logician mkuu
JF-Expert Member
- Jun 2, 2014
- 792
- 221
Mi nawashangaa sana nyie,hivi Ukawa inawahusu kweli nyie wanachama au inawahusu wenyewe tu viongozi wake?
Yaani hio propaganda wapelekee watoto wa chekechea.
Mi nawashangaa sana nyie,hivi Ukawa inawahusu kweli nyie wanachama au inawahusu wenyewe tu viongozi wake?
Yaani hio propaganda wapelekee watoto wa chekechea.
CHADEMA at it's best. Kuamulia vyama vingine cha kufanya na kutokufanya. Naona dalili za stroke kwa mbali kwenye ubongo wa UKAWA.
Chanzo: Habari247
MYTAKE:
1) yaani mbwembwe zote zile za zitto na wenzake kuzunguka nchi nzima wameambulia wanachama 700 tu??? hata kura za kata moja hawajafikisha?? huu sasa utani....ndio maana zzk amekata tamaa na ziara ya pili???
2) Kwani kiongozi Mkuu zitto sialisema Ukawa ni wasakatonge??? na yeye anataka kujiunga na wasakatonge ???
3) Huyu mama sialisema "Nimarufuku Mwana Act kushabikia Ukawa"???
.....................
Professor kilaza.
Chanzo: Habari247
MYTAKE:
1) yaani mbwembwe zote zile za zitto na wenzake kuzunguka nchi nzima wameambulia wanachama 700 tu??? hata kura za kata moja hawajafikisha?? huu sasa utani....ndio maana zzk amekata tamaa na ziara ya pili???
2) Kwani kiongozi Mkuu zitto sialisema Ukawa ni wasakatonge??? na yeye anataka kujiunga na wasakatonge ???
3) Huyu mama sialisema "Nimarufuku Mwana Act kushabikia Ukawa"???
.....................
Professor kilaza.
Chanzo: Habari247
MYTAKE:
1) yaani mbwembwe zote zile za zitto na wenzake kuzunguka nchi nzima wameambulia wanachama 700 tu??? hata kura za kata moja hawajafikisha?? huu sasa utani....ndio maana zzk amekata tamaa na ziara ya pili???
2) Kwani kiongozi Mkuu zitto sialisema Ukawa ni wasakatonge??? na yeye anataka kujiunga na wasakatonge ???
3) Huyu mama sialisema "Nimarufuku Mwana Act kushabikia Ukawa"???
.....................
Professor kilaza.
Kwa nini wana CCM nao wanaonekana kuwa na interest ya kuona Zitto anaingia UKAWA?
Mkuu respect wa boda salam!
Nimefurahishwa na mchango wako wa kwanza kabla ya huu hapa kuhusu, umuhimu wa kuwashirikisha ACT katika UKAWA. Kwangu mimi hilo ni jambo jema sana lakini si salama hata kidogo kufanya hivyo katika kipindi hiki hasa tunapoelekea uchaguzi kwa mtazo huu;
1. Kwa muda mfupi tangu Kiongozi wa chama aondolewe kwa katiba ya chama chake cha zamani, hajaonesha rangi yake halisi kwa uchungu wa kuodolewa katika chama ambacho kwa dhati ya moyo wake alihusika pia kukifikisha hapo kilipo. BADO ANAHASIRA kumuingiza katika kundi akiwa na uhuru mpana kama kiongoz wa chama mshirika wa UKAWA ni sawa na kumpa rungu kumalizia kazi aliyoianza mapema. Ndio anaumuhimu ktk kundi lakini sio sasa. UKAWA watafute njia mbadala ya kuwawin mashabiki na wakereketwa wao lakini si kwa njia uliyopendekeza.
2.Je umejaribu kufikiria chama tawala kitaendesha kampeni gani za kuipunguzia UKAWA wabigakura iwapo jamaa atarudishwa kundini? Je vp kwa watu waliojitolea (dyinhard) wa ukawa watachukulia vp kurudi kwa kiongozi wa chama katika kundi?
Kiufupi nadhani wanaukawa wampe muda kiongozi wa chama huko aliko aweze kupractiz kile anachokiamini kwa muda walau wa miaka miwili ndipo wamrudishe wakati vidonda vya ndg zake wa ukawa vikiwa vimepona.
