ACT - Wazalendo waomba kujiunga na UKAWA

ACT - Wazalendo waomba kujiunga na UKAWA

Ahsante sana Mkuu. Chama kiko ICU hiki sasa wanatafuta uhai kupitia UKAWA. Walijiona wao ndio wao na yule mama kupiga marufuku wanachama wao kuunga mkono UKAWA, sasa imekula kwao, wanahaha huku na kule UKAWA sasa wamekuwa wema/wazuri.

Bwana we BANIANI MBAYA KIATU CHAKE DAWA..................
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Halafu hata aibu hawana! Sasa wanajibaraguza eti wanamshangaa Mbowe na msimamo wake kuhusu ombi lao! Unafiki wa hawa jamaa umepitiliza.

Bwana we BANIANI MBAYA KIATU CHAKE DAWA..................
 
Amma kwa hakika sijapata kuona watu ambao wana muono mfupi zaidi ya bavichaa.

Wanakifanya 'exactly" kile ambacho ACT wamekitarajia kwa kuandika hiyo barua.

Hiyo barua imewakuza ghafala ACT na kuwa "on the par" na vyama vya zamani vinavyfanya umoja wa UKAWA.

Hii ni mbinu nzuri sana ya kisiasa walioitumia na aliyeifikiria hiyo mbinu huko ACT, kama ni yule mama, basi ana kichwa kizuri sana na nnampa pongezi za dhati.

Bavichaa mnapigwa mabao kutumia nguvu zenu wenyewe na kichama kiduuuchu. Amma kwa hakika hii inazidi kuyakinisha kuwa chadema kwa sasa inaongozwa na akili ndogo.

Yaani wewe tunaomba Maulana akusamehe kwa maana hujui ulitendalo, empty head
 
Halafu hata aibu hawana! Sasa wanajibaraguza eti wanamshangaa Mbowe na msimamo wake kuhusu ombi lao! Unafiki wa hawa jamaa umepitiliza.

Tatizo mdogo wangu Zitto hatojifunza kamwe.Inabidi watu wazima wamwambie asijione yeye ni bora kuliko wengine.Kwenye masuala ya siasa watu huwa wanashirikiana kwa matokeo mazuri.Nilijua toka mwanzo kuwa Zitto anawahitaji zaidi Ukawa kuliko anavyofikiria.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Tatizo huyu njemba haambiliki, yeye ndiyo yeye hasikii la mtoa adhana wala la shetani na hili linamgharimu sana kwenye maisha yake kama mwanasiasa na si ajabu katika maisha yake ya kila siku kama binadamu. Sijui kama huwa anakaa chini na kutafakari kwa kina maamuzi yake na kauli zake zinaweza kuja kuwa na athari zipi kwake katika siku za usoni kabla ya kukurupuka. Msome Prof Baregu hapa chini:

PROFESA Mwesiga Baregu, mmoja wa watu wanaoheshimika nchini amesema, aliyepata kuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, anaponzwa na kiburi cha kujiona hakuna zaidi ya yeye. Anandika Saed Kubenea … (endelea).

Amesema, Zitto ambaye alikuwa naibu katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tanzania Bara na naibu kiongozi wa upinzani bungeni, anafanya kazi asiyoifahamu na ambayo haina mavuno.

❝
"Ninamfahamu vizuri. Wakati tuhuma hizi za usaliti zilipoanza kuibuka, Kamati Kuu ilinikabidhi jukumu la kumsaidia mama yake mzazi kumlea kijana huyu."

Kauli ya Baregu ilitolewa siku moja baada ya Zitto kujiondoa bungeni na baadaye kujiunga na Chama cha ACT – Tanzania.

Prof. Baregu aliwahi kuwa "mlezi wa Zitto" ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Alikabidhiwa jukumu hilo na Shida Salum, mama mzazi wa Zitto (marehemu), baada ya mama huyo kuiomba Kamati Kuu (CC) ya chama hicho "kusaidia kumlea."

Prof. Baregu ambaye ni mjumbe wa kamati kuu ya Chadema anasema, "Zitto hamnazo. Amekuwa anajiona yeye ni zaidi ya chama. Hashauriki."

Anasema wakati ule alipopewa kazi ya kumlea Zitto "katikakati ya migogoro, tulikuwa tunazungumza naye mara kwa mara. Ninamfahamu. Kazi hii ya kumlea tulikabidhiwa mimi na mama yake mzazi, Bi. Shida Salum," anaeleza Baregu.

