Kuna watu wanashindwa kutoa maoni yao chanya kisiasa hapa jukwaani kwa kuogopa kutukanwa ama kuitwa Ndumilakuwili.
Ngoja niseme kidogo, kama nitamkwaza somebody then It's my Opinion.!
Watu wazima hukaa chini na kuzungumza, Ni mazungumzo Makini hayo ndiyo yaliyotuweka hapa Wanaukawa tukijadiri namna ya kumuondoa ccm madarakani. Kwa hali ya kisiasa ilivyokuwa hapo mwanzo, hakuna aliyewahi kudhani itakuwapo siku Cdm watakaa chini na Cuf kupanga mikakati mbalimbali ya ushirikiano ili kumwondoa ccm. Iko hivyo kwa Nccr dhidi ya Cdm Na hata NLD ambacho ni chama kidogo sana kisiasa dhidi ya Chama kikubwa kikuu cha upinzani Bungeni na Nchini kwa ujumla Chadema. Kilichofanyika hapa ni umakini wa watu wazima kuzika tofauti zao na kuangalia Malengo na Vipaumbele vyao. Wakajikuta wote kipaumbele na Malengo yao ni mamoja, kumuondoa mtu/chama kimoja kilichoshindwa kuongoza na kuendelea kung'ang'ania kutawala. Kwa kweli ni Mazungumzo Makini toka kwa Watu Makini dhidi ya Malengo Makini, ndiyo yaliyo yifikisha hapa. Na hiki ndicho tunachokihitaji kwa wakati huu.
Kama ni kweli hili limefanyika kwa ACT kutuma Maombi ya kujiunga UKAWA, ni vyema maombi yao yakatathiminiwa na hatimaye kukubaliwa. Katika kipindi hiki ni wazi UKAWA hawatakiwi kukosa hata kura moja, iwe ya Urais,Ubunge au Udiwani. Ni wakati wa kuzileta kura za Wapinzani wote dhidi watawala. Ni wakati tunaohitaji nguvu za uhakika na zile za ziada hata zile ambazo hatuna ili kuhakikisha kweli Ccm inaondoka madarakani kama kweli tuna nia ya dhati kumuondoa huyu Mkoloni mweusi.
Kwa hapa ilipo UKAWA, hakuna siri ambazo kwa hakika zikijulikana na ccm zitaweza kuleta madhala kwa umoja huo kiasi tuogope kuwaingiza ACT kwa hofu ya kuuza siri za Umoja huo kwa Ccm. Mpaka sasa hakuna propaganda yoyote itakayofanikiwa kuwatenganisha UKAWA itakayokubalika kwa wananchi. UKAWA mpaka sasa inawapiga kura wengi ambao hawako tayari kubadirishwa kwa lolote, hawa wanaitwa wafia chama. (UKAWA) Kinachofanyika hapa ni kuwashawishi wale ambao hawana misimamo rasmi na wale ambao ni Die hard Ccm. Wapo wale ambao ni die hard Zitto ambao licha ya uchache wao, kura zao ni muhimu sana. Mtu hata kama ulikuwa na Bilioni moja mtu akaja kukuongezea Milliom moja, pesa zako zitakuwa zimeongezeka kiasi cha kukuhakikishia maisha kwa siku kadhaa kulingana na maisha unayoishi.
Kwahiyo wakuu tusiwe na Misimamo mikali, isiyoyumba kwani mara kadhaa huwa haina faida. Kama hawa jamaa wamejitambua na kuomba kujiunga waruhusiwe na kupimwa nguvu zao ikiwezakana wapewe kulingana na nguvu zao hasa ukizingatia wamechelewa kujiunga. Iko wazi, mtu ukitokea somewhere na kukuta watu wanakula na ukakaribishwa chakula, utakula kulingana na pale ulipokikuta chakula hicho. Hapa pia Cdm,Cuf,Nccr na Nld wawe tayari kupunguza matonge kwaajili ya mgeni aliyefika.
Nirudie tena hii ni kama kweli ACT wametuma maombi hayo, maana awali walidai kutuma maombi, ilhali viongozi wa UKAWA wakidai hawajapokea maombi toka kikundi chochote cha siasa. Hapa ilionekana kama ni ACT kujaribu kununua huruma kwa wananchi kwa kigezo cha kukataliwa na Viongozi wenzao toka UKAWA.
Ni hayo tu wadau.
BACK TANGANYIKA