ACT - Wazalendo waomba kujiunga na UKAWA

ACT - Wazalendo waomba kujiunga na UKAWA

Mwenye nia njema ni yupi, zito? Ukawa wajiloge wamkaribishe waone! mbinu za ccm ni nyingi sana, wakifanikiwa hili la kumpenyeza zitto Ukawa watakuwa wamemaliza kazi kabisaaa.

Inaonekana wanataka kuyamaliza kimya kimya, wanajua kabisa dogo mziki wake mnene, naona mazungumzo ya M23 yanaanza, wakichomoa kichapo kinaanza moja. Ule mkutano wa juzi kukosekana slaa mnyika na lisu ni dalili za kuwepo majadiliano.
 
Sharti la kwanza> arudishe msaada kutoka kwa marafiki wa ndani
 
Apewe Mashart Nani Aya,tolah! Hakilibishwi Mtu Hapa, Kwanini Asijiunge Na Mrema, Ukawa Ina Tuvyama Tu 4 Tu Bado Kuna Mavyama Kibao, Kwanini Asijiunge Navyo? Tena Mmwambie, Aludi Kwa Waliomtuma Akawaambie Pale Hapaingiliki.
 
Tatizo chadema wamejimilikisha ukawa, wanafikiri ukawa sawa taasisi yao ambayo mbowe akiongea akimaliza anauliza hoja hii inaungwa mkono waliobaki wote lazima waitikie ndiyooooooooooooooooooooo

Juzi nilimwona mbatia kila anachoongea mbowe kanachekelea, nadhani anadandia nafasi za viti maalum, manake Vunjo Lyatonga kakomaa.
 
ACT waliambiwa wapeleke maombi kujiunga na UKAWA. hawajafanya hivyo.hawana nia ya kujinga. 'Wasisemewe'.
 
Nia yake inafahamika kuwa kazi aliyotumwa na wahafidhina wa upinzani hakuikamilisha sasa anataka kuikamilisha kwa kuua UKAWA hakuna mwenye akili timamu atakayekubali kujiunga na msaliti yuda Iskarioti.
 
ACT-Wazalendo ndio kiboko yenu BAVICHA.
Mshaambiwa mkasajili Chama kimpya ACT-Wazalendo maana kwa Msajili kule kunasomeka ACT - Tanzania.... mtakuja kula ya chuya October... do something before too late
 
ACT ni chama. Zitto ni mtu kwa nini Ukawa iwe kama ni umoja wa biashara haramu wakati hata ACT lengo lake ni kumwondoa mkoloni Ccm.

ACT wakiomba wapewe masharti ya jumla although kwa Ukawa walipofikia kimakubaliano no window for (not mention a door) ACT

Kwa ujumla wenu mnaonekana watu wenye mioyo safi kumbe ndani yenu mna vitu mmefichama ili kukifanya kwa manufaa ya hao mabwana zenu....ila mkumbuke kuwa mchawi huwa anaroga uck af anajulikana juu ya yote anayoyafanya itakuwa huyu zitto?
 
ACT ni chama ambacho kimejipambanua vzr kufanya kazi ya siasa kuliko vyama vingine vya upinzani. malengo ya wazee wa UKAWA hayaeleweki mara katiba mara uchaguzi mkuu.
 
act ni chama ambacho kimejipambanua vzr kufanya kazi ya siasa kuliko vyama vingine vya upinzani. Malengo ya wazee wa ukawa hayaeleweki mara katiba mara uchaguzi mkuu.

wakati mwingine kukaa kimya ni busara.
Sasa huu utumbo huu nawe umeona ndio .......m.nn
 
Ccm kwa ukawa ni chama pinzani,act wazalendo wanatakiwa kujiunga na ccm
 
Huyu jamaa ana nia njema na nchi hii toka roho yake imeumbwa ila wajinga wachache wanataka kuizima nuru yake kwa maslahi yao binafsi.
Kiongozi usijidanganye. Zitto alipokuwa CDM hakuwa muumini wa UKAWA. Leo yupo ACT kapata wap imani na UKAWA?Nahisi ametumwa kutuvuruga
 
sasa huyu mnafiki zuber alisema UKAWA nia yao kugawana vyeo yeye tena anataka kujiunga na umoja wa wasaka vyeo kweli mnafiki anajivua ngua aende ccm kama ndugu yake kaborou W.

Labda kwa vile na yeye ameshapata cheo kikubwa kuliko vyote walivyonavyo wengine..
Yaani haka kabwanamdogo zzk kimdomo chake tu kinaonesha kalivo kanafiki
 
hahaa zitto hamtamuweza kwakuwa nyie mnapambana naye kwa kutumia manguvu na propaganda za uongo yeye anatumia akili za kuzaliwa na za darasani. zitto will remain mzito
 
Kwa mujibu wa habari iliyochapishwa na gazeti la Mwananchi ni kuwa Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo Anna Mgwira amesema chama hicho hakina matatizo na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na hata sasa kinasubiri majibu ya barua yao waliyoituma kwa umoja huo kuomba kuunganishwa.

Mgwira alitoa kauli hiyo wakati chama hicho kilipofanya ziara ya kutembelea hospitali ya mkoa ya Mt Meru kugawa zawadi mbalimbali katika wodi ya kinamama ikiwa ni njia ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake.

Alisema ACT-Wazalendo wanaunga mkono muungano wowote wa vyama vya upinzani nchini ulio halali.

“Hatuna matatizo na Ukawa tunaunga mkono muungano wowote wa upinzani ulio halali,” alisema kiongozi huyo

Alisema tangu waandike barua ya kuomba mwongozo wa namna ya kujiunga na Ukawa, bado hawajapata mrejesho.

“Tunatamani kuunganisha nguvu katika siasa za vyama vya upinzani na sasa tunasubiri majibu ya barua yetu ya kuomba kuingia Ukawa,” alisema.

Alisema kuwa chama hicho kimepokewa vizuri na wananchi wa mikoa mbalimbali nchini na katika ziara ya awamu ya kwanza walifanikiwa kuingiza jumla ya wanachama wapya 700.

“Tumepokewa vizuri mikoani tumefanikiwa kuingiza wanachama wapya na hoja ya umoja na uzalendo watu wameipokea vizuri,” alisisitiza Mgwira.

Akipokea misaada katika hospitali hiyo Muuguzi Mfawidhi, Sifael Masawe alisema kwamba misaada hiyo itasaidia kupunguza shida za wagonjwa waliofika hospitalini hapo na kuwataka wengine kujitokeza kuwaunga mkono

Chanzo: Habari247

MYTAKE:
1) yaani mbwembwe zote zile za zitto na wenzake kuzunguka nchi nzima wameambulia wanachama 700 tu??? hata kura za kata moja hawajafikisha?? huu sasa utani....ndio maana zzk amekata tamaa na ziara ya pili???

2) Kwani kiongozi Mkuu zitto sialisema Ukawa ni wasakatonge??? na yeye anataka kujiunga na wasakatonge ???

3) Huyu mama sialisema "Nimarufuku Mwana Act kushabikia Ukawa"???

.....................
Professor kilaza.
 
Back
Top Bottom