ACT - Wazalendo waomba kujiunga na UKAWA

Chanzo: Habari247

MYTAKE:
1) yaani mbwembwe zote zile za zitto na wenzake kuzunguka nchi nzima wameambulia wanachama 700 tu??? hata kura za kata moja hawajafikisha?? huu sasa utani....ndio maana zzk amekata tamaa na ziara ya pili???

2) Kwani kiongozi Mkuu zitto sialisema Ukawa ni wasakatonge??? na yeye anataka kujiunga na wasakatonge ???

3) Huyu mama sialisema "Nimarufuku Mwana Act kushabikia Ukawa"???

.....................
Professor kilaza.
Ufanyike muainisho hao wanachama wapya wa act wametokea chama gani, au walikuwa ni mashabiki tu wa vyama. Kama baadhi yao walitoka cuf na cdm basi kuna tatizo.
 
Mkuu Malalika, salam pia!

Nitajibu hoja zako kwa mtindo uleule wa mpangilio wake ktk kuzijenga. Na hapa wakati nikikujibu naomba ieleweke kwamba mimi ni Die hard UKAWA na CHADEMA.!! Sijui litatokea jambo gani la kuniondosha kwenye imani hii niliyonayo dhidi ya umoja huu na chama changu. Na kwa kuthibitisha hilo mkuu Malalika, mimi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa (Sikuwahi kusbiriki zaidi ya mwaka huu) nilikuwa nikipigia kura kwenye chama bila kujari ni kiongozi gani aliyekuwa akigombea kupitia chama changu. Na hapa mpaka leo simjui hata kiongozi mmoja awe mjumbe au Mwenyekiti..! Ninachojua ni kwamba Chadema tulishinda nafasi zote tulizokuwa tukigombea kuanzia Mwenyekiti,Vitongoji mpaka viti maalum..!! Na hili ndilo lililonipa faraja siyo wale walioshinda..!!! Kwahiyo yeyote atakayenihusisha na ACT utaona ni kiasi gani ananivunjia heshima, na hili nitakabiliana nalo kwa nguvu zote...

Twende sasa....

1.Mpaka sasa naweza kusema Zitto hana madhara yoyote kwa UKAWA kile alichokishindwa akiwa Chadema hawezi kufanikiwa akiwa UKAWA. Zitto kwa hivi sasa anaihitaji sana UKAWA ili aendelee kuaminika kwa wananchi. Jamno lolote atakalolifanya kwa muktadha wa kuichafua au kuipalanganya UKAWA itakuwa na madhara kwake, hapa wananchi wote watajua wazi kwamba Zitto ndiye mwenye tatizo pindi ikitokea sintofahamu kama ilivyotokea akiwa Cdm. Yaani ukitokea ugomvi wowote ndani ya UKAWA wenye kumuhusisha Zitto hilo ndilo litakauwa kaburi rasmi la kisiasa kwa Zitto hapa Tanzania, hakuna mwananchi yeyote atakaye.mwamini Zitto kwamba labda anasingiziwa kwa lolote litakalobinika kipindi hicho. Hapa mkuu tambua kwamba wapo mashabiki wa Zitto wanaoamini kwamba Zitto alionewa mpaka kuondoka kwake pale Cdm. Na hii ndiyo nyota anayosafiria Zitto kwasasa.

Kama kunahasira aliyoionyesha Zitto hadharani ni kuwaita UKAWA wasakatonge na maneno mengine kama haya. Hakuna hasira wala rungu la Zitto liakalokuwa na madhara kwa UKAWA lisilomdhuru yeye mwenyewe. Kama kunakipidi chenye umuhimu kwa UKAWA kumuingiza Zitto (Endapo ataomba) ni sasa kwasababu tunaelekea kwenye Uchaguzi mkuu. Baada ya hapo hakutakuwa na umuhimu wowote wa Zitto kuwamo ndani ya UKAWA. Hebu niambie kuna umuhimu gani wa vya vinavyounda CORD pale Kenya baada ya uchaguzi? Hili la UKAWA kutafuta njia ya kuwawin mashabiki wa Zitto kwa mimi binafsi siioni isipokuwa kumuingiza Zitto ndani ya UKAWA. Wapo watu walioapa kufa na Zitto,kuumwa na Zitto na hata kuzikwa na Zitto kisiasa na ni wengi tu kiasi kura zao ni muhimu kuelekea uchaguzi mkuu. Hapa ndip ulipo umuhimu wa Zitto kukubaliwa endapo ataomba kujiunga na umoja huo. Labda kwa mawazo yako mkuu tunaweza kutumia njia gani kuwawin mashabiki wa Zitto?

