Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,499
Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo Ado Shaibu amesema CCM inashinda kwa mbeleko ya dola, akitoa msimamo wa ACT Wazalendo kuhusu Uchaguzi
Kuhusu G-55 na Wabunge 19
"Tutawapokea, umezungumza kuhusu Kundi la G-55, mtu yeyote anayetaka kujiunga na ACT Wazalendo kwa nia ya Kugombea, kwa nia ya kuleta mabadiliko tutampokea hatutasita hata mara moja. Uteuzi utafanywa na vikao vyenye dhamana kwa mujibu wa Katiba, kwahiyo tunawakaribisha sana milango iko wazi"
"Habari ya Wabunge 19, yoyote yule anayetaka kujiunga na Chama hiki tutampokea na hatutasita hata kidogo na ukiona mwanasiasa anasita kumpokea mwanachama mtazame, we pokea mwanacha akishaingia ndani ya Chama ataendeshwa kwa mujibu wa Katiba na taratibu za Chama"
Kuhusu Reforms na Uchaguzi
"Tunashiriki katika Uchaguzi huu ili kwenda kulinda dhamani ya KURA, tumejiridhisha uamuzi wa ACT Wazalendo kususia Uchaguzi huu utafurahiwa Chama cha Mapinduzi hatutaki kutoa nafasi hiyo kwa CCM na sababu ya tatu tumesema CCM imeshindwa kuendesha nchi, ni wakati muafaka ikae pembeni tutaishinda!"
"Uzoefu wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019, Uchaguzi Mkuu 2020 na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 umedhihirisha kwamba CCM hakiingii madarakani kwasababu ya kupata baraka za Wananchi kupitia mchakato wa Kura, ukweli ambao umejidhihirisha bayana CCM inaingia madarakani kwa msaada wa dola"
"Sasa kama CCM inatumia dola kubaki madarakani, sisi tumesema tunashiriki Uchaguzi huu kwenda kupigania thamani ya Kura, tunakwenda kupambana! Na tumewaambia CCM wakae wajue Uchaguzi huu hautaenda kuwa wa kawaida, tutajibu mapigo ya CCM itakavyokuja, tumejiandaa, tumejipanga tunakwenda kukikabili Chama cha Mapinduzi"
"Kupitia oparesheni yetu ya Linda Demokrasia tunakwenda kuwahamasisha Watanzania wasimame imara wapambane na CCM mpaka Haki yao ipatikane"
"Tumekusudia kujenga vuguvugu kubwa la umma la kuwaleta pamoja wadau wote wa Demkrasia pamoja na Wananchi kwa ujumla wao kupambana dhidi ya CCM, nawaambia CCM haijawahi kuwa tested [kujaribiwa] vya kutosha, wametibia 2019 na 2020 tume-react vipi?, 2024 mwitikio wetu ni upi? ACT Wazalendo tunasema hii ngoma haitoenda kuwa kama tulivyozoea inaenda kuwa Nginja nginja"
Fomu Urais, Ubunge muda waongezwa
''Kamati ya Uongozi Taifa ya ACT kwenye kikao chake cha April 15, 2025 ilitoa maelekezo kwa Ofisi ya Katibu Mkuu kuongeza muda wa Wanachama kuchukua na kurejesha fomu za kugombea nafasi za Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Urais wa Zanzibar, Ubunge, Ubunge wa Viti Maalum, Uwakilishi, Uwakilishi wa Viti Maalum, Udiwani na Udiwani wa Viti Maalum ili kutoa fursa ya kutosha kwa wanachama kugombea, ninayo furaha kuwajulisha Wanachzma wa ACT Wazalendo na Wananachi kwa ujumla kuwa muda wa kuchukua fomu za kugombea nafasi za Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Urais wa Zanzibar, Ubunge, Ubunge wa Viti Maalum, Uwakilishi, Uwakilishi wa Viti Maalum, Udiwani na Udiwani wa Viti Maalum umeongezwa''
''Katika utekelezaji wa agizo la kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Feb 23, 2025, Ofisi ya Katibu Mkuu ilitoa maelekezo ya kuruhusu wanachama kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali, licha ya maelekezo hayo kutolewa kabla ya tamko rasmi la Chama cha ACT Wazalendo kushiriki kwenye Uchaguzi Mkuu 2025, Wanachama wetu wengi wamejitokeza kugombea nafasi mbalimbali''
''Mathalani, kwa nafasi za Ubunge, jumla ya Wanachama 317 wamechukua fomu hadi sasa, kwa nafasi ya uwakilishi, jumla ya Wanachama 106 wamejitokeza kuchukua fomu, tunapenda kuchukua fursa hii kuwapongeza Wanachama wetu waliojitokeza kuchukua fomu, kuchukua kwao fomu kabla ya Chama kutangaza ushiriki kwenye uchaguzi ni ishara ya wazi ya utayari wao katika mapambano ya kulinda na kutetea thamani ya kura''