Washabiki wa siasa mnatabu sana,kabla ya ukawa hivyo vyama vilishaitana ccm B,mashoga na wengine hadi walimsaidia Kikwete ashinde. Lakini leo hii wote kwa pamoja et ndiyo wameunda ukawa,hivyo hata si ajabu pia kuona ACT wamejiunga na ukawa.
Alisema kuwa chama hicho kimepokewa
vizuri na wananchi wa mikoa mbalimbali
nchini na katika ziara ya awamu ya
kwanza walifanikiwa kuingiza jumla ya
wanachama wapya 700. yaan hii ni idadi ya wanachadema kijiji cha kibumbe na Ilundo tu Kata ya Kiwira. tukuyu
Umeongea uhalisia wa siasa za kileo hope viongozi wa UKAWA watalifanyia kazi wazo lako.kinachowakera watu wengi ni utoto wa viongozi na mashabiki wa ACT dhidi ya viongozi wa vyama vingine vya Upinzani. Hilo tu ndilo linalowaharibia.Mkuu Malalika, salam pia!
Nitajibu hoja zako kwa mtindo uleule wa mpangilio wake ktk kuzijenga. Na hapa wakati nikikujibu naomba ieleweke kwamba mimi ni Die hard UKAWA na CHADEMA.!! Sijui litatokea jambo gani la kuniondosha kwenye imani hii niliyonayo dhidi ya umoja huu na chama changu. Na kwa kuthibitisha hilo mkuu Malalika, mimi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa (Sikuwahi kusbiriki zaidi ya mwaka huu) nilikuwa nikipigia kura kwenye chama bila kujari ni kiongozi gani aliyekuwa akigombea kupitia chama changu. Na hapa mpaka leo simjui hata kiongozi mmoja awe mjumbe au Mwenyekiti..! Ninachojua ni kwamba Chadema tulishinda nafasi zote tulizokuwa tukigombea kuanzia Mwenyekiti,Vitongoji mpaka viti maalum..!! Na hili ndilo lililonipa faraja siyo wale walioshinda..!!! Kwahiyo yeyote atakayenihusisha na ACT utaona ni kiasi gani ananivunjia heshima, na hili nitakabiliana nalo kwa nguvu zote...
Twende sasa....
1.Mpaka sasa naweza kusema Zitto hana madhara yoyote kwa UKAWA kile alichokishindwa akiwa Chadema hawezi kufanikiwa akiwa UKAWA. Zitto kwa hivi sasa anaihitaji sana UKAWA ili aendelee kuaminika kwa wananchi. Jamno lolote atakalolifanya kwa muktadha wa kuichafua au kuipalanganya UKAWA itakuwa na madhara kwake, hapa wananchi wote watajua wazi kwamba Zitto ndiye mwenye tatizo pindi ikitokea sintofahamu kama ilivyotokea akiwa Cdm. Yaani ukitokea ugomvi wowote ndani ya UKAWA wenye kumuhusisha Zitto hilo ndilo litakauwa kaburi rasmi la kisiasa kwa Zitto hapa Tanzania, hakuna mwananchi yeyote atakaye.mwamini Zitto kwamba labda anasingiziwa kwa lolote litakalobinika kipindi hicho. Hapa mkuu tambua kwamba wapo mashabiki wa Zitto wanaoamini kwamba Zitto alionewa mpaka kuondoka kwake pale Cdm. Na hii ndiyo nyota anayosafiria Zitto kwasasa.
Kama kunahasira aliyoionyesha Zitto hadharani ni kuwaita UKAWA wasakatonge na maneno mengine kama haya. Hakuna hasira wala rungu la Zitto liakalokuwa na madhara kwa UKAWA lisilomdhuru yeye mwenyewe. Kama kunakipidi chenye umuhimu kwa UKAWA kumuingiza Zitto (Endapo ataomba) ni sasa kwasababu tunaelekea kwenye Uchaguzi mkuu. Baada ya hapo hakutakuwa na umuhimu wowote wa Zitto kuwamo ndani ya UKAWA. Hebu niambie kuna umuhimu gani wa vya vinavyounda CORD pale Kenya baada ya uchaguzi? Hili la UKAWA kutafuta njia ya kuwawin mashabiki wa Zitto kwa mimi binafsi siioni isipokuwa kumuingiza Zitto ndani ya UKAWA. Wapo watu walioapa kufa na Zitto,kuumwa na Zitto na hata kuzikwa na Zitto kisiasa na ni wengi tu kiasi kura zao ni muhimu kuelekea uchaguzi mkuu. Hapa ndip ulipo umuhimu wa Zitto kukubaliwa endapo ataomba kujiunga na umoja huo. Labda kwa mawazo yako mkuu tunaweza kutumia njia gani kuwawin mashabiki wa Zitto?
