ACT - Wazalendo waomba kujiunga na UKAWA

ZZK alikosea kukata tawi analojua atajishikilia, yaani alishany.ea chakula pekee alichokuwa nacho hivyo akubali tu matokea ya utukutu wake
 
Kuna watu wanashindwa kutoa maoni yao chanya kisiasa hapa jukwaani kwa kuogopa kutukanwa ama kuitwa Ndumilakuwili.

Ngoja niseme kidogo, kama nitamkwaza somebody then It's my Opinion.!

Watu wazima hukaa chini na kuzungumza, Ni mazungumzo Makini hayo ndiyo yaliyotuweka hapa Wanaukawa tukijadiri namna ya kumuondoa ccm madarakani. Kwa hali ya kisiasa ilivyokuwa hapo mwanzo, hakuna aliyewahi kudhani itakuwapo siku Cdm watakaa chini na Cuf kupanga mikakati mbalimbali ya ushirikiano ili kumwondoa ccm. Iko hivyo kwa Nccr dhidi ya Cdm Na hata NLD ambacho ni chama kidogo sana kisiasa dhidi ya Chama kikubwa kikuu cha upinzani Bungeni na Nchini kwa ujumla Chadema. Kilichofanyika hapa ni umakini wa watu wazima kuzika tofauti zao na kuangalia Malengo na Vipaumbele vyao. Wakajikuta wote kipaumbele na Malengo yao ni mamoja, kumuondoa mtu/chama kimoja kilichoshindwa kuongoza na kuendelea kung'ang'ania kutawala. Kwa kweli ni Mazungumzo Makini toka kwa Watu Makini dhidi ya Malengo Makini, ndiyo yaliyo yifikisha hapa. Na hiki ndicho tunachokihitaji kwa wakati huu.

Kama ni kweli hili limefanyika kwa ACT kutuma Maombi ya kujiunga UKAWA, ni vyema maombi yao yakatathiminiwa na hatimaye kukubaliwa. Katika kipindi hiki ni wazi UKAWA hawatakiwi kukosa hata kura moja, iwe ya Urais,Ubunge au Udiwani. Ni wakati wa kuzileta kura za Wapinzani wote dhidi watawala. Ni wakati tunaohitaji nguvu za uhakika na zile za ziada hata zile ambazo hatuna ili kuhakikisha kweli Ccm inaondoka madarakani kama kweli tuna nia ya dhati kumuondoa huyu Mkoloni mweusi.

Kwa hapa ilipo UKAWA, hakuna siri ambazo kwa hakika zikijulikana na ccm zitaweza kuleta madhala kwa umoja huo kiasi tuogope kuwaingiza ACT kwa hofu ya kuuza siri za Umoja huo kwa Ccm. Mpaka sasa hakuna propaganda yoyote itakayofanikiwa kuwatenganisha UKAWA itakayokubalika kwa wananchi. UKAWA mpaka sasa inawapiga kura wengi ambao hawako tayari kubadirishwa kwa lolote, hawa wanaitwa wafia chama. (UKAWA) Kinachofanyika hapa ni kuwashawishi wale ambao hawana misimamo rasmi na wale ambao ni Die hard Ccm. Wapo wale ambao ni die hard Zitto ambao licha ya uchache wao, kura zao ni muhimu sana. Mtu hata kama ulikuwa na Bilioni moja mtu akaja kukuongezea Milliom moja, pesa zako zitakuwa zimeongezeka kiasi cha kukuhakikishia maisha kwa siku kadhaa kulingana na maisha unayoishi.

Kwahiyo wakuu tusiwe na Misimamo mikali, isiyoyumba kwani mara kadhaa huwa haina faida. Kama hawa jamaa wamejitambua na kuomba kujiunga waruhusiwe na kupimwa nguvu zao ikiwezakana wapewe kulingana na nguvu zao hasa ukizingatia wamechelewa kujiunga. Iko wazi, mtu ukitokea somewhere na kukuta watu wanakula na ukakaribishwa chakula, utakula kulingana na pale ulipokikuta chakula hicho. Hapa pia Cdm,Cuf,Nccr na Nld wawe tayari kupunguza matonge kwaajili ya mgeni aliyefika.

Nirudie tena hii ni kama kweli ACT wametuma maombi hayo, maana awali walidai kutuma maombi, ilhali viongozi wa UKAWA wakidai hawajapokea maombi toka kikundi chochote cha siasa. Hapa ilionekana kama ni ACT kujaribu kununua huruma kwa wananchi kwa kigezo cha kukataliwa na Viongozi wenzao toka UKAWA.

Ni hayo tu wadau.