2.Mkuu hakuna propaganda yoyote yenye madhara kwa UKAWA itakayopigwa na ccm ili kuidhoofisha UKAWA pindi Zitto akijiunga. Kama ingekuwepo basi Ccm wangeishaitumia mpaka sasa kwa Nccr na Cuf ambao wamewahi kutofautiana na Cdm hadharani lakini kiko wapi? Mpaka sasa Cdm,Cuf,Nccr wanakaa meza moja kuplan namna ya kuwaondoa Ccm madarakani, huu ni ushindi mkubwa na hizi ndizo akili kubwa za watu wazima tunazizihitaji. watu tumechoshwa na ccm hatuitaki tena, Hivi kwa propaganda mbaya kama za ugaidi iliyopigwa Chadema ikiambatana na ushahidi wa hapa na pale ulitegemea kwamba yaweza kutupiliwa mbali na wananchi? Kuhusu Mashabiki Die hard wa UKAWA kuuchukuliaje ujio wa Zitto ndani ya UKAWA, naomba nikuondoe shaka Nyingi zinazoendeshwa hapa ni propaganda tu ambazo kwa udhaifu wa kuzijibu ndiomaana unaona kama itakuwa ngumu kwa mashabiki hao kukubaliana na Zitto pindi atakaporubusiwa ndani ya umoja huo.

Hivi unadhani mchango wa Zitto hautakiwi kiasi hicho ndani ya siasa za upinzani? Hebu angalia watu walivyoungana pamoja ktk sakata la Escrow bila kujari tofauti zilizokuwapo, na tunaambiwa Mpaka Zitto alialikwa kwa mara ya kwanza ndani ya kamati ya UKAWA. Je mashabiki na madie hard wa Ukawa walichukua hatua gani? Ondoa shaka mkuu ktk siasa kwa watu wanaoijua vizuri siasa hakuna adui wala rafiki wa kudumu kikubwa ni kuitumia fursa kadiri inavyopatikana.

Nikija kwenye hitimisho lako mkuu, mimi naweza kusema kwamba sikubaliani na wewe. Mimi naona UKAWA wamkubalie Zitto endapo kweli ataomba kujiunga ndani ya UKAWA. HII NI KWASABABU YA UMUHIMU MKUBWA WA UCHAGUZI HUU UNAOKUJA. Unajua mpaka sasa Act hawaeleweki vizuri, lakini utakapofika uchuguzi ndipo madhara ya hawa mabwana ijapokuwa hayatakuwa makubwa, lakini maumivu ni maumivu tu yawe ya ngumi, rungu au kuchanwa na wembe. Hawa jamaa ni Domo la Mamba lilotegeshwa Ziwani, hawa watawapokea wagombea wote wa UKAWA na ccm watakaotemwa na vyama vyao. Hebu chukulia mfano mdogo tu kama jimbo la Kyela tunaambiwa watiania wa ubunge wako zaidi ya Therathini, hawa wote wanang'ang'ania nafasi moja, hivi unadhani hawa wotewakishindwa kwenye kura za maoni watakubali tu na kurudisha nya majeshi? Hapa ndipo lile domo lililotegeshwa litafungiliwa na kuchukua hawa, iwe kwa kujishawishi au kushawishiwa na ccm ili kugawa kura za upinzani. kwa mimi binafsi kama kuna madhara ninayoyaona hapa ni haya.

Na kama hali ikiwa hivyo then hapo mwakani hatutakuwa tukiangalia "makovu" ya vidonda, bali tutakuwa tukiuguza vidonda vibichi kabisa..!! Na muda wa kuwahusisha hawa hatutakuwa nao tena. Wala hakuna atakayekuwa akitamani tena siasa za umoja wa vyama.

