ado shaibu

Ado Shaibu ni mwanasiasa kijana na maarufu nchini Tanzania. Anajulikana sana kwa nafasi yake kama Katibu Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, ambacho ni moja ya vyama vikuu vya upinzani nchini humo.

1. Nafasi ya Uongozi (ACT-Wazalendo)​

  • Ado Shaibu ndiye mtendaji mkuu wa shughuli za kila siku za chama cha ACT-Wazalendo upande wa Tanzania Bara na Zanzibar (pamoja na viongozi wengine wakuu).

  • Amekuwa na mchango mkubwa katika kujenga ushawishi wa chama chake, hasa kupitia midahalo, maandamano ya amani, na mikutano ya hadhara.

  • Kabla ya kuwa Katibu Mkuu, amewahi kushika nyadhifa mbalimbali ndani ya chama hicho, ikiwemo kuwa Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi.


2. Siasa za Hoja na Ushirikiano​

  • Anajulikana kama mwanasiasa anayependa kujenga hoja kuliko kutumia lugha za matusi. Mara nyingi husikika akizungumzia masuala ya uchumi, haki za binadamu, na uwajibikaji wa serikali.

  • Pia ni miongoni mwa viongozi wa upinzani waliounga mkono juhudi za maridhiano kati ya vyama vya siasa na Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, ili kuboresha mazingira ya kidemokrasia nchini.
  1. Roving Journalist

    JamiiForums Tanzania Ado ampigia simu Waziri Aweso kuhusu shida ya maji Tunduru, asema atatuma timu kutoka Wizarani

    Mbunge Ado Shaibu Ado alipiga simu Waziri wa Maji Aweso wakati wa mkutano na wananchi katika kijiji chake ili kuwasilisha changamoto kubwa za maji.Wananchi walikuwa wamelalamika kwa muda mrefu kuhusu maji machafu yanayotolewa kwenye visima, hali iliyowafanya kunywa maji yasiyo safi. Waziri...
  2. Roving Journalist

    JamiiForums Tanzania Mbunge Ado Shaibu: Sitaogopa Binadamu, nitaendeleaza mapambano ya kudai haki

    Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu Ado, ameapa kutoogopa vitisho vyovyote na kuendelea kupigania haki za wananchi wake. Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na umati mkubwa wa wananchi, mbunge huyo aliwahutubia wale wanaokandamiza haki, polisi wanaonyanyasa raia...
  3. BigTall

    JamiiForums Tanzania Ado Shaibu: Kama naenda kasi katika kuwasemea Wananchi niambieni nipunguze

    Wananchi wa Kijiji cha Kidodoma, Tunduru, wamemtaka Katibu wa ACT Wazalendo na Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu Ado kuendeleza kasi ya kuwasemea Wananchi na makundi mbalimbali, hususan katika masuala ya haki, utekaji na changamoto zinazowakabili wananchi. Wamesema hayo Septemba 23, 2026...
  4. Roving Journalist

    JamiiForums Tanzania Wanakijiji wa Machemba - Tunduru wamwambia Ado Shaibu kuwa hawana huduma ya maji safi

    Wananchi wa Kijiji cha Machemba, Wilaya ya Tunduru wameiomba Serikali kuwapatia vyanzo salama vya maji baada ya kueleza kuwa wanategemea kisima ambacho, kwa mujibu wao, hakikidhi viwango vya usalama kwa matumizi ya kila siku. Ombi hilo limetolewa Seotemba 23, 2026 baada ya Mbunge wa Tunduru...
  5. Waufukweni

    JamiiForums Tanzania PostGE2025 Mwananchi amwambia Ado Shaibu, wewe upo Bungeni unachukua posho wakati ndugu zetu walipotea. Wewe unajisikiaje?