BACK TANGANYIKA

HAKUNA KUPOKEA WASALITI! Mmeona UKAWA inazidi kunawiri na mbinu zote za kuivunja zimeshindikana sasa ndio mnataka kujipenyeza ili ukifika wakati wa uchaguzi muuze majimbo na kufanya usaliti wa kila aina kama mlivyozoea! Mlikuwa mnajiona wenye akili na kupewa kichwa na CCM mlipokuwa ndani ya upizanzani sasa mmetoka hamthaminiwi tena wala hamsaidiwi tena ndio manataka kuja na mbinu ya kijinga mkifikiria watanzania wote wana akili fupi kama nyinyi! Mmegonga mwamba na mtaula wa chuya!
 
Alisema kuwa chama hicho kimepokewa
vizuri na wananchi wa mikoa mbalimbali
nchini na katika ziara ya awamu ya
kwanza walifanikiwa kuingiza jumla ya
wanachama wapya 700. yaan hii ni idadi ya wanachadema kijiji cha kibumbe na Ilundo tu Kata ya Kiwira. tukuyu

Yani hata mimi nimeshangaa sana,
Yani wanachama 700?
Namshauri Mwl. Kaijage afungue walau kijiwe cha kufundisha tuition.
 
Last edited by a moderator:
HAKUNA KUPOKEA WASALITI! Mmeona UKAWA inazidi kunawiri na mbinu zote za kuivunja zimeshindikana sasa ndio mnataka kujipenyeza ili ukifika wakati wa uchaguzi muuze majimbo na kufanya usaliti wa kila aina kama mlivyozoea! Mlikuwa mnajiona wenye akili na kupewa kichwa na CCM mlipokuwa ndani ya upizanzani sasa mmetoka hamthaminiwi tena wala hamsaidiwi tena ndio manataka kuja na mbinu ya kijinga mkifikiria watanzania wote wana akili fupi kama nyinyi! Mmegonga mwamba na mtaula wa chuya!

Mkuu habari,

Hii hoja unamwelekezea nani? Mwanachama wa ACT siyo? Ila kwa bahati mbaya umeniquote mimi..!! Wenzako kabla ya kupanua mdomo na mbavu, hupanua kwanza akili. Na kama ungelijaaliwa akili kidogo tu kiasi cha kujaza kizibo cha soda, ungefuatilia michango yangu hapa Jukwaani na hapa ungekuwa unapanua mbavu na kinywa kwa amani kabisa..!!!! Pole kwa hilo

Hivi umepata wasaa wa kusoma nilichokiandika? We ni kupakachuka tu utafikiri Mipakacha ya kule Lindi, au umetokokea huko? Tuliza akili, kama unataka kuwa mchambuzi bora hapa tuliza mshono, kaa chini tafakari wenzako wanajengaje hoja, Wanahitimishaje na kuwasilishaje. Siyo kuropoka tu utafikiri umekula Mlenda usio na bamia wala Magadi kule Hanseketwa..!!!!

Tuliza mshono jenga hoja usikike.

Hivi nikikuuliza kwa hivi sasa UKAWA ni jambo gani litakalofahamika kwa ccm litavunja nguvu za umoja huo kuelekea uchaguzi mkuu utanijibu? Hivi wewe hapo propaganda gani ambayo kwa fikra zako yaweza kuugawanya na kuusambaratisha UKAWA? Kama ccm walishindwa kwa propaganda mbaya za Udini, Ukanda, Ukabila na Ugaidi lipi laweza kuwashawishi wananchi wakubaliane na Ccm na serikali yake chovu dhidi ya UKAWA?

Narudia, Jenga hoja usikwaze watu.

BACK TANGANYIKA
 
UKAWA are smart to know kwamba ACT hawastahili kuwepo kwenye coalition yao

KUna kauli ya kiongozi wao mkuu ilitoka kwamba UKAWA wanagawana majimbo na hawana nia ya kweli ya kuwakomboa Tz... sasa imekuaje na yeye ajoin watu wasiowakilisha mawazo na nia yake??

Please say no to ACT kujiunga na UKAWA
 
chanzo: Habari247

mytake:
1) yaani mbwembwe zote zile za zitto na wenzake kuzunguka nchi nzima wameambulia wanachama 700 tu??? Hata kura za kata moja hawajafikisha?? Huu sasa utani....ndio maana zzk amekata tamaa na ziara ya pili???

2) kwani kiongozi mkuu zitto sialisema ukawa ni wasakatonge??? Na yeye anataka kujiunga na wasakatonge ???

3) huyu mama sialisema "nimarufuku mwana act kushabikia ukawa"???

