Adhabu ya Kunyonga Hadi Kufa imepitwa na wakati?

^^
Mngetupa feedback kwanza,,wale waliohukumiwa kifo mf. Tanzania wangapi Rais amepitisha saini ya kuwanyonga?
Vipi mabwana jela wale ma-specialists wa kunyonga wanatimiza wajibu wao?
^^
 
let me tell you something. kwamba hakuna kitu cha thamani kama uhai ,pale mtu anapoutoa uhai wa mtu mwingine utalinganisha vipi na kifungo cha maisha mtu akifungwa maisha atafanya mambo yafuatayo ,atakula,atalala,akiugua atatibiwa,atakutana na ndugu zake ,jiulize yule aliyeuwawa anapata haki hizo? na nduguzake wanaomtegemea watoto mkewake wanaishi vipi utakuta wanalala njaa hivyo basi hukumu ya kifo lazima itekelezwe ili haki itendeke maana imeandikwa auae kwa upanga atauawa kwa upanga
 
Na isitoshe ni unconsitutional kila mtu anayo haki ya kuishi but there are exceptions hiyo right kuwa terminated" hapa wanaangalia public respond on given agender is it ascertain truth? Example hii issue ya albino..uiengereza walitaka waifanye as genocide but kilichokosekana ni common phenomena...kwa hiyo ilo swala hapa kwetu serikali(public) imelaani hicho kitendo sio tu kinyume cha katiba ni kinyume vilevile cha UDHR..hapo lazima exeption ifanye kazi..nchi nyingine hukumu ya kifo imetolewa...
 
An eye for an eye bila hivi dunia haitokua mahali salama pa kuishi. Imagine majambazi yanayoua watu innocent kikatili unadhani kunyimwa tu uhuru wa kuzunguka mitaani ndo adhabu tosha!!? Tena kunyongwa ingebadilika iwe kuchinjwa kwa msumeno.
 
Nadhani tujenge majengo mengi na makubwa ya magereza maana hukumu ya kifo si nzuri. Tufunge maisha. Zaidi Kwa upande wangu kwa kweli sikubaliani na hukumu ya kifo na sidhani kama inaleta nidhamu kwenye jamii zaidi sana inaondoa uhai wa mtu, kwamba wengine wataogopa kufanya mauaji!

Mabadiliko ya mtu hayatokani na hofu, bali inahitajika badiliko la ndani kujua kuwa kuua ni vibaya, na sipaswi kufanywa hivyo! Pia kama serikali itasimamia vizuri nizamu na sheria zake watu wanaostahili kuuwawa watakuwa wachache.
 
hukumu ya kifo iwepo ili ku deter raia ila inapotolewa lazima tuangalie mazingira huwez kuua familia nzima tukakuacha
 
Utajua umuhimu wa hukumu ya kifo mara baada ya kufikwa na janga la kuwawa kwa mtu wako wa karibu ama wewe kuchanwa mapanga na vibaka. But inatia simanzi kuiruhusu kama halijakufika jamani
 
Kaka nafikiri kifo sio adhabu,ni ngumu kusema kifo ni kibaya wakati hakuna mtu aliyeenda na kurudi kutuambia jinsi kifo kilivyo kibaya,....

Hebu fikiria,mtu anlawiti vitoto,anaua watu kwa sababu na imani za kipuuzi,............hapa ni lazma mtu ajutie kile alicho kifanya

Nakubaliana na wewe mkuu IGWE, HUKUMU YA KIFO SIYO ADHABU bali ni KUMUONDOA MKOSAJI KWENYE JAMII YA WANADAMU, kwa sababu aliyoyatenda ni zaidi ya UNYAMA na HASTAHILI KUISHI! Pia ni funzo kwa waliobaki kuwa ukifanya UNYAMA unanyang'anywa haki ya kuishi.

Jela ni sehemu ya kuwatenga mbali na jamii na kuwahifadhi wale wote walio watendea wenzao (jamii) maovu. Ni sawa na watu walionyongwa kwa muda kisha wakahuishwa. Kwa vile makosa yanatofautiana uzito, NI VYEMA HUKUMU YA KUNYONGWA IENDELEE KUWEPO!-Kama unabisha subiri vibaka wambake na kumnyonga binti yako wa pekee aliyemaliza chuo kikuu kwa ajili ya kumpora smart phone uliyo mnunulia mwezi jana!