2.Mkuu hakuna propaganda yoyote yenye madhara kwa UKAWA itakayopigwa na ccm ili kuidhoofisha UKAWA pindi Zitto akijiunga. Kama ingekuwepo basi Ccm wangeishaitumia mpaka sasa kwa Nccr na Cuf ambao wamewahi kutofautiana na Cdm hadharani lakini kiko wapi? Mpaka sasa Cdm,Cuf,Nccr wanakaa meza moja kuplan namna ya kuwaondoa Ccm madarakani, huu ni ushindi mkubwa na hizi ndizo akili kubwa za watu wazima tunazizihitaji. watu tumechoshwa na ccm hatuitaki tena, Hivi kwa propaganda mbaya kama za ugaidi iliyopigwa Chadema ikiambatana na ushahidi wa hapa na pale ulitegemea kwamba yaweza kutupiliwa mbali na wananchi? Kuhusu Mashabiki Die hard wa UKAWA kuuchukuliaje ujio wa Zitto ndani ya UKAWA, naomba nikuondoe shaka Nyingi zinazoendeshwa hapa ni propaganda tu ambazo kwa udhaifu wa kuzijibu ndiomaana unaona kama itakuwa ngumu kwa mashabiki hao kukubaliana na Zitto pindi atakaporubusiwa ndani ya umoja huo.
Hivi unadhani mchango wa Zitto hautakiwi kiasi hicho ndani ya siasa za upinzani? Hebu angalia watu walivyoungana pamoja ktk sakata la Escrow bila kujari tofauti zilizokuwapo, na tunaambiwa Mpaka Zitto alialikwa kwa mara ya kwanza ndani ya kamati ya UKAWA. Je mashabiki na madie hard wa Ukawa walichukua hatua gani? Ondoa shaka mkuu ktk siasa kwa watu wanaoijua vizuri siasa hakuna adui wala rafiki wa kudumu kikubwa ni kuitumia fursa kadiri inavyopatikana.
Nikija kwenye hitimisho lako mkuu, mimi naweza kusema kwamba sikubaliani na wewe. Mimi naona UKAWA wamkubalie Zitto endapo kweli ataomba kujiunga ndani ya UKAWA. HII NI KWASABABU YA UMUHIMU MKUBWA WA UCHAGUZI HUU UNAOKUJA. Unajua mpaka sasa Act hawaeleweki vizuri, lakini utakapofika uchuguzi ndipo madhara ya hawa mabwana ijapokuwa hayatakuwa makubwa, lakini maumivu ni maumivu tu yawe ya ngumi, rungu au kuchanwa na wembe. Hawa jamaa ni Domo la Mamba lilotegeshwa Ziwani, hawa watawapokea wagombea wote wa UKAWA na ccm watakaotemwa na vyama vyao. Hebu chukulia mfano mdogo tu kama jimbo la Kyela tunaambiwa watiania wa ubunge wako zaidi ya Therathini, hawa wote wanang'ang'ania nafasi moja, hivi unadhani hawa wotewakishindwa kwenye kura za maoni watakubali tu na kurudisha nya majeshi? Hapa ndipo lile domo lililotegeshwa litafungiliwa na kuchukua hawa, iwe kwa kujishawishi au kushawishiwa na ccm ili kugawa kura za upinzani. kwa mimi binafsi kama kuna madhara ninayoyaona hapa ni haya.
Na kama hali ikiwa hivyo then hapo mwakani hatutakuwa tukiangalia "makovu" ya vidonda, bali tutakuwa tukiuguza vidonda vibichi kabisa..!! Na muda wa kuwahusisha hawa hatutakuwa nao tena. Wala hakuna atakayekuwa akitamani tena siasa za umoja wa vyama.
Tafakari.
BACK TANGANYIKA