.....................
Professor kilaza.
hawafai hawa wanafik wa demokrasia na mabadiliko ya kweli#
 
.... Si Mulisema Ukawa Ni Wasaka Tonge, Mnataka Nini Tena Kama Hamjatumwa Na Mabwana Zenu Ccm Kuja Kuvuruga Mambo
 
Hivi zzk anaweza kuungana na wasaka tonge??? Nitamdhalau sana aisee ukawa ni wasaka tonge maneno ya zzk sasa jamaa kawaje tena hadi aungane na hawa jamaa aisee zzk is political dead
 
Yani hata mimi nimeshangaa sana,
Yani wanachama 700?
Namshauri Mwl. Kaijage afungue walau kijiwe cha kufundisha tuition.
Kama wamezunguka nchi nzima wameambulia 700 watuambie awali walikuwa na wanachama wangapi!!? Pole sana ZITO, sisi wengine tuliuona mwisho wako lakini wapambe wakakuponza! Hivi kwanini usijiunge na wenzako TLP, UDP na ADC?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu habari,

Hii hoja unamwelekezea nani? Mwanachama wa ACT siyo? Ila kwa bahati mbaya umeniquote mimi..!! Wenzako kabla ya kupanua mdomo na mbavu, hupanua kwanza akili. Na kama ungelijaaliwa akili kidogo tu kiasi cha kujaza kizibo cha soda, ungefuatilia michango yangu hapa Jukwaani na hapa ungekuwa unapanua mbavu na kinywa kwa amani kabisa..!!!! Pole kwa hilo

Hivi umepata wasaa wa kusoma nilichokiandika? We ni kupakachuka tu utafikiri Mipakacha ya kule Lindi, au umetokokea huko? Tuliza akili, kama unataka kuwa mchambuzi bora hapa tuliza mshono, kaa chini tafakari wenzako wanajengaje hoja, Wanahitimishaje na kuwasilishaje. Siyo kuropoka tu utafikiri umekula Mlenda usio na bamia wala Magadi kule Hanseketwa..!!!!

Tuliza mshono jenga hoja usikike.

Hivi nikikuuliza kwa hivi sasa UKAWA ni jambo gani litakalofahamika kwa ccm litavunja nguvu za umoja huo kuelekea uchaguzi mkuu utanijibu? Hivi wewe hapo propaganda gani ambayo kwa fikra zako yaweza kuugawanya na kuusambaratisha UKAWA? Kama ccm walishindwa kwa propaganda mbaya za Udini, Ukanda, Ukabila na Ugaidi lipi laweza kuwashawishi wananchi wakubaliane na Ccm na serikali yake chovu dhidi ya UKAWA?

Narudia, Jenga hoja usikwaze watu.

BACK TANGANYIKA

Mkuu respect wa boda salam!

Nimefurahishwa na mchango wako wa kwanza kabla ya huu hapa kuhusu, umuhimu wa kuwashirikisha ACT katika UKAWA. Kwangu mimi hilo ni jambo jema sana lakini si salama hata kidogo kufanya hivyo katika kipindi hiki hasa tunapoelekea uchaguzi kwa mtazo huu;
1. Kwa muda mfupi tangu Kiongozi wa chama aondolewe kwa katiba ya chama chake cha zamani, hajaonesha rangi yake halisi kwa uchungu wa kuodolewa katika chama ambacho kwa dhati ya moyo wake alihusika pia kukifikisha hapo kilipo. BADO ANAHASIRA kumuingiza katika kundi akiwa na uhuru mpana kama kiongoz wa chama mshirika wa UKAWA ni sawa na kumpa rungu kumalizia kazi aliyoianza mapema. Ndio anaumuhimu ktk kundi lakini sio sasa. UKAWA watafute njia mbadala ya kuwawin mashabiki na wakereketwa wao lakini si kwa njia uliyopendekeza.

2.Je umejaribu kufikiria chama tawala kitaendesha kampeni gani za kuipunguzia UKAWA wabigakura iwapo jamaa atarudishwa kundini? Je vp kwa watu waliojitolea (dyinhard) wa ukawa watachukulia vp kurudi kwa kiongozi wa chama katika kundi?

Kiufupi nadhani wanaukawa wampe muda kiongozi wa chama huko aliko aweze kupractiz kile anachokiamini kwa muda walau wa miaka miwili ndipo wamrudishe wakati vidonda vya ndg zake wa ukawa vikiwa vimepona.
 
Last edited by a moderator:
Wanachama 700 ni wachache sana kulinganisha na wanachama wa misingi miwili ya chadema, kwani kwenye msingi nilipo kuna wanachama 508
 
Hivi zzk anaweza kuungana na wasaka tonge??? Nitamdhalau sana aisee ukawa ni wasaka tonge maneno ya zzk sasa jamaa kawaje tena hadi aungane na hawa jamaa aisee zzk is political dead

Inawezekana kabisa..mbona chadema kaungana na chama cha mashoga(cuf).
 
