unacho kisema ni kweli hata mimi nimeona. wameajili watu wa chini sana ili wawalipe bei ndogo. madereva wengi ni wale wa kuunga japo wana leseni.
Kinacho udhi zaidi kuna kituko kimetokea huko kimara, basi limetika katiakoo asubuhi na dereva alikua hataki kupakia watu wanao geuza hasa vituo vya baruti, kona , bucha , na korogwe.
Alipo fika bucha akasimamamisha gari mwanzo kabisa mwa kituo sehemu ambayo haina milango ili walioko ndani ya kituo wasiiongine na akawambia abiria wanao shuka bucha watetemkie mlango wa kushoto ulioko karibu na dereva upande ambao magari mengine yanapita.
Huyu dereva nimeshindwa kumwelewa ameamua kuweka maisha ya abiria kwenye hatari ili tuu asipakie wale wanao geuza wakati kazi yake yeye ni kuendesha gari, kufungua milango na kipakia.
Elimu ya watanzania nadhani bado tupo nyuma, naonea huruma wageni wanao dhani kuna usafiri wa BRT dar es salaam.