Tafakari.

BACK TANGANYIKA

zitto hana wanachama wasio wafuasi wa ccm kwa hiyo ujio wake UKAWA utaongeza just mtu mmoja
kwenye upigaji kura ZZK hawezi ipigia UKAWA hata akiwa mwana-ukawa....ataipigia CCM anakoshibia
 
Mkuu sana respect wa boda salam,

1. Katika red color;
Kama kiongozi wa chama hana madhara yeyote, na anaihitaji UKAWA kwa sasa ili aweze kuaminika kwa wananchi basi hilo ni tatizo lake BINAFSI na kama kiongozi wa chama chake na sio tatizo la "wananchi" na UKAWA kwa upande mwingine. Kwa logic tu ya kawaida mkuu respect wa boda, hatakuwa na madhara hapo usoni wakati wa uchaguzi kwani kama kila uchao nguvu zinapungua, jua kufika uzeeni hata kuwa na nguvu kabisa hata za kusimama (wakati wa uchaguzi), Kama ni swala la kuwapokea waliokatwa majina nadhani watatimkia CUF NCCR au chama kingine chenye kufahamika kwa wananchi, kama itatokea kutimkia ACT basi ni kule Kigoma ambapo wanaweza kushinda lakini sitegemei Kyela, Namtumbo, Mpwapwa au Arusha mjini!

2. Blue.
Hakuna tathimini ya kisayansi (evaluative research) iliyofanywa kuonesha kuwa Zitto ananguvu za kuinyima UKAWA ushindi, kinachoonekana ni watu kutaka kusikia atasema nini juu ya mgogoro wake na CHADEMA, wengi wa wahudhuriaji ni watu wenye kiu ya mabadiliko ambao tayari ni wanazi wa wapinzani, ningeona umuhimu wake kama tungepata walau kuona anavuna wananachi wengi kutoka chama tawala. Hivyo hata akiwa huko ACT bado kura zake zitaipunguzia au zitainyima CCM ushindi.

3. Fire brick.
Hembu mkuu tufikiria mfano huu. Zitto na chma chake wamijiunga ukawa, wakati wa kampeni kuna kila dalili ya UKAWA kuchukua kombe, mara anasikika Mh. Mwigulu, Nape na viongozi wakubwa wa serikali na CCM wakaanzisha propanganda na kukiri kuwa Zitto ni mtu wetu, tumemtumia katika 1, 2, 3, na hata sasa tupo nae bega kwa bega wananchi ukawa ni sawa na CCM hiyo hakuna haja ya kuwapa nchi na bla bla kibao! Vipi madhara za propaganda za namna hii kwa walio wanazi wa CUF, CHADEMA na NCCR? Vipi kwa mwananchi aliyekuwa katika msimamo wa kati?. Tambua tunauelewa tofauti na tunatofautiana katika kuinterprate issues. Nadhani hizo ulizozitaja zilikuwa kubwa lakini zilitolewa wakati ambao si wa manufaa kwa CCM. Imagine zingekuwa wakati wa uchaguzi(ref. issue ya CUF 1995 AU 2000 JUU YA UDINI NA VISU VYA MAHITA)

4. Green.
Wasimwamini mara ngapi mkuu? Watu walishajua anamatatizo hawezi kufanya kazi katika mtindo wa teamwork, ameprove failure! haihitaji muda zaidi ili wananchi wajue umimi na political arrongancy the buddy has! Hihitaji kuumwa na nyoka mara mbili ili kutambua madhara ya nyoka, only the first bit itakupa picha madhara ambayo mdudu huyo anaweza kukusababishia. Nikupe mfano kidogo, wakati anaondoka CHADEMA, kungekuwa na madhara makubwa sana kama isingekuwa ujuvi wa kisiasa na kimkakati wa viongozi wa CHADEMA. Walijiingiza sana katika issue ya kuimarisha UKAWA, kelele, majadiliano katika media na social network ikawa juu ya UKAWA kama kivuli za kuzima shida zilizojitokeza baada ya kutimuliwa. Je umejaribu kufikiria kama kusingekuwa na spinning hiyo ya chadema KATIKA ukawa athari za kuondoka kwake zingekuwa kubwa kiasi gani?

