hapa
 
Changamoto niliyoiona,baadhi ya madereva hawapendi kutaja majina ya vituo ila kuna wengine wanataja.Si abiria wote wanajua majina ya vituo kwakweli.Hili waliangalie.Narudia BAADHI YA MADEREVA
Mule ndani ya mabasi niliona kunasehemu ya display anayoweza kuwaonyesha abilia kuwa wamefika kituo fulani itumike hiyo pia wanaweza kurekodi sauti yenye vituo vyote kwenye route husika na wakaseti kwa kutumia spika ndani ya basi dereva anabonyeza batani yenyewe inasema ...ulaya wanafanya hivyo ingawa wao wanatumia mifumo ya sensors zaidi....!
 
N
1. Kwenye daladala abiria ndio mfalme , hata uwe mbali utasubiriwa, hata kama basi limejaa utaambiwa kuna nafasi etc

Sasa UDART ni kinyume chake kabisa, dereva ndio mfalme, anaamua apakie au asipakie, anaweza pita na gari tupu na asipakie, anaweza hata akadanganya eti gari bovu anaenda kupaki kumbe hataki apakie njiani, usumbufu kibao utadhani abiria wanapanda bure.

tofauti nyingine ongezeni..
Ngoja tuwaangalie kwanza
 
mkuu kunatofauti kati ya changamoto za kielemu na taaluma, wanachokosa hawa jamaa ni taaluma, na siku wakiligundua hlo changamoto hzo unazozisema zitabadilika na kuwa suluhisho..

wangekuwa na watu wanaojua kufuatilia mambo hasa wenye taalum ya usafirishaji, m naamini tusingekuwa na malalamiko haya, ila ingekuwa ni namna ya kujiendesha....

huu mradi kama si ufisadi wa namna ya kuuendesha leo hii naul ingekuwa tsh 200, na ingetolewa kama huduma, ila kwa kuwa ni biashara, ndiyo maana tunasema waajiri watu wenye taaluma,
Inachekesha sana, kila mtanzania anamuona mwenzio hana taaluma kwenye anachokifanya.
 
tatizo kubwa na kero ya haya magari ni kufika mbezi, ukishatoka mjini ukafika kimara mwisho unajuta, unaanza kuyakumbuka daladala za zamani.

kwanini hili tatizo la kimara wamekaa kimya?
 
Jamani hivi nauli za haya mabasi ni sh .ngapi maana sijawahi kupanda tangu tuanze kulipia
 
Sasa kwa nini mengine yasimame kila kituo,na mengine baadhi ya vituo kama hayajajaza abiria,huo si ndio usumbufu wenyewe? But daladala wanatafuta abiria kila mahali kwenye line yake! Nadhan wanaohusika wanatakiwa kurekebisha
 
Mimi kero niliyopata kuna dereva alitupitisha kituo ilikuwa tunashuka urafiki akatupitisha hadi shekilango. Yaani walishuka wawili tu akaondoa gari na gari lilikuwa lilimejaa sana hadi wakati wa kushuka ilikuwa ni taabu kufika mlangoni ila yeye hakuliangalia hilo alihesabu zile sekunde zake tu akafunga mlango na kutuacha tunasukumana tunataka kushuka. Kwa kweli hakutumia busara kabisa. Alinikera sana bahati yake sikushika namba ya gari ningemripoti kwa mabosi wake.
 
Sawa mkuu nimekuelewa hizo ni changamoto pia ila natumaini maoni watayasiki warekebishe hizo tatizo

sio kwa kiwango hicho, unapo angalia muda ulio tumia chukua.muda ulio fika kituo then angalia umetumia muda gani kufika unako kwenda.

Tatizo wengi wana angalia muda walio tumia kusafiri bila kuangalia wamatumia muda gani kusubiri tiketi, kusubiri gari na ule wa kusafiri.


wengi wanatumia saa moja hadi saa moja na nusu hata zaidi sometimes ukijumla muda wote unao tumia kupata usafiri.
 
Sasa kwa nini mengine yasimame kila kituo,na mengine baadhi ya vituo kama hayajajaza abiria,huo si ndio usumbufu wenyewe? But daladala wanatafuta abiria kila mahali kwenye line yake! Nadhan wanaohusika wanatakiwa kurekebisha
daladala kwenye customer care wapo vizuri sana.
 
Kero niliyoishuhudia ni kuhusu chenji. Kama hauna 650/# ya chenji utaganda hapo mpaka! Mi nilienda nikiwa na 10,000/# sikuwa na chenji...kila nikipanga foleni nikifikiwa mhudumu anakataa kupokea hela yangu...na siyo mimi tu...wote waliokuwa na 2,000/#, 5,000/# na 10,000/# tulikaa zaidi ya robo saaa wanakataa hela zetu.
 
UDART ni nzuri sema tu kuna mapungufu kidogo:
1. Magari ya kimara morocco ni machache
2. Kuna madereva hawana maadili nilimshuhudia kampitiliza mtoto sijui makusudi sijui bahati mbaya halafu akajibu jeuri
3. Kuna madereva hawaheshimu zebra yeye anakwenda tu sio wote wengine wastaarabu sana narudia wengine wastaarabu sana.
4. Kuna madereva hawajui kutunza muda wanayaendesha kama daladala fulani hivi, kituoni anazubaa bila sababu.
5. Kuna wale wadada wanaosaidia watu kupita kwenye vile vizingiti, wengine wana hulka mbaya, kama mtu akipita pale hajui jinsi ya kuscan risiti wanakuwa wakali badala ya kumuelewesha vizuri. Wanakera sana wanajiona wamefika.
Kumbuka:
Haya si mabasi ya kusubiri abiria, mmoja wawili twende mbele wako abiria. Kama unataka kusubiriwa rudi daladalani.
Siku njema mkuu.

Namba 3 na 5, nitawarudishia majibu mabaya tu siwezi kuvumilia mropokaji
 
yanasaidia ila kwa Morocco problem.Mimi nakuwa nyerere square kila siku SAA 2 usiku hivi.magari ya morocco machache sana.kila gari kimara kimara .mengine matupo yanaenda kupaki na abiria wsnasubiri
 
Back
Top Bottom