    Katika mkutano wa hadhara wa Chama cha ACT Wazalendo wa Septemba 11, 2026, uliofanyika Kata ya Dutwa, Jimbo la Bariadi mkoani Simiyu, mwananchi Fulani amesimama na kumhoji Katibu Mkuu wa chama hicho ambaye pia ni Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu, kuhusu sababu za yeye kuendelea kubaki...
  6. Roving Journalist

    JamiiForums Tanzania Ado Shaibu: Yuko wapi aliyekuwa Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi?

    Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu Ado, ametoa wito kwa familia ya Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Emmanuel Nchimbi kujitokeza hadharani na kuwahahakishia Watanzania kuwa yuko salama. Ado ametoa wito huo Septemba 10, 2026 wakati akizungumza katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika Kata ya...
  7. R

    JamiiForums Tanzania Ado Shaibu: Tundu Lissu ni Mandela wetu hapa Tanzania

    Akizungumza jana, Septemba 8, 2026, kwenye Mkutano wa Kitaifa wa Kutafakari Hali ya Kisiasa Nchini, Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu, amesisitiza kuwa mchakato wa maridhiano ya kisiasa nchini unahitaji mazingira na msingi sahihi ili uweze kuzaa matunda ya kweli. Akitolea uzoefu wa...
  8. Roving Journalist

    JamiiForums Tanzania Ado Shaibu asema Soko Kuu la Tunduru (Soko la Azimio) lipo katika hali mbaya, ahoji ujenzi utaanza lini?

    Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu akiwa Bungeni leo Septemba 2, 2026 amehoji kuhusu ujenzi wa soko la kisasa na la kimkakati katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru ambalo ameeleza kuwa Soko Kuu la Azimio lililopo sasa halikidhi mahitaji ya mazingira ya sasa.
  9. Roving Journalist

    JamiiForums Tanzania Ado Shaibu ahoji kuhusu utekeleza ahadi ya ujenzi wa Kituo cha Afya Namiungo wilayani Tunduru

    Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu Ado, amehoji hatua zinazochukuliwa na Serikali kutekeleza ahadi ya ujenzi wa Kituo cha Afya Namiungo wilayani Tunduru, akisema ahadi hiyo ilitolewa na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli. Ado amesema Kata ya...
  10. DodomaTZ

    JamiiForums Tanzania Ado Shaibu Ado katika Ibada ya Jubilei ya Miaka 25 ya Upadre ya Mhashamu Askofu Filbert Mhasi, Tunduru

    Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu Ado ameshiriki Ibada ya Jubilei ya Miaka 25 ya Upadre ya Mhashamu Askofu Filbert Mhasi wa Jimbo Katoliki Tunduru Masasi iliyofanyika katika viwanja vya Kanisa la Mtakatifu Xavery Tunduru, Agosti 23, 2026.
  11. DodomaTZ

    JamiiForums Tanzania Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu Ado alivyopokelewa Tunduru

    Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu Ado amepokelewa kwa kishindo na shangwe kwenye mkutano wake wa hadhara uliofanyika viwanja vya Baraza la Idd Tunduru Mjini, tarehe 23 Agosti 2026 kwa ajili ya kutoa mrejesho wa Mkutano wa Bunge la Bajeti na kukusanya maoni kuelekea Mkutano wa Bunge ujao...
  12. Roving Journalist

    JamiiForums Tanzania Ado Shaibu: Nimewasilisha Hoja ya kulitaka Bunge liazimie Serikali iwasilishe ramani ya mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya

    TAARIFA KWA UMMA Nimewasilisha Bungeni mapendekezo ya masuala mawili muhimu kwa ajili ya kupangiwa muda na kushughulikiwa katika Mkutano wa Nne wa Bunge, unaotarajiwa kuanza tarehe 26 Agosti 2026. 1. HOJA KUHUSU MCHAKATO WA KATIBA MPYA Kwa mujibu wa Kanuni ya 64(1) ikisomwa pamoja na Kanuni ya...
  13. K

    JamiiForums Tanzania Ado Shaibu: CCM na Serikali hazina nia ya dhati ya KATIBA mpya