5. Purple
Umuhimu wa vyama vilivyounda CORD si wakudhaulika hata kidogo, pamoja na kushindwa katika kiti cha urais, bado waliongeza idadi ya wabunge na maseneta katika vyombo vyao vya kutunga sheria wenda kila chama kama FORD KENYA, kingesimama pekee na kuiachia JUBILEE pekee wasingepata idadi hiyo wa wawakilirishi.

Kifupi mkuu respect wa boda, kwangu mie, sioni kama kuna umuhimu wa ulazima wa kuwaingiza kundini ACT, Lakini iwapo UKAWA wataamua kuwaincoparate hao wajamaa wanao watusi na kuwadharau waliberali na wasocial democracy sina tatizo kwa kuwa kwangu mimi nimuumini wa kufanya maamuzi basing on my understanding and my counscious.
Pole kwa kukulazimisha kusoma maneno meengi.

Last edited by a moderator:
HAKUNA KUPOKEA WASALITI! Mmeona UKAWA inazidi kunawiri na mbinu zote za kuivunja zimeshindikana sasa ndio mnataka kujipenyeza ili ukifika wakati wa uchaguzi muuze majimbo na kufanya usaliti wa kila aina kama mlivyozoea! Mlikuwa mnajiona wenye akili na kupewa kichwa na CCM mlipokuwa ndani ya upizanzani sasa mmetoka hamthaminiwi tena wala hamsaidiwi tena ndio manataka kuja na mbinu ya kijinga mkifikiria watanzania wote wana akili fupi kama nyinyi! Mmegonga mwamba na mtaula wa chuya!

Mkuu waambie hao! Sijui wamekula maharage ya wapi hao!
 
Kuchokoa ni kuchokoza. Ni kukera na kumpotezea umakini anayekerwa. Haihitajiki darubini wala microscope kuona kuwa ACT hawatakiwi UKAWA. Kiongozi wao Mkuu alishawaita UKAWA wasakatonge. Leo wamekuwa wema? Unafiki tu

Tena,UKAWA imeundwa kimkataba. Mkataba ulisainiwa hadharani Jangwani na CHADEMA,CUF,NCCR-Mageuzi na NLD. ACT itajiungaje kiholela bila kusaini mkataba? Nani yuko tayari kurudi kusaini ili kuwapokea ACT? Acheni chokochoko za unoko.

Kama mna nia,sababu na uhitaji wa umoja,jiungeni na TLP,DP,TADEA,CCK na wengineo. Tafadhali, wapeni nafasi na utulivu UKAWA wajipange. Acheni chokochoko!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha)
 
Mh. Lema aliwahi kusema, nanukuu, "ni heri simba wakali mia walioko nje kuliko nyoka mdogo aliyeko ndani", mwisho wa kunukuu. Leo hii baada ya kutupwa nje huko amejidhihirisha sio nyoka mdogo tena, bali chatu mkali mla watu halafu mwazungumzia kumkaribisha tena ndani!? UKAWA wajaribu wakione cha moto!
 
Ahsante sana Mkuu. Chama kiko ICU hiki sasa wanatafuta uhai kupitia UKAWA. Walijiona wao ndio wao na yule mama kupiga marufuku wanachama wao kuunga mkono UKAWA, sasa imekula kwao, wanahaha huku na kule UKAWA sasa wamekuwa wema/wazuri.

Kuchokoa ni kuchokoza. Ni kukera na kumpotezea umakini anayekerwa. Haihitajiki darubini wala microscope kuona kuwa ACT hawatakiwi UKAWA. Kiongozi wao Mkuu alishawaita UKAWA wasakatonge. Leo wamekuwa wema? Unafiki tu

Tena,UKAWA imeundwa kimkataba. Mkataba ulisainiwa hadharani Jangwani na CHADEMA,CUF,NCCR-Mageuzi na NLD. ACT itajiungaje kiholela bila kusaini mkataba? Nani yuko tayari kurudi kusaini ili kuwapokea ACT? Acheni chokochoko za unoko.