Watu wanaoipinga hukumu hii, ni wale ama wanatenda maovu yaliyopitiliza ama wanania ya kutekeleza uovu wao hapo baadaye. Au ni watu ambao wanauwezo na kujiwekea ulinzi ili asije fanyiziwa na wakora.

Hukumu hii inatakiwa itekelezwe kwenye nchi za wastaarabu waliojiwekea misingi mizuri ya sheria na utekelezaji wake. Nchi kama Tanzania, pesa na madaraka viko juu ya sheria, hivyo utekelezwaji wa hukumu hii itatumiwa vibaya na wenye pesa na madaraka! Ndiyo maana hata marais wanaogopa kusaini utekelezaji wa kunyonga kwa sababu wanajua udhaifu wa mahakama zetu.
 
VoiceOfReason

Kiukweli watu wengi tunaishi lakini kifo kinaogope na kinaleta fear sana so adhab ya kifo kwa namna moja au nyingine inasaidia,na sana inakuwa funzo kwa wengine kuogopa adhab ya kifo
 
Ukweli nikwamba adhabu ya kifo iwepo ili liwefunzo kwa wengine kama unavyo jua kifo kina ogopeka unapo kifuata.Hiyo inabidi iwepo.
 
Nakubaliana na hukumu ya kifo,iwepo na iendelee kutumika bila kumcheleweshea haki muuaji.(aliyehukumiwa kufa)

Nielewavyo mimi ni kwamba, hadi ifikiapo mtu kuhukumiwa kifo ni kuwa imethibitishwa wazi kuwa mtu huyo alikusudia kutenda mauaji(kifikra na kwa kutenda)...ni dhahiri naye kuhukumiwa vivyo hivyo kufa(mara moja pasipo huruma)

kwasababu, malengo ya hukumu ni kutufunza,kutukumbusha wajibu wetu,kuzuia uwezekano wa kujirudia kosa wakati mwingine, na pia kumuadhibu mkosaji...inategemeana na aina ya kosa.

Katika kosa la kuua, ni vyema hukumu ibebe mjumuisho huo wa malengo yote kwani hapo hakuna tena rufaa ya maisha ya marehemu, hakuna ajuae gharama ya ghadhabu ya waathirika wa kifo marehemu n.k
 
Ndiyo imepitwa na wakati, kwani tukiangalia lengo la hukumu ya kifo kama adhabu kwa wahalifu haijafaulu, adhabu ipo lakini watu bado wanaua labda kama llengo ni kulipiza kisasi(REVENGE) bas haijapitwa na wakati lakin kama ni (DETERENCE) IMEPITWA NA WAKATI
 
Ndiyo imepitwa na wakati, kwani tukiangalia lengo la hukumu ya kifo kama adhabu kwa wahalifu haijafaulu, adhabu ipo lakini watu bado wanaua labda kama llengo ni kulipiza kisasi(REVENGE) bas haijapitwa na wakati lakin kama ni (DETERENCE) IMEPITWA NA WAKATI

Na kifungo cha maisha ni deterrence?

Binafsi sidhani kama lengo ni detterence. Lengo ni kutenda haki tu, basi.
 
at the moment death by hanging has been declared to be inhuman act, which is against "customary international law" which is binded in most of treaties under international law principles(UN charter) one is 2 promote "jus cogency" covered by "pacta sunt serevanda" principle that any treary a state sign..should observe these principles hapa kwetu tumesaini mikataba mingapi ya nje? tumesaini mikataba mingi siyo?

kwa huyo jueni, any act which includes derogation ambazo zimetajwa ni genocide, war crime,and crime against humanity kwenye ICC statute zinapinga any act which is against humanity(state to individuals) within international norms kwa hiyo ni ngumu raisi kusaini adhabu ya kifo coz zipo ad hoc comittee kutoka umoja wa kimataifa barazaa la usalama la jamii za kimataifa wanaoobserve these principles za kimataifa, kwa hiyo ni ngumu kwa raisi kusaini adhabu ya kifo.
 
hivi mtu anaua watu kinyama bila huruma,mtu anachukua binadamu anamchinja harafu anaweaka nyama dukani ya binadamu huyo ni mtu?huyo anastahili nae kufa tu maana si binaadamu wa kawaida.ni bora kuondoa mtu mmoja kuliko mmoja akasababisha madhara makubwa.HII sheria haijapitwa na wakati
 
Back
Top Bottom