Nsanzagee
JF-Expert Member
- Jun 28, 2023
- 1,940
- 4,127
Heko Hayati JPM kwa uamzi huu ambao hukusikiliza kelele za wachumia tumbo na wanasiasa wajaza tumbo, kwao nchi badaye ila tumbo ndio kipaombele chao.
Miongoni mwao mwa wanaohitajika kufika kwa pilato ni, Waziri Nape na Waziri January Makamba, hawa ndio walikuwa msitari wa mbele kama wanasiasa kupinga mradi huu ambao ndio mwarobaini wa mgao wa Umeme nchini
Na wote waliokaa kitako kuitishia serikali ya awamu ya tano kwamba, iachane na ujenzi wa Bwawa la Umeme huko Rufiji kwa sababu kutasababisha madhara makubwa, moja wapo ni kutokunyesha mvua nchini, kwani miti itakayokatwa, inatosha kabisa kuifanya nchi yetu isiwe inapata mvua.
Kama utafiti wao ni kweli, Hizi mvua zinatokana na nini?
Naishauri Serikali, kama kweli tumedhamiria kupiga hatua za kimaendeleo, wasomi aina hii ya watu waongo kiasi kile, wachukuliwe hatua kali ili iwe fundisho kwa wasomi wengine wenye nia ya kupotosha.
Poleni watu wa Dar kwa mafuriko, watu wa Hanang'i, kule Morogoro, Geita, Mwanza n.k, Pole na hongera pia kwa Serikali kwa kuwajali wahanga wa mafuriko na kuwapatia mahitaji na vitu kadha wa kadha vya kibinadamu.
Hongera nyingi zimwendee Hayati Magufuli kwa kuwapuuza hawa wasomi njaa na kuendelea kujenga hiki kituo kikubwa kabisa nchini cha kuzalishia Umeme, si ajabu hata hao wasomi watanufaika na umeme huo
Shida yoote hii huwenda inasababishwa na wasomi waongo, wachumia tumbo, kwa kuwa wamekuwa wakifanya tafiti za kiulaghai bila kizingatia masilahi ya nchi yetu kwanza.
Mungu ibariki TANZANIA