    Mbunge Ado Shaibu wa jimbo la Tunduru Chama cha ACT-Wazalendo amewasilisha hoja nzito akibainisha kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan hazina madhumuni ya dhati ya kuwapatia Watanzania Katiba Mpya. Akizungumza katika Kongamano la Vijana...
  14. Mwanamwana

    JamiiForums Tanzania Ado Shaibu: Ukifunga mlango wa Demokrasia, unafungua mlango wa machafuko

    Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu, amesema maridhiano ya kisiasa hayawezi kufanikiwa bila kuwepo kwa ukweli na uwajibikaji kuhusu matukio ya kisiasa yaliyotokea nchini. Amesema hatua ya kwanza katika mchakato wa maridhiano ni kuweka wazi ukweli kuhusu matukio yaliyojitokeza kabla, wakati...
  15. R

    JamiiForums Tanzania Ado Shaibu: Ndani ya bunge hairuhusiwi kuzungumzia utekaji, ufisadi, yaliyotokea Oktoba 29 hata kurejea ripoti ya CAG

    Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu, akizungumza katika Jukwaa la Demokrasia lililofanyika leo Julai 9, 2026, amesema; "Kwa sasa bungeni ni kama umewekwa utaratibu ambao haumo kwenye kanuni, lakini hakuna space ya kuzizungumzia. Hauruhusiwi ndani ya bunge kuzungumza juu ya utekaji...
  16. McLaren

    JamiiForums Tanzania Ado Shaibu: Wanajifanya nao wanataka Katiba Mpya kama mbinu ya kuhujumu na kuchelewesha mchakato

    Wakuu, Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu, amedai kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakina dhamira ya kuendeleza mchakato wa Katiba Mpya, akisema hadi sasa hakuna hatua zozote zinazoonyesha utekelezaji wa ahadi iliyotolewa kuhusu kuanza kwa mchakato huo. "Sasa mimi nawauliza, tangu tuapishwe...
  17. Mwanamwana

    JamiiForums Tanzania Ado Shaibu: Polepole ametekwa, CCM imeshindwa kumtetea - Kama hawawezi kuteteana wenyewe, watawezaje kuwatetea wananchi?

    Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu Ado, ameikosoa vikali CCM kwa ukimya wake kuhusu madai ya kutekwa kwa aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho na Balozi wa Tanzania, Humphrey Polepole, akidai hatua hiyo inaonesha unafiki wa kisiasa na kudhoofisha matumaini ya wananchi kupata...
  18. M

    JamiiForums Tanzania PostGE2025 Ado Shaibu: Jeshi Kuna kitu kimoja wakilinde kwa nguvu zote, kitu hiko ndio roho ya thamani yao Jeshi lijitenge na Siasa

    Mbunge Ado Shaibu amesema akichangia Bungeni leo, Mei 19, 2026 amesema kuwa kati ya vitu ambavyo Jeshi linapaswa kuvilinda sana ni kutojihusidha na Siasa. Hayo ameyasema akiwa Bungeni wakati akichangia hoja Pia soma: ACT Wazalendo: Spika Zungu anatumia madaraka vibaya, amkalisha chini Ado...
  19. R

    JamiiForums Tanzania Ado Shaibu: Maveterani vita vya Kagera hawajalipwa hadi leo, Je ahadi ya Serikali ilikuwa ni siasa ya maneno matupu?

    Akizungumza Bungeni leo Mei 19, 2026, Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu, amezua mjadala kuhusu kucheleweshwa kwa malipo ya posho kwa Maveterani wa Vita vya Kagera "Mimi jimboni kwangu, wazee hawa wapo. Wengi wao, umri wao ni baina ya miaka 70 mpaka 90. Vikongwe. Lakini taarifa nilizonazo...
  20. R

    JamiiForums Tanzania Ado Shaibu: Namuomba Mungu Mapambano ya kuing'oa CCM Madarakani yafanikiwe

    Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu, amesema hayo Aprili 27,2026 akiwa katika mahojiano Wasafi FM
Back
Top Bottom