Mama mzazi wa Zitto, alifariki dunia Juni mwaka jana, baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Kauli ya Prof. Baregu ilifuatia gazeti hili kutaka maoni yake juu ya mustakabali wa kisiasa wa Zitto baada ya kuwahi kujiondoa ndani ya Chadema.

Tatizo mdogo wangu Zitto hatojifunza kamwe. Inabidi watu wazima wamwambie asijione yeye ni bora kuliko wengine. Kwenye masuala ya siasa watu huwa wanashirikiana kwa matokeo mazuri. Nilijua toka mwanzo kuwa Zitto anawahitaji zaidi Ukawa kuliko anavyofikiria.
 
Yaani wewe tunaomba Maulana akusamehe kwa maana hujui ulitendalo, empty head

Nisome vizuri sana hiyo post yangu, nnakusikitikia sana kuwa hujaiona mantiki ya ACT kutuma ile barua, sikulaumu kwani nnajuwa upeo wako na waliokurupuka kuwashutumu ACT ni mmoja, na ni mfupi sana.

Mimi nnasema ACT ni wajanja sana kisiasa na hapo wanaendelea kupata free ride ya media na publicity ya kila aina kwa barua moja tu, ambayo nnauhakika wangekubaliwa ingewaumiza zaidi na walijuwa hilo na nnadhani walipoipeleka walikuwa wanaomba ikataliwe.

Sasa hivi kijichama kiduchu ambacho kipo kwenye kutambaa kipo on the par kwenye "publicity stunt" na jichama lililopo zaidi ya miaka 20 kwa barua moja tu. Fikiri.
 
Tatizo mdogo wangu Zitto hatojifunza kamwe.Inabidi watu wazima wamwambie asijione yeye ni bora kuliko wengine.Kwenye masualua ya siasa watu huwa wanashirikiana kwa matokeo mazuri.Nilijua toka mwanzo kuwa Zitto anawahitaji zaidi Ukawa kuliko anavyofikiria.

Ndugu zangu lazima kuwa makini. ACT wawao nia yao tangu mwanzo ni kuvuruga. Walipofanya mikutano wananchi walikuwa wanawauliza kwa nini msijiunge na Ukawa? Hilo likawa swali gumu kwa Zitto. Sasa ndio wameamua kuja na mbinu hii ya kujidai kuomba kujiunga ukawa wakijua kabisa watakataliwa ili wapate cha kujibu kwa wananchi. Hiyo kuomba kujiunga ni mtego tu. Ili wapate sababu. Tuwe makini. Na wajibiwe kwa umakini km lweli wameomba. Nia ya jawa watu kwa sasa ni kuvuruga lwa sababu wanataka kukomoa waliowafukuza! Bado wana hasira. Wapewe mudahali ikitulia baada ya km mwala au miwili ndio wakaribishwe!
 
Nisome vizuri sana hiyo post yangu, nnakusikitikia sana kuwa hujaiona mantiki ya ACT kutuma ile barua, sikulaumu kwani nnajuwa upeo wako na waliokurupuka kuwashutumu ACT ni mmoja, na ni mfupi sana.

Mimi nnasema ACT ni wajanja sana kisiasa na hapo wanaendelea kupata free ride ya media na publicity ya kila aina kwa barua moja tu, ambayo nnauhakika wangekubaliwa ingewaumiza zaidi na walijuwa hilo na nnadhani walipoipeleka walikuwa wanaomba ikataliwe.

Sasa hivi kijichama kiduchu ambacho kipo kwenye kutambaa kipo on the par kwenye "publicity stunt" na jichama lililopo zaidi ya miaka 20 kwa barua moja tu. Fikiri.

Huyu Zito ni mvurugaji tu ndo maana wanamkatalia. Ametumwa ili wawe wanapata habari ya kinachoendelea ukawa. Naunga mkono kutomkubalia. Yeye ajenfe ACT yake watakutana mbele ya safari. Hiv sasa hivi yuko wapi? na yale makeke yake yameishia wapi?
 
Ungekuwa unafikiri japo kiduchu ungeona mantiki ya kutumwa barua.
 
wao UKAWA wanalielewa hivo. Walishasema msaliti na kwa maana hiyo kumkubalia kwa muda huu mfupi wa usaliti wake ni kula matapishi yao.
 
