Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 4,783
- 14,975
ACT-Wazalendo, tumeshangazwa na kushtushwa na Ujumbe mfupi wa SMS, kutoka Tume ya Uchaguzi Zanzibar, ambao wanatumiwa wananchi, kufika katika Ofisi za Uchaguzi za Wilaya kuchukua Vitambulisho vyao vya kupiga kura (Vote I'd), kuanzia tarehe 17/07/2025, katika Siku na saa za kazi.
ACT Wazalendo, tunauchukulia Utaratibu huu mpya wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), kuwataka wananchi kufuata vitambulisho vyao katika Ofisi za Wilaya, kuwa ni Mpango Maalum unaoratibiwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar kwa Mashirikiano makubwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), wa kuwanyima na kuwakosesha wananchi wengi haki yao ya kikatiba ya kupiga kura, kwani ni dhahiri kwamba mbinu hii hii ndio ambayo inatumika kuwanyima wananchi wa Zanzibar Vitambulisho vya Mzanzibari na kuwanyima fursa wananchi wapatao 20,715 haki ya kuandikishwa katika Daftari la Kudumu la Mpiga kura.
ACT Wazalendo, Tunaitaka Tume ya Uchaguzi Zanzibar, kuachana mara moja na Utaratibu huu na mbinu hii ya kuisaidia CCM kwa kupunguza wapiga kura kwa kuwanyima Vitambulisho vyao kupitia Ofisi za Wilaya, ni wazi kwamba katika zama hizi CCM hasa kwa upande wa Zanzibar, haisaidiliki tena hasa kwa aina ya Mgombea ambae wamempitisha, wananchi wa Zanzibar wamechoshwa na Umasikini na Ufisadi unafanyika ndani ya Serikali inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi.
ACT Wazalendo, Tunaitaka Tume ya Uchaguzi Zanzibar, kurudi katika Utaratibu uliozoeleka wa kupita katika Shehia na kugawa vitambulisho hivyo, jambo hili litasaidia wananchi walio wengi kupata vitambulisho vyao kwa urahisi na haraka na kuwapungizia Usumbufu na gharama zisizo za lazima, kulazimisha vitambulisho hivyo kutoka Wilayani bila ya kueleza Utaratibu ambao utatumika ni njama ya kuwakosesha wananchi hao haki yao na kuwaletea Usumbufu usio wa lazima na kusababisha taharuki.
ACT-Wazalendo, tunapatwa na mashaka makubwa na kujiuliza ikiwa ZEC wametueleza kwamba kwa Awamu ya Pili wameandikishwa wapiga kura wapya 101,641. Ni kwa namna gani watagawa vitambulisho hivyo katika Ofisi za Wilaya tu, ni wazi kwamba upo Mpango Maalum wa kupunguza idadi ya Wapiga kura hasa baada ya kutathmini na kuhakikisha kwamba Chama Cha Mapinduzi na Mgombea wao Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi wamekataliwa na Wazanzibari walio wengi, hivyo wanatafuta namna ya kumsaidia ingawa kwa Sasa wamecherewa kwani hasaidiliki tena.
Wito wetu.
1. Tunawataka wananchi wote wa Zanzibar, kwenda kwa Wingi katika Ofisi za Wilaya Kuchukua Vitambulisho vyao na wasikubali kuvunjwa moyo na kukatishwa tamaa kwani huu ni Mwaka wa Maamuzi kwa Wazanzibari wa Kuendelea kuikataa CCM katika sanduku la kura, na Kwa Mwaka huu hakuna kitakachutuzuia tusichukue na kuongoza Nchi hii ili wananchi wa Zanzibar wafaidi matunda ya Mageuzi yao.
2. Tunaitaka Tume ya Uchaguzi Zanzibar, mara moja kurejesha utaratibu wa kutoa vitambulisho vya wapiga kura katika Shehia kama ilivyozoeleka na ambavyo wamekuwa wakifanya mara zote, iweje zoezi la uandikishaji wapiga kura lifanyike katika Shehia lakini ugawaji wa Vitambulisho ufanyike Wilayani?
Imetolewa tarehe 17/07/2025 na:-
Salim Bimam,
Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma,
ACT Wazalendo.