Kama mna nia,sababu na uhitaji wa umoja,jiungeni na TLP,DP,TADEA,CCK na wengineo. Tafadhali, wapeni nafasi na utulivu UKAWA wajipange. Acheni chokochoko!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha)
 
Amma kwa hakika sijapata kuona watu ambao wana muono mfupi zaidi ya bavichaa.

Wanakifanya 'exactly" kile ambacho ACT wamekitarajia kwa kuandika hiyo barua.

Hiyo barua imewakuza ghafala ACT na kuwa "on the par" na vyama vya zamani vinavyfanya umoja wa UKAWA.

Hii ni mbinu nzuri sana ya kisiasa walioitumia na aliyeifikiria hiyo mbinu huko ACT, kama ni yule mama, basi ana kichwa kizuri sana na nnampa pongezi za dhati.

Bavichaa mnapigwa mabao kutumia nguvu zenu wenyewe na kichama kiduuuchu. Amma kwa hakika hii inazidi kuyakinisha kuwa chadema kwa sasa inaongozwa na akili ndogo.
 
Chanzo: Habari247

MYTAKE:
1) yaani mbwembwe zote zile za zitto na wenzake kuzunguka nchi nzima wameambulia wanachama 700 tu??? hata kura za kata moja hawajafikisha?? huu sasa utani....ndio maana zzk amekata tamaa na ziara ya pili???

2) Kwani kiongozi Mkuu zitto sialisema Ukawa ni wasakatonge??? na yeye anataka kujiunga na wasakatonge ???

3) Huyu mama sialisema "Nimarufuku Mwana Act kushabikia Ukawa"???

.....................
Professor kilaza.

Katika siasa hakuna rafiki wala adui wa kudumu. Kwa hapa tulipofika wapinzani hawapashwi kugawana kura wao kwa wao. Adui namba moja wa wapinzani wote wenye lengo moja ktk nchi hii lazima awe CCM. Biblia inasema nanukuu "mitume walimwendea Yesu wakamwambia, tumemkuta mtu mmoja anahubiri na kutoa pepo kwa jina lako tukamzuia asifanye hivyo, Yesu akawauliza, kwa nini mmemzuia, wakasema tumemzuia kwa sababu anahubiri kwa jina lako wakati hafuatani na sisi. Yesu akawaambia msimzuie kwa sababu asiye kinyume chetu yu upande wetu. Kama ACT wana nia njema wasizuiwe kwa sababu wale wasio kinyume cha UKAWA wako upande wao. Siku zote umaoja ni nguvu na utengano ni udhaifu
 
Amma kwa hakika sijapata kuona watu ambao wana muono mfupi zaidi ya bavichaa.

Wanakifanya 'exactly" kile ambacho ACT wamekitarajia kwa kuandika hiyo barua.

Hiyo barua imewakuza ghafala ACT na kuwa "on the par" na vyama vya zamani vinavyfanya umoja wa UKAWA.

Hii ni mbinu nzuri sana ya kisiasa walioitumia na aliyeifikiria hiyo mbinu huko ACT, kama ni yule mama, basi ana kichwa kizuri sana na nnampa pongezi za dhati.

Bavichaa mnapigwa mabao kutumia nguvu zenu wenyewe na kichama kiduuuchu. Amma kwa hakika hii inazidi kuyakinisha kuwa chadema kwa sasa inaongozwa na akili ndogo.

You're a political genius, NOT.
 
zzt tunajuwa uwezo wako wa kuchapa kazi,hachana na wanasiasa wa majukwaani,wasiokuwa na tija kwetu, miaka kenda bungeni lakini hakuna lolote zaidi ya mipasho tu isiyotusaidia sisi masikini
 
Zitto anaweweseka ccm b na ukawa wapi kwa wapi ajiunge na ccm kubwa waanzishe ukawa yao
 
wewe inaelekea hujitambui, UKAWA ilianzia kwenye issue kubwa sana ya kitaifa, unapoongelea katiba ya taifa letu unaweka uadui pembeni na manapigania maslahi ya nchi kwa pamoja, huo ndio uliokuwa msingi wa kuanzishwa ukawa, wakati ule walipigania maslahi mapana ya nchi na kwa kupitia bunge hilo la katiba ndipo waligundua kumbe wao ni wamoja na adui yao ni ccm na vibaraka wake, na wakaona ili kuja kulipa katiba bora taifa hili yawapasa kuungana kuitoa ccm madarakani na ndipo wafanye mapinduzi ya kweli kiuchumi na kijamii, kwa hiyo ndugu usikariri na kutoa tafsiri mfu hapa, fikiri kwa makini na uje na hoaja.