Nisome vizuri sana hiyo post yangu, nnakusikitikia sana kuwa hujaiona mantiki ya ACT kutuma ile barua, sikulaumu kwani nnajuwa upeo wako na waliokurupuka kuwashutumu ACT ni mmoja, na ni mfupi sana.

Mimi nnasema ACT ni wajanja sana kisiasa na hapo wanaendelea kupata free ride ya media na publicity ya kila aina kwa barua moja tu, ambayo nnauhakika wangekubaliwa ingewaumiza zaidi na walijuwa hilo na nnadhani walipoipeleka walikuwa wanaomba ikataliwe.

Sasa hivi kijichama kiduchu ambacho kipo kwenye kutambaa kipo on the par kwenye "publicity stunt" na jichama lililopo zaidi ya miaka 20 kwa barua moja tu. Fikiri.

bi kikongwe...

kwenye hili he got exactly what he expected, sasa anashangaa nini... dogo anajikosha, aliweka karata ccm, ccm wamemtosa, sasa he is confused
 
bi kikongwe...

kwenye hili he got exactly what he expected, sasa anashangaa nini... dogo anajikosha, aliweka karata ccm, ccm wamemtosa, sasa he is confused

Hana cha kushangaa anafanyiwa kazi zake za kujitangaza na hiyo barua moja tu, he is now on the par with old parties, can you imagine even a little bit?
 
Hana cha kushangaa anafanyiwa kazi zake za kujitangaza na hiyo barua moja tu, he is now on the par with old parties, can you imagine even a little bit?

wangemjibu in public na kuendeleza malumbano kama anavyojaribu kuchokoza sawa, lakini kwa sasa amedharaulika mno, kwa wewe uliyekimbia nchi hujui tu!! The boy just screwed himself
 
wangemjibu in public na kuendeleza malumbano kama anavyojaribu kuchokoza sawa, lakini kwa sasa amedharaulika mno, kwa wewe uliyekimbia nchi hujui tu!! The boy just screwed himself

Hilo ndilo analotaka na hilo ndilo exactly ndoano yake kwa wananchi, sasa hivi anaongelewa yeye tu, bila kutia lake zaidi kijibarua cha uchokozi tu.
 
Hilo ndilo analotaka na hilo ndilo exactly ndoano yake kwa wananchi, sasa hivi anaongelewa yeye tu, bila kutia lake zaidi kijibarua cha uchokozi tu.

unahangaika, sio kila anachotaka huyo kijana ndio lulu au a right thing kwake au his strategy works; he needs chadema kujipiga kick, hana song, hana rhyme hana chochote

Either way wewe ungesema ndicho anachotaka, wangekubali pia ungesema hivyohivyo, yeye ni dalali wa CCM, so I didnt expect anything new kwako au kwake

what chadema did is right, sasa hana nyimbo mpya, atahanjahanja, huku watu wakikumbushia a simple like, usaliti. He has just shot his own foot; sababu ya papara za ujana na naivety... mbaya zaidi ni corrupt mind yake inamsumbua
 
Binafsi ninapata mashaka na hawa jamaa ACT. Kwani walikuja na hoja kutoitambua UKAWA, na wakaenda mbali zaidi kwa kusema "KWA GHARAMA ZOZOTE WATAHAKIKISHA WANAYANYAKUA MAJIMBO YA KAWE, UBUNGO, UKONGA NA MAJIMBO YOTE YANAYOMILIKIWA NA CUF HUKO MAENEO YA KUSINI MWA TANZANIA"

Nashindwa kuwaelewa leo wakisema kuwa wanatamani kujibu barua yao.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!

MIZAMBWA ndiyo nini?
 
Washabiki wa siasa mnatabu sana,kabla ya ukawa hivyo vyama vilishaitana ccm B,mashoga na wengine hadi walimsaidia Kikwete ashinde. Lakini leo hii wote kwa pamoja et ndiyo wameunda ukawa,hivyo hata si ajabu pia kuona ACT wamejiunga na ukawa.

Hao unawaongelea walitukanana wakiwa 'bar' na kwenye 'vijiwe vya kahawa' lakini walikuja kumtambua adui na nguvu yao halisi wakiwa vitani na huko huko wakaunganisha nguvu.
Lakini huyo jamaa na kundi lakini yeye alitukana na kusaliti wenzake walipikuwa vitani na akaona aibu kujitambulisha kama mmoja wa wenzake......una cha kushauri hapo kiongozi?
 
Back
Top Bottom