Mi nawashangaa sana nyie,hivi Ukawa inawahusu kweli nyie wanachama au inawahusu wenyewe tu viongozi wake?
 
Kuna watu wanashindwa kutoa maoni yao chanya kisiasa hapa jukwaani kwa kuogopa kutukanwa ama kuitwa Ndumilakuwili.

Ngoja niseme kidogo, kama nitamkwaza somebody then It's my Opinion.!

Watu wazima hukaa chini na kuzungumza, Ni mazungumzo Makini hayo ndiyo yaliyotuweka hapa Wanaukawa tukijadiri namna ya kumuondoa ccm madarakani. Kwa hali ya kisiasa ilivyokuwa hapo mwanzo, hakuna aliyewahi kudhani itakuwapo siku Cdm watakaa chini na Cuf kupanga mikakati mbalimbali ya ushirikiano ili kumwondoa ccm. Iko hivyo kwa Nccr dhidi ya Cdm Na hata NLD ambacho ni chama kidogo sana kisiasa dhidi ya Chama kikubwa kikuu cha upinzani Bungeni na Nchini kwa ujumla Chadema. Kilichofanyika hapa ni umakini wa watu wazima kuzika tofauti zao na kuangalia Malengo na Vipaumbele vyao. Wakajikuta wote kipaumbele na Malengo yao ni mamoja, kumuondoa mtu/chama kimoja kilichoshindwa kuongoza na kuendelea kung'ang'ania kutawala. Kwa kweli ni Mazungumzo Makini toka kwa Watu Makini dhidi ya Malengo Makini, ndiyo yaliyo yifikisha hapa. Na hiki ndicho tunachokihitaji kwa wakati huu.

Kama ni kweli hili limefanyika kwa ACT kutuma Maombi ya kujiunga UKAWA, ni vyema maombi yao yakatathiminiwa na hatimaye kukubaliwa. Katika kipindi hiki ni wazi UKAWA hawatakiwi kukosa hata kura moja, iwe ya Urais,Ubunge au Udiwani. Ni wakati wa kuzileta kura za Wapinzani wote dhidi watawala. Ni wakati tunaohitaji nguvu za uhakika na zile za ziada hata zile ambazo hatuna ili kuhakikisha kweli Ccm inaondoka madarakani kama kweli tuna nia ya dhati kumuondoa huyu Mkoloni mweusi.

Kwa hapa ilipo UKAWA, hakuna siri ambazo kwa hakika zikijulikana na ccm zitaweza kuleta madhala kwa umoja huo kiasi tuogope kuwaingiza ACT kwa hofu ya kuuza siri za Umoja huo kwa Ccm. Mpaka sasa hakuna propaganda yoyote itakayofanikiwa kuwatenganisha UKAWA itakayokubalika kwa wananchi. UKAWA mpaka sasa inawapiga kura wengi ambao hawako tayari kubadirishwa kwa lolote, hawa wanaitwa wafia chama. (UKAWA) Kinachofanyika hapa ni kuwashawishi wale ambao hawana misimamo rasmi na wale ambao ni Die hard Ccm. Wapo wale ambao ni die hard Zitto ambao licha ya uchache wao, kura zao ni muhimu sana. Mtu hata kama ulikuwa na Bilioni moja mtu akaja kukuongezea Milliom moja, pesa zako zitakuwa zimeongezeka kiasi cha kukuhakikishia maisha kwa siku kadhaa kulingana na maisha unayoishi.

Kwahiyo wakuu tusiwe na Misimamo mikali, isiyoyumba kwani mara kadhaa huwa haina faida. Kama hawa jamaa wamejitambua na kuomba kujiunga waruhusiwe na kupimwa nguvu zao ikiwezakana wapewe kulingana na nguvu zao hasa ukizingatia wamechelewa kujiunga. Iko wazi, mtu ukitokea somewhere na kukuta watu wanakula na ukakaribishwa chakula, utakula kulingana na pale ulipokikuta chakula hicho. Hapa pia Cdm,Cuf,Nccr na Nld wawe tayari kupunguza matonge kwaajili ya mgeni aliyefika.

Nirudie tena hii ni kama kweli ACT wametuma maombi hayo, maana awali walidai kutuma maombi, ilhali viongozi wa UKAWA wakidai hawajapokea maombi toka kikundi chochote cha siasa. Hapa ilionekana kama ni ACT kujaribu kununua huruma kwa wananchi kwa kigezo cha kukataliwa na Viongozi wenzao toka UKAWA.

Ni hayo tu wadau.

BACK TANGANYIKA

Kwa nini wana CCM nao wanaonekana kuwa na interest ya kuona Zitto anaingia UKAWA?
 
Back
Top Bottom