Walipowaita Cuf kuwa ni Ccm B je,walikuwa na maana gani kipindi hicho kama sio Cuf ni kibaraka wa Ccm? Ndiyo maana nasema Ukawa ni muungano wa wenyewe hao viongozi hivyo usishangae utakapoona ACT nao wamejiunga Ukawa,wewe tulia tuli tu kama ulivyotulia baada Chadema na Cuf kujifanya kungana na bila kupewa ufafanuzi wa uccm B wa Cuf umeishaje wala yale maneno ya Lipumba aliyoyaongea msikitini kuhusu Chadema nayo yaliishaje.
 
Mkuu habari,

Hii hoja unamwelekezea nani? Mwanachama wa ACT siyo? Ila kwa bahati mbaya umeniquote mimi..!! Wenzako kabla ya kupanua mdomo na mbavu, hupanua kwanza akili. Na kama ungelijaaliwa akili kidogo tu kiasi cha kujaza kizibo cha soda, ungefuatilia michango yangu hapa Jukwaani na hapa ungekuwa unapanua mbavu na kinywa kwa amani kabisa..!!!! Pole kwa hilo

Hivi umepata wasaa wa kusoma nilichokiandika? We ni kupakachuka tu utafikiri Mipakacha ya kule Lindi, au umetokokea huko? Tuliza akili, kama unataka kuwa mchambuzi bora hapa tuliza mshono, kaa chini tafakari wenzako wanajengaje hoja, Wanahitimishaje na kuwasilishaje. Siyo kuropoka tu utafikiri umekula Mlenda usio na bamia wala Magadi kule Hanseketwa..!!!!

Tuliza mshono jenga hoja usikike.

Hivi nikikuuliza kwa hivi sasa UKAWA ni jambo gani litakalofahamika kwa ccm litavunja nguvu za umoja huo kuelekea uchaguzi mkuu utanijibu? Hivi wewe hapo propaganda gani ambayo kwa fikra zako yaweza kuugawanya na kuusambaratisha UKAWA? Kama ccm walishindwa kwa propaganda mbaya za Udini, Ukanda, Ukabila na Ugaidi lipi laweza kuwashawishi wananchi wakubaliane na Ccm na serikali yake chovu dhidi ya UKAWA?

Narudia, Jenga hoja usikwaze watu.

BACK TANGANYIKA

Kampeni yako ni ya kitoto sana. Unafikiri watu wote wana akili fupi kama ya kwako hivyo ''utawachota''. Umenoa!
 
Katika siasa hakuna rafiki wala adui wa kudumu. Kwa hapa tulipofika wapinzani hawapashwi kugawana kura wao kwa wao. Adui namba moja wa wapinzani wote wenye lengo moja ktk nchi hii lazima awe CCM. Biblia inasema nanukuu "mitume walimwendea Yesu wakamwambia, tumemkuta mtu mmoja anahubiri na kutoa pepo kwa jina lako tukamzuia asifanye hivyo, Yesu akawauliza, kwa nini mmemzuia, wakasema tumemzuia kwa sababu anahubiri kwa jina lako wakati hafuatani na sisi. Yesu akawaambia msimzuie kwa sababu asiye kinyume chetu yu upande wetu. Kama ACT wana nia njema wasizuiwe kwa sababu wale wasio kinyume cha UKAWA wako upande wao. Siku zote umaoja ni nguvu na utengano ni udhaifu

Katika siasa KUNA adui wa kudumu na rafiki wa kudumu! Adui wa kudumu ni ufisadi, dhulma na usaliti. Na rafiki wa kudumu ni haki, ukweli na bidii ya kazi. ATC ya Zitto wanaangukia kwenye ''maadui wa kudumu'' kwani ni wasaliti, waongo na wanashirikiana na mafisadi!
 
Back
Top Bottom